MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI.
SOMO: ZABURI 46:1.
Biblia inatuakikishia kwamba Mungu wetu ni “Msaada wa karibu.” Maanake ni kwamba Mungu wetu yu karibu nasi. Hivyo, kwa sababu Mungu yu karibu sana yeye yuko tayari kutusaidia kwa nguvu zake na neema yake.
Maisha yamejaa nyakati za majaribu, kukosa hakika na dhaoruba za kila haina. Hakuna mtu yeyote asiyepitia majaribu na dhiki, iwe dhiki ya kifedha, kiroho, kimwili na kijamii.
Katika nyakati hizo kinachohitajika si usaidizi wa mwanadamu, lakini msaada wa Mungu.
Msaada wa MUNGU unapita nguvu za mwanadamu. Msaada wa Mungu unapatikana wakati nguvu za mwanadamu zimeshindwa na kumalizika.
Mungu ni msaada wa karibu wakati wa mateso, Maanake MUNGU yuko karibu kuingilia kati wakati tumeshindwa.
Leo, tunajifunza jinsi msaada wa Mungu unaonekana, kivutio kikuu cha msaada wa Mungu na jinsi ya kujiweka tayari kupokea msaada wa Mungu wakati wa mateso. Hebu tuone:-
MUNGU NDIYE KIINI HASA CHA MSAADA.
- Mungu pekee ndiye msaada wa karibu wakati wa mateso-Zaburi 46:1.
- Mungu hayuko mbali na watu wake, yeye yuko pale pale tunapomuomba.
- Msaada wa mwanadamu ni kidogo sana, lakini ule msaada wa Mungu hauna kipimo-Zaburi 60:11-12.
- Mwanadamu anaweza kutuacha lakini Mungu yu mwaminifu.
- Mungu anatutazama kila saa-Zaburi 121:4-5.
- Msaada wa Mungu umepandwa katika Agano la upendo wake-Isaya 41:13.
- Mungu anatusaidia kwa sababu ya upendo wake kwetu.
- Mfalme ASA aliutafuta msaada wa Mungu katika vita-2 Nyakati 14:1.
JINSI YA KUUPOKEA MSAADA WA MUNGU.
- Mwite Mungu kwa njia ya imani na unyenyekevu-Zaburi 50:15.
- Msaada wa Mungu umehakikishwa tunapomwita kwa moyo wa kweli na tunapomtegemea kabisa.
- Tembea karibu na Mungu wako-Mithali 3:5-6.
- Msaada wa Mungu ni wa hakika kwa wale wanatembea katika utii.
- Uwe mwaminifu kwa maagizo yake Mungu-2 Wafalme 4:1-7.
- Ni lazima kufuata masharti yake.
- Jihadhari sana na kutegemea njia mbili, njia zake pekee ndizo zinazompendeza-Isaya 31:1.
- Kutegemea Misri (dunia) ni kumkataa Mungu wa Israeli.
- Mfalme Yehoshaphati alipata msaada kupitia ibada ya sifa-2 Nyakati 20:21-22.
- Kwa kumtegemea Mungu, mbingu zilifunguliwa na kumpa msaada.
TABIA NA ISHARA ZA MSAADA WA MUNGU.
- Msaada wa Mungu unakuja wakati wa Mungu na hakuna kuchelewa-Habakuki 2:3.
- Msaada wa Mungu unafika tu wakati unapohitajika.
- Msaada wa Mungu ni ajabu-Kutoka 14:21-31.
- Msaada wa Mungu unavunja kanuni zote kuleta ukombozi.
- Msaada wa Mungu unaleta utukufu kwa Mungu pekee-Yohana 11:4.
- Mungu anapoleta msaada wake, sifa ni kwake pekee.
- Msaada wa Mungu unanyamazisha adui na kumpa nguvu mwenye imani-Zaburi 118:13-14.
- Danieli alipotupwa katika tundu la simba alipokea msaada wa Mungu-Danieli 6:22.
VIZUIZI VYA MSAADA WA MUNGU.
- Dhambi inavunja ushirika wetu na Mungu-Isaya 59:1-2.
- Dhambi ni kizuizi kikubwa cha kupokea msaada wa Mungu.
- Kutoamini kunakatisha msaada kutoka juu-Yakobo 1:6-7.
- Bila imani ni ngumu kupokea kutoka juu.
- Kiburi kinapigana sana na Mungu-Yakobo 4:6.
- Kukosa shukrani kunakatisha msaada kutoka juu-Luka 17:17-18.
- Tukumbuke kila wakati kumshukuru Mungu kwa mema ya jana hili tutazamie msaada wake kesho.
- Mfalme Sauli alipoteza msaada wa Mungu kwa siku ya kesho kwa kuwa alijiweka mbali na Mungu-1 Samweli 15:22-23.
FAIDA YA MSAADA KUTOKA KWA MUNGU.
- Tunapata amani katikati ya dhoruba-Wafilipi 4:7.
- Msaada wa Mungu unapoesha fedhaa na kuchanganyikiwa.
- Msaada wa Mungu unatoa ngome na mizigo na nira-Mathayo 11:28-30.
- Tunapata raha nafsini mwetu.
- Msaada kutoka mbinguni huleta maburudisho ndani ya roho zetu na kufungua milango iliyofungwa-Ufunuo 3:7-8.
- Msaada kutoka juu unatengeneza njia mahali hapana njia.
- Msaada kutoka juu inaweka nguvu hatima-Zaburi 75:6-7.
- Bila msaada wa Mungu, hatuwezi kupandishwa juu.
- Kiwete aliyekaa kwa mlango hekaluni alipopata msaada wa Mungu, alipandishwa juu zaidi. Hakurudi tena pale mlangoni.
MWISHO
- Katika dunia iliyojaa changamoto msaada wa Mungu unahitajika sana.
- Haijalishi shida zako ni kubwa kiasi gani, Mungu yu tayari kusaidia wote watakaomlilia.
- Jiweke mahali pa imani, utii na unyenyekevu ukapokee msaada wa Mungu.
- Tunapotizama Mungu na kumtegemea, msaada wake ni karibu.
- Msaada wetu u katika Bwana.
The following two tabs change content below. Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.