Categories: Swahili Service

MSHALE URUKAO

SOMO: ZABURI 91:5.

 

Shetani anarusha mishale dhidi ya watoto wa Mungu kiasi awatese katika eneo moja au nyingine. Lakini kuna uhuru na ushindi mkuu kupitia kwa Roho Mtakatifu.

  • Mshale ni chombo cha kuumiza, kinacho nguvu na uwezo wa kuharibu na kuua mtu, ndege au mnyama.
  • Mishale ya kiroho ni uvamizi usioweza kuonekana kwa macho. Mishale hii inarushwa kutoka kwa ushetani na ufalme wa giza. Mishale hii inaelekezwa kwa shabaha fulani, wakati mwingine mishale ya shetani haina shabaha kamili, hivyo inaweza kukujia mara na kwa ghafla. Mungu ameahidi ulinzi na usalama kutokana na mishale ya shetani irukao mchana. Hebu tujifunze:-

AINA TOFAUTI ZA MISHALE

  • Mshale wa mauti na kifo.
  • Mshale wa mauti umetumwa kuua watu mbele ya wakati wao wa kufa- 2 Wafalme 4:18-22.
  • Watu wengi wanauliwa na mishale ya mauti. Watu wengine wanakufa katika usingizi bila kuwa wagonjwa, wengine waingia kwa ajali ya ghafla, motokaa, ndege, moto, nyumba kuanguka, mafuriko, mishale hii inatoka kwa shetani na ufalme wa giza.
  • Wakati mwingine mshale wa mauti unakaa katika mwili kwa muda mrefu, mtu anaweza kuwa hospitali kwa muda baadae akafa. Hii ni baada ya kutumia pesa nyingi kwa matibabu.
  • Tunahitaji kuliitia jina la Yesu Kristo kwa hima na moto wa Roho Mtakatifu kuvunja na kuchoma mishale ya mauti.
  • Tunahitaji kukata mauti na kifo na kuungama, “Sitakufa bali nitaishi- kwa jina la Yesu.”
  • Mshale wa dhiki.
  • Wakati mshale wa dhiki umetumwa kwa shabaha, matokeo ni dhiki, shida na mateso. Kwa kawaida mishale ya dhiki haina suluhisho ya kawaida isipokuwa kiroho- Luka 8:43-48.
  • Huyu mwanamke alikuwa na hali ambayo dawa na matibabu ya hospitali hayangeweza kutibu. Upako wa Roho Mtakatifu ndio uliweza shida yake.
  • Mishale ya dhiki ni pamoja na kifafa ya kiroho, kuanguka ovyo, Asthma, maumivu ya viungo.
  • Mshale wa kuchanganyikiwa na kutengana.
  • Mshale huu unawatenganisha marafiki wa kweli- Matendo ya Mitume 15:36-41. Paulo na Barnaba walikuwa marafiki wa dhati, lakini mshale ukawatenganisha mara moja.
  • Mshale huu unatenganisha ndoa, mme na mke bila sababu wanaachana.
  • Mshale huu unaleta machungu na dhiki. Lazima kurudisha mshale huu kwa aliyeutuma mara unapouona.
  • Jamii kutengana, ghadhabu, moja kwa mwenzako, baba na watoto, watoto na mama, kukosa umoja. Omba moto wa Roho Mtakatifu kuvunja mishale ya maumivu, chuki na kulaumiana katika jamii, kanisa na pia nchi.
  • Mshale wa kuharibu tabia (character disorder)- Yohana 13:2, 26-27.
  • Mshale huu unaharibu tabia ya mtu mwema. Mshale huu ndio ulitumwa kwa Yuda, usaliti na kukana, kupenda pesa kama jinsi Gehazi, Yuda Alexander, Vashiti- Esta 1:10-12. Mshale huu unaharibu tabia na utukufu wa mtu.
  • Mshale wa mharibu- Ayubu 1:13-19. Mshale huu ulimwingia Ayubu mara moja.
  • Mshale huu unaharibu mara moja. Mtu anapata pesa na mali lakini hajui jinsi zinakwisha.
  • Mungu ameahidi kukemea- Malaki 3:8-12.
  • Mshale wa ngome za kizazi na laana.
  • Mshale huu unaleta maovu katika familia, ugonjwa fulani unashika jamii yote, mauti na jamii mtawalia. Laana aliyopokea Gehazi ilikuwa ifuate Gehazi na jamii yake milele- 2 Wafalme 5:20, 6:1.
  • Mshale wa kuharibu hatima (destiny manipulation).
  • Mshale huu umeundwa kubadilisha mwongozo wa maisha. Waovu wanao uwezo wa kuona utukufu wa mtu au mtoto. Hawa wanatoa kikomo kwa hatima ya mtu na ndoto zake kama jinsi Yusufu na ndugu zake.

KWA NINI MISHALE HII INAFANYA KAZI?

  • Kuna sababu inayoweza kufanya mtu haraka kupokea mishale ya shetani.
  • Maisha bila kinga na ulinzi.
  • Wokovu ni kinga kubwa juu ya mishale ya shetani.
  • Lakini tunapoishi katika dhambi bila kuungama dhambi zetu, tunajiweka wazi kwa mishale.
  • Kuishi kama mkristo wa mwilini na kukosa maombi.
  • Kutovaa silaha zote za Mungu- Waefeso 6:10-13.
  • Kukosa kuelewa na mbinu za shetani na kutoelewa haki zetu kama wana wa Mungu.
  • Kukosa kuelewa na nguvu za Mungu- Luka 10:18-19.
  • Kukosa kuelewa na sheria za shetani na haki zake panapo dhambi, mali na madhabahu yake.
  • Kukata kusamehe, shida ya uchungu na dhambi- Wakolosai 3:9-13.
  • Mungu ametukataza kuishi katika chuki na watu, ghadhabu na kutosamehe.

MASHARTI YA USHINDI JUU YA MISHALE INAYORUKA

  • Damu ya Yesu ndio silaha kubwa dhidi ya mishale ya shetani- Ufunuo 12:11.
  • Funika kila jambo na kila kitu chini ya damu ya Yesu Kristo.
  • Maombi ya vita- Yakobo 5:16-18.
  • Kaa katika ushirika na Yesu Kristo- Isaya 54:17.
  • Ondoa kila mshale na kurudisha kwa mwenye kuutuma kwako.
  • Vaa silaha zote za Mungu- Waefeso 6:10-12.
  • Kata ushirika wako na Matendo ya giza.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Rev, DR. Willy Mutiso

Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Share
Published by
Rev, DR. Willy Mutiso

Recent Posts

MUNGU WA ISHARA NA MAAJABU

MFULULIZO: MJUE MUNGU WAKO. SOMO: ISAYA 8:18.   Mungu wetu ni YEHOVAH. Yehovah si Mungu…

5 days ago

DEEP CALLS TO DEEP-A JOURNEY INTO GOD

SERIES: “NEARER MY GOD TO THEE.” TEXT: PSALM 42:7.   Many believers settle for shallow…

5 days ago

THE KIND OF FAST GOD LOVES

SERIES: THE POWER OF PRAYER AND FASTING  TEXT: ISAIAH 58:3-9   God desires that we…

5 days ago

MUNGU NI MUNGU WA MABONDENI

MFULULIZO: MJUE MUNGU WAKO. SOMO: 1 WAFALME 20:23-28.   Mabonde si mahali pa kuachwa lakini…

2 weeks ago

THE SECRET PLACE: FINDING GOD’S PRESENCE

SERIES: NEARER MY GOD TO THEE.” TEXT: PSALM 91:1-2.   The secret place is not…

2 weeks ago

HOW FASTING MOVED MOUNTAINS

SERIES: THE POWER OF PRAYER AND FASTING. TEXT: JOEL 2:12.   Prayer and fasting has…

2 weeks ago