Categories: Swahili Service

MTU WA MUNGU-KIMBIA MAMBO HAYA

MFULULIZO: NIFANYE NIWE BARAKA

SOMO: 1 TIMOTHEO 6:1-16 (11)

 

Katika 1 Timotheo 6:1-11, Mtume Paulo alikuwa akinena na kijana mtumishi wa Mungu Timotheo. Lakini ukitazama kwa makini zaidi mtume Paulo anaongea na mtu aitwaye “Mtu wa Mungu.” “Lakini wewe, mtu wa Mungu”- V.11.

Kuitwa “Mtu wa Mungu” au “Mwanamke wa Mungu” ndio cheo na jina ya maana zaidi katika ufalme wa Mungu.  “Mtu wa Mungu” ni jina linalopewa mtumishi au mhubiri wa injili.

Zamani wachungaji waliitwa “mtu wa mavazi au “mtu wa vazi.” Hii ilianza wakati wa karne ya 17 wakati watumishi wa kanisa walianza kuvaa mavazi (Robes). Lakini kwa kuvaa mavazi hakuwezi kumfanya mtu kuwa “mtu wa Mungu.” Lakini jina au cheo cha kuitwa “mtu wa Mungu au mwanamke wa Mungu” ndio Daraja na cheo cha juu zaidi katika ufalme wa Mungu. Mfalme Daudi aliitwa “Mtu wa Mungu” kwa sababu alikuwa mtu ambaye moyo wake ulimwelekea Mungu. Maanake ni kwamba moyo wake mfalme Daudi ulimwelekea Mungu. Mapenzi yake Daudi, Imani yake, tamaa yake na dhamana zake zilimfuata Mungu (Values).

Mfalme Daudi anaitwa “Mtu wa Mungu” kwa sababu nia yake ilikuwa kuyapenda mambo anayopenda Mungu. Alidhamini vitu ambavyo Mungu anadhamini. Hivyo ni heshima kubwa mtu kuitwa “mtu wa Mungu au mwanamke wa Mungu.” Kuna majina mengi watu wanaitwa; kwa mfano daktari, wakili, seremala, mwalimu, profesa… lakini cheo na daraja la juu zaidi mtu aweza kuitwa “mtu wa Mungu au mwanamke wa Mungu.”

  • Musa aliitwa “Mtu wa Mungu”- Kumbukumbu 33:1.
  • Samweli aliitwa “Mtu wa Mungu”- 1 Sam. 9:6.
  • Daudi aliitwa “Mtu wa Mungu”- “2 Mambo ya Nyakati 8:14.
  • Elija aliitwa “Mtu wa Mungu”- 1 Wafalme 17:24.
  • Elisha aliitwa “Mtu wa Mungu”- 2 Wafalme 4:9.

Cheo cha “Mtu wa Mungu” “Mwanamke wa Mungu” Si jina la kujipatia bali ni jina la kuitwa na Mungu au watu walio na wakati wa kuchunguza tabia, Maisha, huduma na moyo wa mtu mbele za Mungu (Earned).

Mtu anapoingia katika jeshi si yeye anasema anataka kuwa Sajenti, Koroneli, Lieutenant au Generali, lazima kuhitimu kile cheo ili tuitwe “Mtu wa Mungu” au “Mwanamke wa Mungu lazima kuhitimu kile cheo (Earn).

Paulo anatumia neno “Mtu wa Mungu” katika 1 Tim. 6:11. Paulo anatupatia mambo tunayohitaji kufanya kuitwa “Mtu wa Mungu.” 

  • Paulo anatupa mambo ya kufanya (Vices). Matendo na ushindi wa kuitwa “Mtu wa Mungu.”
  • Leo tunajifunza mambo ya kufanya.

Hebu tujifunze:-

MTU WA MUNGU LAZIMA KUKIMBIA: (Flee)

  • Neno “kimbia” kwa “Greek” ni neno “Pheug.” Ndio tunapata neno la kiingereza (fugitive).
  • Fugitive (mkimbizi) ni mtu anayekaa katika hali ya kukimbia, kuhama hama.
  • Tunakimbia kwa sababu shetani anatukimbiza kila saa, kila siku- 1 Petro 5:8.
  • Shetani anatuwinda popote.
  • Shetani ni kama simba anaye ghuruma akitafuta kukumeza.
  • Unapoona simba utakimbia, shetani ni adui si wa kucheza naye.
  • “Mtu wa Mungu” na “Mwanamke wa Mungu ni lazima kumkimbia shetani.

MTU WA MUNGU LAZIMA KUKIMBIA DHAMBI- 1 Wathesalonike 5:22

  • “Jitengeni na ubaya wa kila aina.”
  • Dhambi ni jambo hatari sana, tunahitaji;-
  1. Kujitenga na ubaya wote.
  2. Kukaa mbali na sura yote ya dhambi.
  • Dalili zote za dhambi zinahitaji kutufanya kukimbia – “Flee.”
  • Runinga zetu zikionyesha dhambi tunahitaji kuzifunga.
  • Kompyuta yako ikileta dhambi izime.
  • Simu yako ya mkono ikionyesha dhambi unahitaji kuizima- Mathayo 18:8-9.
  • Wazazi wameacha watoto wao kucheza na Hollywood.
  • Mtu wa Mungu na Mwanamke wa Mungu lazima kukimbia dhambi.
  • Mtu wa Mungu lazima kukimbia dhambi yote- Mathayo 5:27-32.
  • Huwezi kuitwa mtu wa Mungu au mwanamke wa Mungu ikiwa kila wakati unatamani dhambi.
  • Kule Amerika kuna mji unaoitwa Las Vegas “mji wa dhambi.” Watu wa mji huu wanao msemo, “kinachofanyika Las Vegas kinakaa au kinaachwa Las Vegas.”
  • Lakini hiyo si kweli kinachofanyika Las Vegas kinaenda na mtu mpaka kwake.
  • Akili zetu ni kama jinsi kompyuta zinarekodi chochote tunachotazama.
  • Kuwa mtu wa Mungu lazima kuikimbia dhambi.
  1. Kimbia kiburi- Wagalatia 6:14.
  2. Kimbia uchafu wote- Hesabu 5:1-4.
  3. Kimbia wenye dhambi- Walawi 13:45.
  4. Kimbia dhambi za wengine- 1 Tim. 6:5.
  5. Wakimbie wanaoleta mgawanyiko katika wandugu- Warumi 16:17.
  6. Jitenge na watu waitwao ndugu lakini hawana msimamo kamili- 2 Wathesalonike 3:6, 2 Yohana 10-11.
  • Ikiwa utaitwa mtu wa Mungu au mwanamke wa Mungu, kimbia ubaya wote.
  1. Kimbia watu ambao hawatosheki- 1 Tim. 6:6-8.
  • Huwezi kuwa mtu wa Mungu ikiwa hutosheki.
  1. Lazima kukimbia tamaa mbaya- 1 Tim. 6:9.
  • Alexander the Great hakutosheka hata baada ya kuimiliki dunia yote, bado alipenda zaidi. Alikufa katika hali ya ulevi.
  • Hannibal baada ya kujaza gunia na pete za dhahabu kutoka kwa wafalme aliowashinda, baadae alimeza sumu akafa. Hakuna mtu aliye mwomboleza Hannibal.
  • Julius Caesar (kaisari) alipaka mavazi yake damu ya milioni moja ya adui zake aliowaua. Baada ya kushinda vita katika miji 800 aliuawa na rafiki wake wa karibu.
  • Napoleoni baada ya kumiliki ulimwengu wote kupitia vita baadae alikufa peke yake katika kisiwa cha St. Hellena katika uamisho.
  1. Lazima kukimbia tamaa ya fedha- 1 Tim. 6:10. Tuweze kuwa mtu wa Mungu.

MWISHO

  • Kuwa mtu wa Mungu au Mwanamke wa Mungu, lazima kuikimbia dhambi na tamaa na kila ishara ya dhambi.
  • Ee Bwana nifanye kuwa baraka.
  • Je, wewe ni “Mtu wa Mungu?”
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Rev, DR. Willy Mutiso

Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Recent Posts

MSAADA WA MUNGU WAKATI WA MATESO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: ZABURI 46:1.   Biblia inatuakikishia kwamba Mungu wetu ni “Msaada…

2 weeks ago

GOD GUIDES OUR DESTINIES.

SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: PROVERBS 3:5-6.   Every destiny is a divine…

2 weeks ago

PUT OFF AND PUT ON

SERIES: THROUGH THE BOOK OF COLOSSIANS. TEXT: Colossians 3:5-10   We have put off the…

2 weeks ago

GOD OF THE BREAKTHROUGHS

SERIES: THE GOD WE SERVE TEXT: 2nd SAMUEL 5:17-20   Breakthroughs are divine interventions that…

4 weeks ago

WHO IS SPEAKING TO YOU?

SERIES: DRAWING NEAR TO GOD TEXT: LAMENTATIONS 3:37 It reminds believers that God's word alone…

1 month ago

CHECHEA MSHINDI ALIYE NDANI YAKO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: 1 YOHANA 5:4.   Wakristo wengi wanaishi maisha ya kushindwa…

1 month ago