Categories: Swahili Service

MTU WA MUNGU LAZIMA KUPIGA VITA

MFULULIZO: NIFANYE NIWE BARAKA

SOMO: 1 TIMOTHEO 6:11-16

 

Tumeona katika mfululiza huu wa “nifanye kuwa baraka” kwamba cheo cha juu zaidi na heshima ya juu zaidi katika ufalme wa Mungu juu ya mtu katika maisha haya ni kuitwa “mtu wa Mungu” au “mwanamke wa Mungu.” Lakini si kila mtu anao mawazo hayo. Kuna watu wanapenda kuitwa:-

  • Mfanya biashara mashuhuri.
  • Mwanariadha shupavu.
  • Mwenye kutumbuiza mkuu.
  • Meneja mkuu.
  • Rais, fundi mkuu, mwanasiasa n.k.

Lakini watakapo simama mbele za Mungu mbinguni, watapenda sana kuitwa “mtu wa Mungu” au “mwanamke wa Mungu.”

Mtu wa Mungu anajulikana kwa mambo matatu:-

  1. Mtu wa Mungu anaikimbia dhambi.
  2. Mtu wa Mungu anafuata haki, utauwa, imani, upendo, subira na upole (righteousness, godliness, faith, love, patience and meekness).
  3. Mtu wa Mungu anapigana vita vizuri vya imani.
  • Je, wewe unapotembea barabarani, watu wanasema wewe ni nani?
  • Kila unapotembea mbele ya watu, mara wanapokuona tu kuna kitu wanafikiri kukuita.
  • Hata ikiwa ni kwa jina tu unapoitwa jina watu wanasema kitu kukuhusu. Kwa mfano-
  • Bill Clinton-(Monica Lewinsky.
  • Elvis Pressley-mwimbaji.
  • Michael Jordan-basketball.
  • O.J Simpson-muuaji.
  • Riggy G. Gachagua-mlima.
  • Linturi-mbolea fake.
  • Kalonzo Musyoka-
  • Rais Ruto-Zakayo.
  • Tunahitaji jina lako linapotajwa watu waseme, huyu ni mtu wa Mungu au mwanamke wa Mungu.
  • Paulo alipofikiri juu ya Timotheo alimwaza kama mtu wa Mungu. Hebu tutazame:-

JE, TIMOTHEO ALIKUWA NANI?

  • Timotheo alipokea waraka (barua) mbili katika Agano jipya kutoka kwa mtume Paulo.
  • Timotheo alikuwa mwana wa baba Mgiriki na mama Myahudi.
  • Timotheo alimpokea Yesu Kristo na kuokoka katika ujana wake.
  • Timotheo mama yake alikuwa Eunike na nyanya yake aliitwa Loisi.
  • Alipoitwa kwa huduma Timotheo alikuwa kijana wa miaka 21.
  • Timotheo alikuwa na imani timilifu, imani hii timilifu pia ilikuwa imani ya mama yake Eunike na nyanya yake Loisi-2 Tim. 1:1-5.
  • Paulo anamwita huyu kijana mtu wa Mungu.
  • Katika ujumbe wa leo, tunaona kuna vitu ambavyo tunahitaji kupigania.
  • Vita si kitu tunachofundisha kwa wakristo lakini hili tuwe watu wa Mungu kuna vita vya kupigania-1 Tim. 6:11-12.

PIGANA VITA NZURI YA IMANI-1 Tim. 6:11-12.

  • “Pigana” katika Kigiriki ni “agonizou” kiingereza ni “agonize” struggle, battle contend, fight for a prize.
  • Maanake ni kupigana vita, kushindania zawadi, kung’ang’ania kitu.
  • Kuna watu wanaopenda vita sana, wanaenda wakitafuta vita.
  • Kuna watu wanapenda vita sana kuliko chakula.
  • Upande mwingine kuna watu hawapendi vita, hawa hawajapigania chochote katika maisha yao.
  • 1st Timotheo 6:12, Biblia inasema “pigana vita vizuri vya imani.” Shika uzima ule wa milele uliotiwa ukaungama maungamo mazuri mbele ya mashahidi wengi.”
  • Tazama mambo mawili katika kifungu cha 12.
  1. Vita vya kiroho “vita nzuri.”
  • Vita vya imani ni vita nzuri.
  • Hili mema yapatikane ni lazima mtu kupigana.
  1. “Shika uzima ule wa milele.”
  • Wale waendao mbinguni lazima wapigane katika safari ya kwenda mbinguni.
  • Hawapigani hili waokoke lakini kwa sababu tayari wamekwisha okoka.

Je, vita vizuri vya imani ni nini?

  1. Lazima kuipigania imani yetu-Yuda 3-4.
  • Lazima kuipigania imani iliyokabidhiwa Watakatifu mara moja tu.
  • Kuna wale siku hizi wanapigana sana kwamba Yesu Kristo alizaliwa na bikira-Mathayo 1:23.
  • Lakini kama Kristo hakuzaliwa na bikira basi hatuwezi kuokolewa.
  • Lazima kusimama na kupigana wakati imani yetu inaaribiwa.
  • Kupigania imani yetu ni pamoja na kuamini neno la Mungu na ahadi za Mungu-Waebrania 10:23.
  • Paulo anatuimiza kuitetea ile imani na kuishi ile imani-Wafilipi 4:1; 1 Wathesalonike 2:15.
  • Katika kanisa la kwanza:-
  • Wakristo waliomba tofauti.
  • Wakristo walihubiri tofauti.
  • Wakristo waliongea tofauti.
  • Wakristo waliishi tofauti.
  • Lakini leo mambo ni tofauti sana.
  • Leo watu hawaokoki, kanisa hakuna mwaliko.
  • Leo wakristo wengi ni wadhaifu sana.
  • Leo kutembelea washirika ni lazima kuwapigia simu kwanza hili “wajipange.”
  • Leo wengine wanafundisha hyper-calvinism!! Hyper Calvinism ni kufundisha- wanaookolewa ni wale wamechaguliwa-limited salvation.
  • Lakini Yesu aliwafia wote, damu ya Yesu Kristo ni kwa wote, “atakaye na aje” ndio ahadi.
  • Ni lazima kuipigania imani yetu.

LAZIMA KUPIGANIA IMANI KATIKA NYIMBO ZA KANISA.

  • Nyimbo za Injili lazima kuwe kwa mizani ya neno la Biblia.
  • Pia masomo ya Biblia yanayo fundishwa katika shule zetu ni mbali sana na imani yetu (comparative religions).
  • Nyimbo nyingi za Injili zimetolewa kutoka kwa vitabu vya nyimbo.
  • John Wesley wa Charles Wesley wakilishi wa kanisa ya Methodist waliandika zaidi ya nyimbo 500. Nyimbo zao zilienda pamoja na Biblia. Nyimbo kama:-
  1. Sioshwi dhambi zangu, bila damu.
  2. There is a fountain filled with blood (damu imebubujika.
  • Ni lazima wimbo wa Injili kutaja Yesu Kristo, damu ya Yesu, msalaba, kufufuka, kupaa, kurudi tena, Roho mtakatifu, Mungu baba, dhambi, jehanamu, mbinguni, kuokoka.
  • Ni lazima kuangalia dance tunaoleta kanisani (ndombolo-haiwezi kuwa ya Yesu Kristo).
  1. Lazima kupinga sana Injili inaofundisha “kila mtu ataenda mbinguni” kila njia, na kila dini ni njia ya mbinguni.
  2. Lazima kupinga vikali kwamba kila mtu amekufa amepokelewa mbinguni.
  • Lazima kupinga mafundisho ya kwamba kila mtu ni mtoto wa Mungu-Yohana 8:44.
  1. Lazima kupinga mafundisho kwamba kuna njia nyingi kwenda mbinguni-Yohana 14:6.

JE, KUNA IMANI NGAPI?

  • Biblia inafundisha imani ni moja, Bwana mmoja, ubatizo moja-Waefeso 4:5.
  • Mbinguni kunaenda wale wameokoka pekee.
  • Lazima kupigania imani juu ya Biblia.
  • Tafsiri nyingi za Biblia ni za kishetani, maana zinakataa:-
  • Yesu alizaliwa na bikira.
  • Yesu Kristo ni Bwana.
  • Yesu yuarudi tena katika mwili.
  • Yesu amefufuka kutoka kwa wafu.
  • Yesu alipaa mbinguni.
  • Utatu wa Mungu.
  • Tafsiri za Biblia ni mbili:
  1. Thought for thought-wazo kwa wazo.
  2. Literal translation.
  • Hii ya pili ndio sawa.
  • Leo kuna Biblia nyingi sana.
  • Biblia ya walawiti (homosexuals).
  • Biblia ya Mormons.
  • Biblia ya mashahidi wa Yehova.
  • Biblia ya catholics (St. Joseph Catholic Bible).
  • Biblia ya wanarika (Teens Slimline Bible).
  • Biblia nyingi leo, zimeacha Kristo, Bwana, Yesu, Mungu, utatu wa Mungu, Lucifer, shetani, jehanamu, mbinguni, hukumu, damu, wokovu, neno la Mungu, neno la Bwana, Bwana Yesu Kristo.
  • NIV, imeacha maneno muhimu 5,219.
  • NASV, imeacha maneno muhnimu 3,561.
  • NRSV, imeacha maneno muhimu 3,890.
  • RSV, imeacha maneno muhimu 6,985.
  • Living, imeacha maneno muhimu 17,003.

Lazima kupigania neno la Mungu.

LAZIMA KUPIGANIA MAUNGAMO YETU-1ST TIM. 6:12.

  • Wote waliokoka wana ungamo (profession of faith).
  • Ni lazima kuungama Yesu Kristo ni Bwana wa maisha yako.
  • Timotheo aliungama maungamo mema mbele ya watu wengi.
  • Kristo aliungama maungamo mazuri mbele ya Potio Pilato.
  • Tunaungama pamoja na mavazi yetu, mazungumzo yetu, maisha yetu, vitabu tunavyosoma vipindi tunavyo tazama.

MWISHO

  • Mtu wa Mungu lazima kukimbia dhambi.
  • Mtu wa Mungu lazima kufuata haki, utauwa, imani, upendo, subira na upole.
  • Mtu wa Mungu lazima kupigania imani yake.
  • Je, wewe unakimbia, unafuata, unapigana vita?
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Rev, DR. Willy Mutiso

Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Recent Posts

MSAADA WA MUNGU WAKATI WA MATESO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: ZABURI 46:1.   Biblia inatuakikishia kwamba Mungu wetu ni “Msaada…

2 weeks ago

GOD GUIDES OUR DESTINIES.

SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: PROVERBS 3:5-6.   Every destiny is a divine…

2 weeks ago

PUT OFF AND PUT ON

SERIES: THROUGH THE BOOK OF COLOSSIANS. TEXT: Colossians 3:5-10   We have put off the…

2 weeks ago

GOD OF THE BREAKTHROUGHS

SERIES: THE GOD WE SERVE TEXT: 2nd SAMUEL 5:17-20   Breakthroughs are divine interventions that…

4 weeks ago

WHO IS SPEAKING TO YOU?

SERIES: DRAWING NEAR TO GOD TEXT: LAMENTATIONS 3:37 It reminds believers that God's word alone…

1 month ago

CHECHEA MSHINDI ALIYE NDANI YAKO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: 1 YOHANA 5:4.   Wakristo wengi wanaishi maisha ya kushindwa…

1 month ago