Categories: Swahili Service

MTUMIKIE MUNGU MPAKA MWISHO

MFULULIZO: MUNGU NI PENDO

SOMO:   MALAKI 3:13-18

Mungu wetu yuasikia yote tuyasemayo na tunayowaza moyoni yetu. Katika  kifungu hiki cha Malaki 3:13-18, Mungu aliyasikia makundi mawili yaliyozungumza. Kundi la kwanza    lililalamika na kunungunika dhidi ya Mungu. Kundi la pili lilimwogopa Mungu na kumsifu kwa  mema aliyotenda. Mungu aliyasikia yote.

Hebu nasi tusikize walivyosema:-

I.  KUNDI LA KWANZA – WALILALAMIKA NA KUNUNGUNIKA (3:13-15)

  • Hawa watu walikuwa na malalamiko matatu kwa Mungu.
  1. “Hatukusema maneno juu yako” V.13
  • Malalamiko yao ya kwanza ni hatujasema mambaya juu yako.
  • Hawa watu kwa mara ya saba wamekataa kwamba wako na shida “tumesema nini mbaya juu yako?”
  • Mungu anawaeleza kwamba maneno yao yamekuwa magumu juu yake.
  • Hawa watu walizungumuza wao kwa wao juu ya Mungu
  • Wenye manunguniko wanapenda wenye manunguniko wenzao
  1. “Kumtumikia Mungu hakuna faida” (V.14)
  • Walisema, kutumika, kuabudu, kutoa fungu na zaka haina faida, ni bure, ni tupu.
  • Walimtumikia Mungu wakiwa na fikira ya “je, nitapata kitu gani kutumika?”
  • Watu wa Malaki walikuwa fikira moja na watu wa Isaya 58:3 na Ayubu 21:15.
  • Wengine wetu tumekataa kumtumikia Mungu kwa maaana hatuoni faida. Wengine wameishi maisha safi mbele ya Mungu lakini hatujaona faida yeyote.
  • Lakini kumtumikia Bwana kuna faida nyingi (I Wakorintho 15:58) Waefeso 2:10
  • Tumebarikiwa hili tutumike (saved to serve)
  • Tumebarikiwa hili tubarikie wengine
  • Tumeponywa hili tuwaponye wengine
  • Lakini tunatumika kwa hiari ya Bwana wala si kwa hiari yetu wenyewe (we serve at the will of God)
  1. “Mungu si mwenye haki” (V.15)
  • Malalamiko ya tatu yalikuwa “Mungu si mwenye haki”
  • Walipo tazama waliona mwenye kiburi ndio walio heri, watendao uovu ndio walio wajengwao, wamjaribuo Mungu ndio waponywao!
  • Malalamiko haya ni sawa na yale ya Asaph, katika (Zaburi 73:3-28)
  • Kwanini waovu wanapata yale yaliahidiwa watoto wa Agano?
  • Walisema kwa maana Mungu ametusahau, basi nasi tumsahau (Zaburi 73:4-5)

II.  KUNDI LA PILI: WALIMSHUKURU MUNGU NA KUTUMIKA (3:16-17)

  • Katika tabia yao—walimshukuru Bwana na kumsifu
  • Katika mwenendo wao-walisemezana wao kwa wao
  • Hawa watu walimcha Mungu (I Samweli 12:24)
  • Kumjua Mungu ni kamcha yeye na kutetemeka mbele zake (Kumbu Kumbu 5:29)
  • Kumcha Mungu ni kuelewa mambo mawili
  1. Mungu huenda akanijeruhi
  2. Pengine huenda nikamjeruhi Mungu kwa njia zangu (Wafilipi 2:12)
  • Kikundi hiki cha pili walikuwa ni mabaki ya walio waminifu mbele za Mungu
  • Walikutana mara kwa mara kutoa ushuhuda wa jinsi Bwana amewatenda (Zaburi 66:16)
  • Walishiriki, wakafungua mioyo yao na kuimizana
  • Walikutana kuungama dhambi zao, walilia pamoja na kuomba pamoja
  • Ushirika wao ulikuwa pamoja na Mungu na wao kwa wao. (Vertical and Horizontal) Mithali 13:20
  • Je, marafiki zako wanakujenga? Je, wanakupa moyo kumtumikia Bwana zaidi? (Waebrania 3:13-19)
  • Tufanye hima kumcha Mungu na kuimizana sisi kwa sisi (Waebrania 10:24-25)
  • Tunapo mtumikia na kumcha Bwana na kujengana sisi kwa sisi, basi tutafahamu mambo tano juu ya tabia ya Mungu (Malaki 3:16-17)
  1. Mungu anatusikiza na kusikia (V.16) Zaburi 33:18, 34:15
  2. Mungu anatukumbuka (V.16) kutoka 32:32, Zaburi 56:8
  • Mungu anayaona machozi yako na hofu zako zote.
  • Mungu anaandika kitabu chako na kitabu cha uzima (Ufunuo 20:12)
  1. Mungu anatudai kuwa wanawe (V.17)
  • Wanao mcha Bwana ndio watoto wake (Yeremia 32:38-41) I Wakorintho 6:19-20, I Peter 2:9
  1. Mungu anatudhamini sana (V.17) Isaya 62:3, Zephaniah 3:17)
  2. Mungu atatuwachilia (spare us) V.17 (Warumi 8:32)

MWISHO

  • Katika vikundi hizi mbili, je wewe ni kikundi gani?
  • Umeokoka hau umepotea? Huko hai katika Kristo hau umekufa katika dhambi zako? Je, wewe huko katika nuru hau katika giza, kwa ufalme wa Mungu hau Shetani?
  • Je, huko katika njia ya kwenda mbinguni hau jehanamu?
  • Je, unamtumikia Mungu hau la?
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Rev, DR. Willy Mutiso

Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Share
Published by
Rev, DR. Willy Mutiso

Recent Posts

DAMU YA UTAKASO.

MFULULIZO: AGANO LA UTAKASO. SOMO: KUTOKA 12:12-13.   Damu ya Yesu Kristo ndiyo mhuri wa…

14 hours ago

KEY TO DIVINE SPEED.

SERIES: SUPERNATURAL ADVANCEMENT. TEXT: HABAKKUK 3:19.   The journey of fulfilling your destiny does not…

16 hours ago

BE YE THANKFUL TO GOD.

SERIES: THROUGH THE BOOK OF COLOSSIANS. TEXT: COLOSSIANS 3:15   Thankfulness is a great attitude…

18 hours ago

LEVELS OF THE ANOINTING.

SERIES: THE ANOINTING. TEXT: EZEKIEL 47:1-5   There are levels of the anointing and each…

4 days ago

UMETAKASWA KUPOKEA KIBALI.

MFULULIZO: AGANO LA UTAKASO. SOMO: ESTA 2:15-18.   Kibali cha Mungu ndicho kinacho watenga watoto…

1 week ago

THE GOD WHO SHIFTS THE HEAVENS IN YOUR FAVOR.

SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: HAGGAI 2:6-9.   God has the power to…

1 week ago