Categories: Swahili Service

MUNGU ALIMGEUZA MFALME AKAWA NG’OMBE

MFULULIZO: DANIELI-MUNGU NDIYE HAKIMU.

SOMO: DANIELI 4:1-37

Kiburi cha mfalme Nebukadreza kiliongezeka na kupanda juu zaidi. Mungu alimpa mfalme Nebukadreza ndoto kama onyo. Kwa kukataa ile ndoto na kutubu dhambi yake Nebukadreza alienda kichaa na wazimu wa kuwa mnyama, akala nyasi kama ng’ombe, akatembea miguu nne, akamea ngozi kama jinsi ng’ombe, akaingia porini kama mnyama (boanthropy). Mungu alimwonea huruma na Nebukadreza akapata kuokoka. Kisa cha Nebukadreza ni kisa cha hatari za kiburi cha mwanadamu.

Kiburi kinao gharama nyingi zaidi pamoja na kuleta mauti na kifo.

Leo tunatizama mtu aliyejifikiria kuwa mkuu zaidi. Nebukadreza alijitwika mamlaka, sifa na utukufu ambao Mungu pekee anahitaji kupewa.

Hebu tuone huyu mfalme, mwana siasi ambaye Mungu alimfanya ng’ombe wa porini.

HALI YA NDOTO ALIYEOTA MFALME NEBUKADREZA.

  1. Nebukadreza alikuwa mfalme mwenye nguvu zaidi ulimwenguni.
  • Ufalme wa Nebukadreza ulitapakaa kila mahali duniani, Europa, Afrika, Mashariki ya kati, Asia.
  • Danieli alimwambia Nebukadreza kwamba Mungu alimpa utawala juu ya mataifa yote.
  • Makao makuu ya mfalme Nebukadreza yalikuwa kule Babeli.
  • Kuta za kuzingira mji wa Babeli zilikuwa futi 350, kwenda juu (grorofa 35) upana ulikuwa futi 87. Kulikuwa na ngome 250 juu ya ule ukuta. Pia kulikuwa ukuta wa pili kwa ulinzi kamili. Ilikuwa ngumu sana adui awaye yote kuingia Babeli.
  • Nebukadreza alikuwa tayari ametawala miaka 35 tangu ndoto ya kwanza. Alikuwa tayari amemiliki Misri (Afrika) na kumaliza vita vyake vyote.
  • Kama ni ulinzi na usalama Nebukadreza alikuwa salama kabisa.
  1. Ustawi wake Nebukadreza ulikuwa bila kifani.
  2. Nebukadreza alikuwa tajiri zaidi na kustawi zaidi kuliko wote duniani.
  • Nebukadreza alikuwa na mamlaka juu ya pesa zote za sadaka za hekalu ya miungu yake. Pesa zote za ushuru zilienda kwake binafsi (Ki-E-Citizen). Utajiri wake kifedha na dhahabu, mashamba na nafaka hazikuweza kuhesabika!!
  1. Lakini utajiri, ustawi na fedha ni hatari zaidi.
  • Mungu anatuonya juu ya ustawi, mali na fedha (Kumbu kumbu 8:11-18.
  • Tunapokuwa na mali nyingi ni haraka kupata kiburi kubwa na kufikiri hakuna chochote kinaweza kutuleta chini mavumbini.
  1. Tunapokuwa na ustawi na mali nyingi, tunapenda Injili rahisi, neema rahisi, tunapenda kuhubiri neema pekee bila kutubu dhambi, ubatizo bila nidhamu, ushirika bila kuungama, kukiri dhambi bila kuungama, neema bila msalaba.
  • Neema bila Yesu Kristo.
  • Lakini Mungu wetu anaamuru tukibeba msalaba ule Yesu Kristo alibeba msalaba wa kunyenyekea, kufa kila siku kwa mapenzi yetu na kuubeba msalaba wetu.

ONYO KUTOKA KWA MUNGU.

Mungu anatumia ndoto kutuonya.

  1. Mifano ya onyo kutoka kwa Mungu.
  • Yusufu na jamii walionywa juu ya njaa kubwa.
  • Yusufu alionywa na Mungu kwa ndoto juu ya Herode kumuua mtoto Yesu.
  • Mke wa pilato alionywa na Mungu juu ya Yesu Kristo.
  • Nebukadreza alionywa na Mungu kwa ndoto juu ya kiburi chake.
  • Mungu anatuonya hili tusitende dhambi.
  1. Mungu ni mwenye huruma anatuonya hili tusifanye dhambi.
  • Kaini alionywa asimuue ndugu yake Habeli-Mwanzo 4:6-7.
  • Abimeleki alionywa asimchukue Sara kuwa mke wake-Mwanzo 20:6.
  • Pilato asimhukumu Yesu Kristo-Mathayo 27:19.
  • Juda asimsaliti Yesu Kristo-Mathayo 26:25.
  • Petro asimkane Yesu Kristo mara tatu-Mathayo 26:34.
  • Leo pamoja na ndoto tunapata onyo kupitia neno la Mungu, dhamiri zetu, Roho Mtakatifu na pia wajumbe wa Mungu.
  1. Je, kwa nini kiburi ni dhambi kubwa?
  2. Kiburi ni mbaya kwa sababu:-
  • Kwa kiburi kerubi mkuu Lucifer alianguka dhambi-Isaya 14:12.
  • Kwa kiburi farao wa Misri aliangamia-Kutoka 5:2.
  • Kwa kiburi mfalme Uzzia alipata ukoma na mauti-2 Mambo ya Nyakati 26:16.
  • Kwa kiburi Paulo mtume alipewa muiba katika mwili wake-2 Wakorintho 12:7.

Tabia (4) nne za kiburi.

  • Kiburi kinafanya kufikiri sisi ni wema kuliko wale wengine. Kwa sababu tumesoma zaidi, tunao mali, tuwarembo zaidi, tunao akili nyingi, tumefaulu zaidi.
  • Hakuna tulionacho ambacho hatukupewa na Mungu.
  • Kiburi kinaleta faragano-Mithali 13:10.
  • Faragano ndio inaleta vita, kutengana, kuvunjika ndoa na jamii, kutengana jamii na kanisa.
  • Kiburi kitatufanya tusisuluhishe shida zetu.
  • Mwenye kiburi wanapoona tayari ndoa imevunjika.
  • Yesu Kristo anapokuwa juu ya enzi, mambo yanakuwa shwari.

Sababu Mungu alimhukumu mfalme Nebukadreza.

  • Mungu alimpa Nebukadreza Ufunuo mkuu sana kuliko Wafalme wengine katika historia isipokuwa kuna mfalme Daudi.
  • Nebukadreza alipewa Ufunuo wa historia ya ulimwengu kutoka 570BC-mpaka kurudi kwa Yesu Kristo mara ya pili-Danieli 2.
  • Nebukadreza aliona jinsi Mungu aliwahifadhi Shedraka, Meshaki na Abednego katika ile tanuri ya moto na jinsi Mungu alijidhihirisha katika ule moto.
  • Ni jambo la hatari sana kuonyeshwa na Mungu mambo makuu na kudharau Ufunuo wa neno lake.

HUKUMU YA MUNGU JUU YA MFALME NEBUKADREZA.

  1. Uzito wa hukumu ule:
  2. Nebukadreza alipoteza utu wake, akawa ng’ombe.
  3. Nebukadreza alifanyika kuwa m’baya zaidi kuliko wendawazimu. Alipoteza utu, akawa ng’ombe (boanthropy). Hukumu ilimjia baada ya mwaka.
  4. Nebukadreza angefanyika simba au dubu lakini ng’ombe, kwa miaka saba.
  5. Urejesho wake.
  • Mungu alimwonea huruma-Waefeso 2:4-7.
  • Matokeo ya urejesho ulikuwa wa Nebukadreza kumpa Mungu utukufu na sifa. Tizama ushuhuda wake mfalme Nebukadreza-Danieli 4:34-37.

MWISHO

  • Tunapodharau sauti ya Mungu kwa muda mrefu mioyo yetu inapata kuwa ngumu sana.
  • Nebukadreza alionywa na Mungu, alikataa kwa sababu ya kiburi chake.
  • Kiburi kinatufanya kukataa sauti ya Mungu anenapo. Kiburi ni dhambi kubwa sana.
  • Mungu alimpa Nebukadreza muda wa mwaka moja (miezi 12). Je, Mungu amekupa wewe miezi ngapi?
  • Je, utangoja mpaka upoteze yote ndipo utubu dhambi?-Waebrania 9:27.
  • Leo tubu dhambi, Mjie Yesu Kristo sasa.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Rev, DR. Willy Mutiso

Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Recent Posts

MSAADA WA MUNGU WAKATI WA MATESO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: ZABURI 46:1.   Biblia inatuakikishia kwamba Mungu wetu ni “Msaada…

3 weeks ago

GOD GUIDES OUR DESTINIES.

SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: PROVERBS 3:5-6.   Every destiny is a divine…

3 weeks ago

PUT OFF AND PUT ON

SERIES: THROUGH THE BOOK OF COLOSSIANS. TEXT: Colossians 3:5-10   We have put off the…

3 weeks ago

GOD OF THE BREAKTHROUGHS

SERIES: THE GOD WE SERVE TEXT: 2nd SAMUEL 5:17-20   Breakthroughs are divine interventions that…

4 weeks ago

WHO IS SPEAKING TO YOU?

SERIES: DRAWING NEAR TO GOD TEXT: LAMENTATIONS 3:37 It reminds believers that God's word alone…

1 month ago

CHECHEA MSHINDI ALIYE NDANI YAKO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: 1 YOHANA 5:4.   Wakristo wengi wanaishi maisha ya kushindwa…

1 month ago