Categories: Swahili Service

MUNGU ATAKUPIGANIA VITA

SOMO: KUTOKA 14:14

Huu ni mwaka mpya 2020. Lakini safari bado vita vya kiroho vingaliko, lakini kwa mwaka huu hebu tukamruhusu Mungu atupiganie vita. Bwana anapotupigania ushindi ni lazima. Kufahamu jinsi ya kupata ushindi ni jambo la busara sana. Kila mwana wa Mungu anaye jemedari ambaye hajapoteza vita yeyote. Katika kutoka 14:14 “Bwana atawapigania hinyo, nanyi mtanyamaza kimya.” Wengi wetu hatuna subira ya kumruhusu Bwana kutupigania, mara, tunaona kama Mungu ni mpole wa kazi.  (Isaya 63:4) tena katika warumi 12:19. kulipiza kisasi ni kazi ya Mungu. Hebu tuone njia nane za Mungu kutupigania:-

I.  BWANA ATAWASUBUA ADUI ZAKO (KUTOKA 14:24-26).

  • Wana wa Israeli walipita katika bahari ya shamu kama jinsi katika inchi kavu.
  • Wamisri waliwafuata nyuma kwa kasi sana, walikuwa na magari ya moto lakini Bwana akayatoa magurudumu ya magari yao.
  • Hata wamisri walijua ya kwamba Mungu alikuwa katika vita hivi (Kutoka 14:27-28)

OMBA

Ee Bwana naomba uwasumbue adui zangu wanaonifuata nyuma, katika Jina la Yesu     Kristo.

II.  BWANA ATATUMA MALAIKA WAKE MBELE YAKO, KUPIGANA NA ADUI ZAKO. (II SAMWELI 5:23-25)

  • Kuna wakati Mungu atamtuma Malaika wake mbele yako kupigana na adui wako.
  • Mfamle Daudi alikuwa anapanga vita na wafilisti.
  • Wafilisti tayari walikuwa wameaza vita, Daudi, alimwomba Mungu. Israeli tayari walikuwa wamewashinda wafilisti, lakini wafilisti walikataa kushindwa.
  • Malaika wa Bwana ndiye alipigana, kazi ya Israeli ilikuwa ni kupokea ushindi.

OMBA

Ee, Bwana, tuma malaika wako mbele yangu     kupigana vita vyangu, katika jina ya Yesu Kristo.

III.  BWANA ATAFANYA ADUI WAKO KUSIKIA SAUTI YA KUTISHA                   (II WAFALME 7:5-7)

  • Sauti ya magari iliwafadhaisha washamu mpaka wakakimbia.

OMBA

Ee Bwana wafadhaishe adui zangu wanaopigana nami waniache, katika jina la Kristo.

IV.  BWANA ATATUMA MALAIKA WAKE KUWAUA ADUI ZAKO (MAMBO YA NYAKATI 32:21).

  • Mfalme wa Shamu alimtumia Hezekia, barua ya kutisha, lakini Bwana alimwakikishia Hezekia ushindi mkuu.
  • Bwana alimtuma malaika wake, kesho yake jeshi lote la shamu lilikuwa maiti.
  • Mwanaye mfalme wa shamu alimuua kwa upanga.

OMBA

Ee Bwana fanya adui zangu wapigane wao kwa wao na kuuana wao kwa wao.

V.  BWANA ATAWAFANYA ADUI ZAKO KUOTA NDOTO ZA KUWATISHA (WAAMUZI 7:9-14)

  • Ndoto pekee iliweka hofu ya Gideoni katika mioyo ya wamidiani , hivyo wakaogopa na kukimbia.

OMBA

Ee, Bwana watumie ndoto za ajabu adui zangu wakanihofu sana.

VI.  BWANA ATAWAPIGA MAWE KUTOKA MBINGUNI (Yoshua 10:10-11)

  • Mungu alinyesha mvua ya mawe na ngurumo.

OMBA

Ee, Bwana nyesha mvua ya mawe na ngurumo zako juu ya adui zangu, katika jina la Kristo.

VII.  BWANA ATATUMIA NJIA ZOTE KUWAPIGA ADUI ZAKO.                          (I WAFALME 20:29-30).

OMBA

Ee, Bwana wakimbize adui zangu kwa kila njia katika jina la Yesu Kristo.

 

VIII. BWANA ATAWAFANYA ADUI ZAKO KUPIGANA WAO KWA WAO. (II MAMBO YA NYAKATI 20:17-25).

  • Kuna wakati Bwana atawatuma malaika, lakini Bwana atawafanya adui zako kupigana wao kwa wao.
  • Mungu aliwafanya adui kwenda vitani na mali zao, dhahabu na fedha! Hivyo vita vyako vitakuwa pato kwako! Ajabu

MWISHO

  • Katika vita vyangu nitamwacha Bwana anipiganie, hivyo nitatulia katika Amani – katika jina la Yesu Kristo.
  • Adui zako watakimbia na kuuana katika jina la Yesu.
  • Ee, Bwana zubaisha adui zangu, hili vita vyangu viwe faida kwangu, katika jina la Yesu. Ameni.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Rev, DR. Willy Mutiso

Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

View Comments

  • I'm really inspired together with your writing skills and also with
    the structure in your blog. Is this a paid topic or did you customize it your self?

    Anyway keep up the nice quality writing, it is uncommon to look a great blog like this one these
    days..

Share
Published by
Rev, DR. Willy Mutiso

Recent Posts

MUNGU WA ISHARA NA MAAJABU

MFULULIZO: MJUE MUNGU WAKO. SOMO: ISAYA 8:18.   Mungu wetu ni YEHOVAH. Yehovah si Mungu…

5 days ago

DEEP CALLS TO DEEP-A JOURNEY INTO GOD

SERIES: “NEARER MY GOD TO THEE.” TEXT: PSALM 42:7.   Many believers settle for shallow…

5 days ago

THE KIND OF FAST GOD LOVES

SERIES: THE POWER OF PRAYER AND FASTING  TEXT: ISAIAH 58:3-9   God desires that we…

5 days ago

MUNGU NI MUNGU WA MABONDENI

MFULULIZO: MJUE MUNGU WAKO. SOMO: 1 WAFALME 20:23-28.   Mabonde si mahali pa kuachwa lakini…

2 weeks ago

THE SECRET PLACE: FINDING GOD’S PRESENCE

SERIES: NEARER MY GOD TO THEE.” TEXT: PSALM 91:1-2.   The secret place is not…

2 weeks ago

HOW FASTING MOVED MOUNTAINS

SERIES: THE POWER OF PRAYER AND FASTING. TEXT: JOEL 2:12.   Prayer and fasting has…

2 weeks ago