MFULULIZO: DANIELI-MUNGU NDIYE HAKIMU
SOMO: DANIELI 2:1-20
Danieli alipewa na Mungu maarifa na ujuzi katika elimu na hekima. Zaidi ya hayo Danieli alikuwa na ufahamu katika maono yote na ndoto. Maarifa, ujuzi, ufahamu na hekima ndizo tunahitaji ili kupanda mpaka juu zaidi. Luka 21:15, “Kwa sababu mimi nitawapa kinywa na hekima ambayo watesi wenu wote hawataweza kushindania nayo wala kuipinga.”
Kulikuwa na uwepo na uwezo uliofanya Danieli kuwa na maarifa, ujuzi, hekima na maono. Unapopewa hekima kama jinsi Danieli, adui na wapinzani wako hawawezi kukushinda kamwe. Ni maombi yangu kwamba Mungu atupe roho ya maarifa, ujuzi, hekima, maono na ndoto tusaidiwe kupanda mpaka juu zaidi ya adui zetu katika jina la Yesu Kristo.
Leo yaweza kuwa maombi yetu ya imani kwamba tupewe roho ya maarifa, ufahamu, ujuzi, hekima, maono na ndoto za kutupandisha juu zaidi.
Katika kila kazi, biashara omba ukapewe maarifa, ufahamu, hekima, maono, ndoto za kufahamu zaidi kazi yako na biashara yako-upate kupandishwa juu zaidi ya washindani wako.
Kazi na biashara, elimu na maarifa ni ushindani unapopokea roho ya maarifa, ufahamu na hekima kutoka mbinguni basi umepaa kuliko wote.
Mungu anao uwezo wa kukufanyia hivyo ndani ya maisha yako leo.
Mungu wa Danieli ndiye tunahitaji kupaa juu kama jinsi nyota.
Mungu wa Danieli ndiye tunamwona katika Danieli 1:17, “Mungu aliwapa maarifa na ujuzi katika elimu na hekima, ufahamu wa maono yote na ndoto.
Hebu tumwone Mungu wa Danieli.
MUNGU WA DANIELI NI MUNGU WA UFUNUO-Danieli 1:17.
- Mungu wa Danieli ni Mungu wako, anao uwezo wa kukuonyesha mitihani kabla haijafanywa.
- Mungu wa Danieli anawafunulia watu wake mambo yote kabla hujafika kwa mtihani au interview.
- Mungu wa Danieli anafichua siri zote kwa wateule wake.
- Tangu jadi, tangu dunia kuwako hakuna mtu aliye na maarifa, maono na ndoto aliweza kushindwa na kitu.
- Shida kubwa leo ni badala ya wakristo wengi kuota maono ya maarifa, na hekima ya kubuni vitu, wao wanaota ndoto na kuona maono ya mashetani, majeneza, wanyama wa pori, ndoto za ngono, kifo, kaburi na misoga ya watu na ajenti!!
- Wakristo wengine wanapambwa sana na waume na wake na maroho wachafu.
- Mungu wa Danieli pekee anao uwezo wa kutupilia mbali ndoto na maono chafu na kukupatia ndoto na maono ya mbinguni, ndoto za maarifa, hekima, juu na ufahamu hili upate kupandishwa juu katika biashara, utafiti, elimu, siasi.
- Badala ya kusikiza dunia (ground) upepo na mapepo utapata maarifa ya kukuendeleza mbele zaidi.
- Mungu wa Danieli ni Mungu wa Ufunuo.
- Mungu wa Danieli anao uwezo wa kukupatia ndoto, maono, maarifa na ufahamu wa jinsi utajikomboa kutoka umasikini ambao umezorotesha jamii yenu kwa miaka elfu elfu.
- Wakati Mungu amekupa maono na ndoto zake ni wakati wa kunyamaza mpaka tamati yeke, maana shetani akijua ndoto na maono yako mapema atayavunja mara moja.
- Adui hapendi kusikia maono yako na ndoto za maendeleo, nyamaza mpaka ndoto na maono yatimie.
- Wewe, pamoja nami tunahitaji maono na ndoto za kiungu kurekebisha maisha yetu na kustawi katika maisha.
MUNGU WA DANIELI NI MUNGU MKUU, ANATAWALA JUU YA YOTE-Danieli 2:21.
“Yeye hubadili majira na nyakati; huujulu Wafalme na kuwamilikisha Wafalme, huwapa hekima, uwapa wenye ufahamu maarifa.”
- Mungu wa Danieli utawala mataifa yote.
- Mungu wa Danieli anao uwezo na nguvu na kuwainua Wafalme na kushusha Wafalme.
- Mungu wa Danieli anao uwezo na nguvu zote kuwashusha wenye majivuno ya dunia hii.
- Mungu wa Danieli anawang’oa wale wamesimama kuzuia maendeleo yako.
- Wote wanaokuzuia kupanda juu washuke chini katika jina la Yesu Kristo.
MUNGU WA DANIELI NI MUNGU ANAYEWEKA SIRI-Danieli 2:22.
“Yeye hufunua mambo ya fumbo na siri, huyajua yaliyo gizani na nuru hukaa kwake.”
- Mungu wa Danieli ufunua siri na mafumbo yote.
- Siri zote za mbinguni, duniani na kuzimu zinajulikana na Mungu.
- Mungu wa Danieli aweza kueleza kabisa hatima ya kila taifa na kila kiumbe!!
- Mungu wa Danieli anaweza kukuonyesha yote adui anakupangia katika maisha yako.
- Mungu anaweza kukufunulia wachawi na kazi zao, adui na mipango yao mpaka maneno yao juu yako.
- Sasa hivi kuna siri ya maisha yako, unahitaji kujua, mara utakapofahamu siri ya maisha yako-maisha yako yatanawiri na kulipuka kwa mshangao kwa wengi.
- Omba Mungu wa Danieli akufichulie siri ya utauwa wako, siri ya kupanua biashara yako, kutoka duka mpaka supermarket, kutoka rejareja mpaka wholesale (jumla).
- Kutoka gari ndogo kwenda gari kubwa, kutoka boda boda mpaka Tuk-tuk, taxi mpaka kampuni ya usafiri, mpaka ndege!!
- Unapofunuliwa siri ya maisha yako, siri ya maendeleo yako, siri ya kilimo chako, siri ya maisha yako utastawi na kupanda juu zaidi kwa utukufu wa Mungu.
- Omba sana Mungu akufunulie siri ya maendeleo yako!!
MUNGU WA DANIELI NI MUNGU WA UKOMBOZI-Danieli 6:20-22.
- Danieli mara alipoingia tundu la simba, simba wote walimtambua kama mwana simba mwenzao.
- Mungu wa Danieli ni Mungu atakaye kukomboa na adui na watesi wako.
- Katika tundu la simba, wanapokutupa watu, Bwana Mungu wa Danieli akuonekanie pale.
MUNGU WA DANIELI NI MUNGU WA ISHARA NA MAAJABU-Danieli 6:26-27.
- Mungu wetu, Mungu wa Danieli hawezi kujulikana kupitia masomo ya kitabu cha theologia, Mungu anajulikana kupitia Ufunuo.
- Mungu anajulikana kupitia Ufunuo wa maajabu na ishara zake.
- Wana wa Israeli walimjua Mungu wao kwa ishara na maajabu yake kwao.
- Katika njaa nyikani walimjua Mungu kama Yehova Jire, waliona wokovu na ukombozi wake. Katika giza la maisha yako muone Mungu kama nuru yako.
MWISHO
- Mungu wa Danieli kimbiza wanao nikimbiza, katika jina la Yesu Kristo.
- Mungu wa Danieli nifunulie siri ya maisha yangu.
- Mungu wa Danieli nifunulie siri ya ufanisi na utauwa wangu.
The following two tabs change content below. Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.