Categories: Swahili Service

MUNGU WA MILELE NA MIKONO YAKE YA MILELE

SOMO: KUMBUKUMBU LA TORATI 33:27.

 

Mungu wa milele ni Mungu mkuu zaidi, anawaongoza watu wake kutoka na maovu ya kila haina. Mikono yake ya milele na wema wake vinaonekana katika kila sehemu ya maisha yetu.

Mungu anatambulishwa kwetu kama Mungu wa milele. Huyu Mungu wa milele ndiye maficho yetu. Tunashikwa na mikono yake na mikono yake ni ya milele. Changamoto za maisha zinaweza kuodhoreshwa kwa makundi matatu:

  1. Uchungu wa mambo yaliojiri wakati uliopita.
  • Haya ni mambo na vituko vinavyofanyika katika historia yetu na bado tunabeba mizigo na machungu ya pale kale mpaka leo.
  1. Presha au uzito wa mambo na vitu vinavyo tufanyikia sasa au wakati huu.
  • Mambo tunayopitia sasa yanatuchanganya na kutuweka presha na uzito hivi punde.
  1. Matarajio ya mambo yatakayo tufanyikia siku zijazo usoni.
  • Haya ni mambo tunayotarajia huenda yakafanyika siku zijazo pamoja na yale tusiyojua. Haya yanatufanya kuwa na hofu na fadheha. Hatujui yatakayo kuja kamwa yatakuwa salama.

Katika changamoto hizi zote, Mungu wa milele yupo hili atupe usaidizi na faraja kwa maana yeye ni yule jana na leo na hata milele-Waebrania 13:8. Hebu tutazame:-

UKUU WA MUNGU WA MILELE.

  • Tunapo tazama ukuu wa Mungu, tunahitaji kujua kwamba tuliumbwa na chapa na umbo wake Mungu ili tuonyeshe utukufu wake.
  • Unapowaza juu ya ukuu wa Mungu, papo hapo utavutiwa kum’bariki Mungu kwa sifa za moyoni.
  • Tabia za Mwenyezi Mungu ni pamoja na zifuatazo:-
  1. Mungu wetu ni Mungu anayefahamu yote.
  • Anayajua makosa na udhaifu wetu, anajua dhambi na uasi wetu, lakini bado anatupenda.
  1. Mungu wetu ni mwenye uwezo na nguvu zote.
  • Mungu anao uwezo wa kufanya vitu vyote na kuharibu vyote.
  • Mungu anaweza kutuangamiza sisi sote safari moja, lakini anaendelea kutubariki na uzima.
  1. Mungu wetu yuko kila mahali wakati wote.
  • Yuko kila mahali kila wakati. Mungu anatutazama na anajishughulisha na yote tufanyayo.
  • Lakini Mungu anatuonyesha neema yake na kutuongoza maisha yetu kutokana na kila hatari za kiroho na za kibinafsi katika mikono yake ya milele.
  • Mungu anatuonyesha ukuu wake na pia anashiriki ukuu wake na utukufu pamoja nasi.
  • Mungu alituumba katika chapa na umbo wake hili tuonyeshe ukuu na utukufu wake-Mwanzao 1:26-28.
  • Mungu ameshiriki umbo na sura yake, pamoja na watu wake, lakini sisi hatuwezi kupata sura na utukufu wake kikamilifu kwa sababu hatuwezi na hakuna siku tutakuwa Mungu.
  • Tunaweza kuwa kama Mungu, lakini hatuwezi kuwa Mungu mwenyewe.
  • Kwa sababu Mungu amejifichua kwetu kwa mwana wake Yesu Kristo na kwa sababu Mungu ameshiriki ukuu na sura yake kwetu, basi tumbariki kwa sifa na shukrani, tukapate kuinua jina lake katika mataifa yote.
  • Mungu anayeshiriki na kujidhihirisha kwa watu wake anastahili sifa zote kutoka kwa watu wake.
  • Hakuna aliye kama Mungu wa Israeli, Mungu wa milele hafananishwi na yeyote yule.
  • Hafananishwi na miungu ya dunia hii.
  1. Mungu wetu Yehova ni mkuu kwa maana yeye pekee ndiye muumba wa vyote.
  2. Mungu wetu ni mkuu kwa maana hakuna anayefanana naye au kushindana naye katika utukufu, heshima, uweza, mamlaka, utakatifu na hekima.
  • Huyu ni Mungu aliye mchungaji mkuu, mchungaji mwema anayetoa uhai wake kwa uhai wa kondoo zake, huyu Mungu si mwajiriwa, ndiye mchungaji mwema.
  1. Mungu wetu ni mkuu kwa maana hekima ya kweli inakaa na yeye-Warumi 11:34.
  2. Mungu wetu ni mkuu kwa maana yeye ni Bwana wa mabwana juu ya mataifa yote na wote wenye mamlaka.
  • Mataifa wanafikiri wao ndio wanatawala lakini kumbe ni Mungu anatawala mataifa.
  • Mataifa wanafikiri wao ndio kusema na hatma zao ziko mikononi yao, lakini Mungu yuko katika uongozi katika mataifa yote, yeye ndiye Bwana juu ya mataifa yote-Wakolosai 1:15-20.
  1. Mungu ni mkuu kwa sababu yeye ni mkuu kuliko miungu ya dunia hii.
  • Mtume Paulo anatukumbusha kwamba miungu ya dunia hii ni ovyo-Warumi 1:18-23.
  • Hebu tukapate kuelewa kwamba Mungu wetu ni Mungu mkuu, peke yake anaishi mbinguni. Miungu ya dunia hii wanaishi hapa duniani, wengine milimani, wengine mitoni, wengine majini na wengine chini ya miti na miamba!!

UONGOZI WA MUNGU WA MILELE.

  • Mungu wa milele anatuongoza kwa mikono yake ya milele. Anatulinda na kutuokoa kutoka kwa maovu ya kila haina, iwe ni maovu ya kiroho, ya nafsi na ya mwili.
  • Kuishi katika uongozi wake kunahitaji Matendo na nia zifuatazo:-
  1. Tafakari neno lake-Zaburi 119:105.
  • Kama jinsi nguzo la moto usiku na wingu kwa mchana yaliongoza wana wa Israeli, leo neno lake linaongoza iwe usiku na iwe mchana.
  1. Tuweze kuwa maana sana kwa uongozi wa Roho Mtakatifu kila wakati-Yohana 16:13.
  • Roho mtakatifu anatuongoza katika kweli.
  • Mungu ametupa chochote kinachohitajika kuishi katika utakatifu, kazi yetu ni kuishi kwa kutumia hazina zile ametupa tayari. Tayari ametupatia Roho Mtakatifu, maombi, neno lake, ushirika wa Watakatifu, meza ya Bwana, utakatifu na kanisa lake.
  1. Uamuzi wa kungojea wakati wa Mungu-Isa-64:4.
  • Kabla ya kukimbia kuanza siku yako, mngojee Mungu kwa uongozi wake, soma neno lake, omba sana, jifunike kwa neno lake na damu ya mwana kondoo-Ufunuo 12:11.
  1. Mfuate Mungu wakati uonapo giza-Mithali 3:5-8.
  • Unapo changanyikiwa na maisha na watu mtumaini yeye aliye taa ya maisha yako.
  1. Tembea katika Roho Mtakatifu kila mara, pokea nguvu na ujasiri-Yoshua 1:9.
  • Mungu ndiye kiini cha imani, tumaini nguvu na ujasiri wako.
  1. Uwe tayari kwa vita vya kiroho-Matendo 5:29-32.
  • Tunaishi katika ulimwengu ulio kinyume na Mungu wa mbinguni.
  • Wakati mwingine imani yetu itakuwa kinyume na utamaduni wetu.
  • Tunahitaji mwongozo wa Roho Mtakatifu kila siku, kila wakati.

WEMA WA MUNGU WA MILELE.

  • Mungu anaonyesha wema wake kwa njia tofauti.
  • Njia za Mungu zinaonekana zaidi wakati sisi tumefika mwisho wa hekima zetu. Tunapooishiwa na nguvu tunahitaji msaada wake.
  • Wema wa Mungu unaonekana katika:-
  1. Rehema zake.
  • Tunahitaji rehema za Mungu kila wakati.
  • Hakuna mtu anaweza kuokolewa asiyeona udhaifu wake, dhambi zake na upungufu wake wa kumlilia Mungu na kuomba msaada na rehema zake-Luka 18:13.
  • Lakini rehema za Mungu si kwa wokovu pekee.
  • Yesu Kristo ni mwenye huruma kwa udhaifu wetu, ametualika tuje katika kiti chake cha neema, tukapokee rehema na kupata neema kutusaidia wakati wa mahitaji-Waebreania 4:15-16.
  1. Neema zake.
  • Neema ya Mungu ni bila masharti ni kibali chake kwetu kupitia kwa Yesu Kristo.
  • Kwa neema zake alitukomboa, akatuokoa, akatusamehe dhambi na makosa yetu.
  • Msalaba ndio ishara kuu ya neema zake.
  • Yesu Kristo alikufa mahali petu, atukomboe kutoka dhambini-Waefeso 2:8-9.
  • Tumeokolewa kwa neema, tunaishi kwa neema zake.
  1. Upendo wake.
  • Wema wa Mungu hauna kipimo, upendo wa Mungu ni mkamilifu na tena haubadiliki.
  • Ishara kuu ya upendo wa Mungu ni msalaba wa Yesu Kristo-Yohana 3:16.
  • Njia pekee ya wema wa Mungu ni damu ya Yesu Kristo.
  • Mungu anatangaza wema wake kwetu kupitia:-
  1. Baraka zake za asili-Zaburi 145:3-4.
  2. Fadhili zake-Zaburi 107.
  3. Mwana wake Yesu Kristo-Wakolosai 1:15; Warumi 5:8.
  4. Yesu Kristo ametufungulia wema wake kwa njia mpya-2 Wakorintho 1:20.
  • Baraka zote za Mungu zinatujia kupitia uhusiano wetu na Yesu Kristo.
  • Wema wa Mungu unaanza na Kristo na kumalizika na Kristo.

MWISHO

  • Mungu wetu ni wa milele. Mungu anawaongoza watu wake na kuwalinda na maovu yote.
  • Mikono yake ni ya milele na inaonyesha wema wake katika kila eneo ya maisha yetu.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Rev, DR. Willy Mutiso

Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Recent Posts

MSAADA WA MUNGU WAKATI WA MATESO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: ZABURI 46:1.   Biblia inatuakikishia kwamba Mungu wetu ni “Msaada…

3 weeks ago

GOD GUIDES OUR DESTINIES.

SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: PROVERBS 3:5-6.   Every destiny is a divine…

3 weeks ago

PUT OFF AND PUT ON

SERIES: THROUGH THE BOOK OF COLOSSIANS. TEXT: Colossians 3:5-10   We have put off the…

3 weeks ago

GOD OF THE BREAKTHROUGHS

SERIES: THE GOD WE SERVE TEXT: 2nd SAMUEL 5:17-20   Breakthroughs are divine interventions that…

4 weeks ago

WHO IS SPEAKING TO YOU?

SERIES: DRAWING NEAR TO GOD TEXT: LAMENTATIONS 3:37 It reminds believers that God's word alone…

1 month ago

CHECHEA MSHINDI ALIYE NDANI YAKO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: 1 YOHANA 5:4.   Wakristo wengi wanaishi maisha ya kushindwa…

1 month ago