MFULULIZO: MJUE MUNGU WAKO.
SOMO: ZABURI 121:1-2, 1 WAFALME 20:23-28.
“Mungu wa milima” si Mungu wa milima kigeographia, lakini Mungu wa milima kiroho. Katika Biblia milima inawakilisha changamoto, Ufunuo wa Mungu nyakati za kujitakasa na mahali pa kumkabidhi Mungu. Katika Biblia milima imetumika kama mahali pa mwanadamu kukutana na Mungu. Katika Mlima Sayuni, kutoka mlima wa Moria mpaka mlima wa Mzeutuni Mungu ametumia milima kama mahali pa kujivua kwa mwanadamu. Milima ni mahali palipoinuka juu zaidi ya mabonde, mahali vikwazo na vidhibiti vya mwanadamu vinabadilishwa kuwa mahali pa Ufunuo wa Mungu.
Katika 1 Wafalme 20:23-28, majeshi ya Shamu waliamini kimakosa kwamba Mungu wa Israeli ni Mungu wa milima pekee, kwamba Mungu wa Israeli hawezi vita vya nchi tambarale na mabonde!!
Lakini Yehova alijidhiirisha kwamba yeye ni Mungu wa milima, nchi tambarare na mabondeni, Yehova ni Mungu kila mahali.
Tunapojifunza somo hili tutaona jinsi Mungu anatumia milima katika maisha yetu kudhihirisha nguvu na uwezo wake, kudhibitisha imani yetu na kudumisha hatima zetu. Hebu tutazame:-
MUNGU ANAJIDHIHIRISHA MLIMANI.
Milima ni mahali Mungu amechagua kujidhihirisha-Kutoka 19:16-20.
Mlima ni ishara ya kujitenga kwa Mungu-Isaya 2:2-3.
Juu ya mlima Mungu anaongea vyema zaidi-Kutoka 20:1.
Mlima ni mahali pa kuwa karibu na Mungu zaidi-Mathayo 17:1-2.
MUNGU ANATOA JUU YA MLIMA.
Mungu anajaribu imani kabla kutoa-Mwanzo 22:1-2.
Mungu atatoa juu ya mlima-Mwanzo 22:14.
Kutoa kunakuja baada ya utii-Mwanzo 22:12-13.
Mungu anatoa kile huwezi kuona na macho yako mpaka utakapofika pale-Mwanzo 22:8.
MUNGU HUBADILISHA WATU MLIMANI.
Kubadilika kunakuja panapo uwepo wa Mungu-Mathayo 17:1-8.
Milima inageuza maono yetu-Kutoka 34:29.
Tunapokutana na Mungu maisha yetu yanabadilika kabisa-Isaya 6:1-8.
Mlima utakuinua juu zaidi ya yote na vikwazo vyote-Marko 6:46.
MUNGU ANAWAPA WATU WAKE USHINDI KUTOKA MLIMA.
Mungu hajakabwa na hali na mahali-1 Wafalme 20:28.
Milimani ni mahali pa vita vya kiroho-2 Nyakati 20:20.
Ibada juu ya mlima anaongoza kwa kupenya-Zaburi 121:1-2.
Kutoka juu ya milima tunaona vyema zaidi kuliko bondeni-Kumbu kumbu 34:1-4.
MWISHO
MFULULIZO: MJUE MUNGU WAKO. SOMO: ISAYA 8:18. Mungu wetu ni YEHOVAH. Yehovah si Mungu…
SERIES: “NEARER MY GOD TO THEE.” TEXT: PSALM 42:7. Many believers settle for shallow…
SERIES: THE POWER OF PRAYER AND FASTING TEXT: ISAIAH 58:3-9 God desires that we…
MFULULIZO: MJUE MUNGU WAKO. SOMO: 1 WAFALME 20:23-28. Mabonde si mahali pa kuachwa lakini…
SERIES: NEARER MY GOD TO THEE.” TEXT: PSALM 91:1-2. The secret place is not…
SERIES: THE POWER OF PRAYER AND FASTING. TEXT: JOEL 2:12. Prayer and fasting has…