Categories: DANIELSwahili Service

MUNGU WETU ANAWEZA

DANIELI 3:1-30

UTANGULIZI

Ni lazima kuchukua msimamo wetu katika Mungu wetu kama vile Danieli (Mungu ndiye hakimu wangu) Hanania (Mungu ni mwenye rehema)    Mishaeli (Mungu hafananishwi) na Azaria (Mungu ndiye anisaidiaye). Imani yetu lazima kujaribiwa. Mungu wetu tunaye mwabudu ni muweza wa yote. Mungu wetu anaokoa.

Hebu Tuone:-

I. HATA IKIWA MUNGU HATATUOKOA-HATUTA ABUDU HAU KUISUJUDIA  MIUNGU YAKO (Danieli 3:1-30)

  • Kumbuka wewe na mimi tu askari Jeshi wa Kristo (2 Timotheo 2:3-5)
  • Askari mwema wa Kristo ni mfuasi, mwaminifu, anajua sauti ya komanda wake, silaha zake za vita, anajua adui yake, rafiki zake, yeye ni mpiganaji na anamaliza kazi vyema. Katika mlango huu wa tatu tuko Babeli.
  • Nebukadneza mfalme wa Babeli alijaribu sana kugeuza hawa vijana wane.
  • Lugha (1:40 Elimu na vitabu (1:4) Tabia (1:5) (Lifestyle) msimamo (1:7) majina yao yaligeuzwa.

II.  SHIDA ALIYOPATA MFALME NEBUKADNEZA

  • Hata ingawa vijana hawa walikuwa mbali na nyumbani (maili 1500) mbali na jamaa zao.
  • Vijana walikataa kubandili Imani na desturi za Yuda.
  • Kumsimamia Bwana ni hali ya uamuzi wa moyo wako.
  • Hawa vijana waliamua katika nafsi zao kutojitia unajisi.

III. WATU WA MUNGU NI WATU WANAOTESWA (3:19-23)

  • Imani yako lazima kujaribiwa.
  • Tunajaribiwa sana kupiga magoti yetu kwa dunia hii, kazini, shuleni, mitaani,nyumbani.
  • Hivyo mfalme Nebukadneza aliazimu kuwaharifu hawa vijana.
  • Mfalme aliamua vijana kutupwa motoni uliowaka kwa nguvu mara saba zaidi (3:9-18)
  • Hawa vijana waliteswa kwa sababu
  1. Msimamo wao (3:8-12)
  2. Mwokozi wao (3:13-15)
  3. Imani yao (3:16-18)

IV.  WATU WA MUNGU WANADUMISHWA NA MUNGU WAO (Danieli 3:24-27)

  • Hawa vijana walipotupwa motoni walijikuta hawakuwa pekee yao.
  • Mungu alijiunga pamoja na wao (Isaya.43:2-4)
  • Hawa vijana walikuwa huru katika moto– Moto ulichoma Kamba pekee!!
  • Hawa vijana walikuwa salama Zaidi katika ule moto. Hawakuchomeka, hawakufa, walipitia motoni, lakini moto haukupita ndani yao. (Warumi 8:28)
  • Mtu wa nne hakutoka katika ule moto, alibaki dani. Mwana wa Mungu (Kristo) anakungoja hapo (V.26)
  • Nebukadneza alipowakangua hao vijana, alishangaa sana (v.27)

V.  WATU WA MUNGU NI WATU WA KUPANDISHWA CHEO (28-30)

  1. Mtu wa Mungu ni mtu wa kusifiwa (V.29)
  2. Watu wa Mungu wanapandishwa cheo (v.30)
  3. Watu wa Mungu wanaonewa wivu wa dunia hii (3:8, 12)
  4. Watu wa Mungu hawafuati umati (Zaburi 100:3)
  5. Mungu wetu hafananishwi.

 

MWISHO

  • Moto huu haukupangiwa kukumaliza lakini kukutakasa.
  • Moto huu ulipangwa kuchoma kile kilikuwa kimekufunga.
  • Unaposimamia ukweli huenda utasimama peke yako.
  • Unapotembea na Mungu, huwezi kuwa pekee yako.
  • Mungu wetu anaweza.
  • Mungu ni Mungu hata wakati serikali inamkataa, hata dunia wakikataa, hata wafuasi wake wakikataa, hata shida zikija Mungu ni Mungu. Mungu ni Mungu hata wakati hauna pesa, watoto wako wamemuasi Mungu, ndoa yako inapoyumba yumba, mauti inapokujia, Mungu ni Mungu. (I Petro 4:12-13)

 

The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Rev, DR. Willy Mutiso

Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

View Comments

  • Like!! I blog quite often and I genuinely thank you for your information. The article has truly peaked my interest.

Share
Published by
Rev, DR. Willy Mutiso

Recent Posts

DAMU YA UTAKASO.

MFULULIZO: AGANO LA UTAKASO. SOMO: KUTOKA 12:12-13.   Damu ya Yesu Kristo ndiyo mhuri wa…

12 hours ago

KEY TO DIVINE SPEED.

SERIES: SUPERNATURAL ADVANCEMENT. TEXT: HABAKKUK 3:19.   The journey of fulfilling your destiny does not…

14 hours ago

BE YE THANKFUL TO GOD.

SERIES: THROUGH THE BOOK OF COLOSSIANS. TEXT: COLOSSIANS 3:15   Thankfulness is a great attitude…

16 hours ago

LEVELS OF THE ANOINTING.

SERIES: THE ANOINTING. TEXT: EZEKIEL 47:1-5   There are levels of the anointing and each…

4 days ago

UMETAKASWA KUPOKEA KIBALI.

MFULULIZO: AGANO LA UTAKASO. SOMO: ESTA 2:15-18.   Kibali cha Mungu ndicho kinacho watenga watoto…

1 week ago

THE GOD WHO SHIFTS THE HEAVENS IN YOUR FAVOR.

SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: HAGGAI 2:6-9.   God has the power to…

1 week ago