Categories: Swahili Service

MWALIKO WA USHIRIKA

SOMO:  HESABU 10:29-32

UTANGULIZI

Biblia ni kitabu cha mialiko mikuu. Katika Biblia Mungu anaendelea kuwaalika watu wamjie na kushiriki katika kazi yake. Katika somo hili Musa anaongea na mtu kwa jina Hobabu. Hobabu alikuwa mkwe wake Musa. (Waamuzi 4:11) Hobabu kwa jina linguine aliitwa Yethro kuhani mkuu wa Midiani (Kutoka 18). Yethro alimtembelea Musa na wana wa Israeli jangwani. Hivyo Musa alipata Nafasi ya Kumwalika kujiunga na wao kwenda Kanaani Inchi ya Ahadi. Sisi nasi tumeitwa kuwaalika watu kujiunga katika safari ua Mbinguni.

Hebu tujifunze:-

I.  NJOO, JIUNGE NASI KATIKA SAFARI. (Hesabu 10:29)

  1. Watu maalumu
  • Musa alimwalika mkwe kujiunga na watu waliobarikiwa na Mungu.
  • Wana wa Israeli walikuwa maalumu kwa maana wamechanguliwa (Kumbukumbu 7:6)
  • Wana wa Israeli ni watu waliokombolewa (Kutoka 15:13)
  • Watakatifu wa Mungu ni watu maalumu, wamekombolewa na kuchanguliwa (Waefeso 1:4, Yohana 15:16, I Petro 1:18-19, I Petro 2:9)
  1. Pahali maalumu.
  • Musa alimwalika Hobabu kwenda Inchi na pahali maalumu.
  • Inchi, bora Zaidi, inchi ya baraka , inchi inafurika maziwa na asali. (Kutoka 3:8)
  • Sisi nasi tumeitwa kwenda inchi na mji bora Zaidi (Ufunuo.21:4; 27, Yohana 14:1-3)
  1. Nafasi Maalumu
  • Hobabu hakuwa mmoja wa wateule wa Mungu.
  • Hobabu hakuwa katika Agano, lakini kama Hobabu atashiriki na wana wa Israeli atakuwa kama watu wa Israeli. (Mathayo 28:19-20, Marko 16:15)

II. NJOO, USHIRIKI KATIKA JAMII YA MUNGU. (Hesabu 10:29-32)

  1. Uje ushiriki katika jamii yetu. Hakuna wokovu inje ya Kristo Yesu. (waebrania 7:25)
  2. Uje ushiriki katika baraka za Mungu wetu. Tunakuitaji na wewe pia unatuhitaji. (v.31)
  • Watu wanatuhitaji (Warumi 12:15;15 1-2; Wagalatia 6:2 ; Mathayo 22:39)
  • Njoo pamoja nasi: tutakutenda mema. (v.32)

III. NJOO, SHIRIKI KATIKA AHADI ZETU.  (Hesabu 10:29)

Bwana amenena mema juu ya Israeli”

Uje ushiriki ahadi ya Mji bora.

  • Dunia hii si mahali petu, kwetu ni mbinguni. (I Petro 2:11)
  • Twaenda inchi ya ibada na sifa (Ufunuo 4:5, 7:9-17)
  • Twaenda inchi ya ishara na maajabu (Ufunuo 21-22)
  • Twaenda inchi ya afya (Ufunuo 21:4; 27)

Uje ushiriki ahadi ya tumaini (v.29)

  • Itakuwa siku ya raha, kukutana na wenzetu, itakuwa siku ya dhawabu. (Matt.10:29-32, I Wak. 3:10-15)

Uje ushiriki ahadi ya kusaidiwa.

  • Ameahidi uwepo wake. (wafilipi 4:9, Matt.4:25-34)
  • Ameahidi utakaso wake. (II wak. 5:17)
  • Amahidi utoshelevu na usalama wake (II wak.12:9)

 

MWISHO

¨ Hobabu (Yethro) kwanza alikataa mwaliko (V.30)

¨ Hobabu baadaye alikubali mwaliko (Waamuzi 4:18-22)

¨ Yaeli alikuwa mke wa mwana wake Hobabu

¨ Je, Mungu amenena na maisha yako ? Basi mjie Kristo.

¨ Je, Mungu amenena juu ya shida yako ? Njoo kwake.

¨ Usimkatae Mungu anaponena kwako.

 

 

The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Rev, DR. Willy Mutiso

Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Share
Published by
Rev, DR. Willy Mutiso

Recent Posts

DAMU YA UTAKASO.

MFULULIZO: AGANO LA UTAKASO. SOMO: KUTOKA 12:12-13.   Damu ya Yesu Kristo ndiyo mhuri wa…

10 hours ago

KEY TO DIVINE SPEED.

SERIES: SUPERNATURAL ADVANCEMENT. TEXT: HABAKKUK 3:19.   The journey of fulfilling your destiny does not…

12 hours ago

BE YE THANKFUL TO GOD.

SERIES: THROUGH THE BOOK OF COLOSSIANS. TEXT: COLOSSIANS 3:15   Thankfulness is a great attitude…

14 hours ago

LEVELS OF THE ANOINTING.

SERIES: THE ANOINTING. TEXT: EZEKIEL 47:1-5   There are levels of the anointing and each…

4 days ago

UMETAKASWA KUPOKEA KIBALI.

MFULULIZO: AGANO LA UTAKASO. SOMO: ESTA 2:15-18.   Kibali cha Mungu ndicho kinacho watenga watoto…

1 week ago

THE GOD WHO SHIFTS THE HEAVENS IN YOUR FAVOR.

SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: HAGGAI 2:6-9.   God has the power to…

1 week ago