MFULULIZO: MAISHA NA NYAKATI ZA ELISHA.
SOMO: I WAFALME 19:19-20; 2 WAFALME 2:1-25
Elisha alikuwa nabii msaidizi wa nabii Eliya. Elisha alikuwa nabii wa upako marudufu ya Eliya.
Hebu tuone mwito wake kwa kazi ya unabii:-
KUJIBU MWITO WA MUNGU.
Mwito-1st Wafalme 19:19.
- Mungu alikuwa amemjulisha Eliya kumtia Elisha mafuta. Elisha mkulima ndiye atakuwa nabii katika nchi ya Israeli-lakini Mungu hakumjulisha Elisha.
- Elisha ni mkulima, wala si mhubiri anafanya kazi ya ukulima.
- Eliya alipotokea kwa Elisha, mara moja Elisha alimtambua.
- Kila mtu alimfahamu Eliya.
- Hivyo, Elisha alielewa mara tu alipomwona Eliya kwamba Mungu atampaka mafuta kuwa nabii Israeli.
Kujitoa kwa Elisha-1st Wafalme 19:20.
Mara moja Elisha aliposikia sauti ya Eliya, Elisha aliacha kila kitu na kumfuata Eliya. Vs. 20 “Naye akawaacha ng’ombe akamfuata Eliya mbio, akasema nipe ruhusa, nakuomba, nibusu baba yangu na mama yangu, kisha mimi nitakufuata. Eliya akamwambia Elisha, enenda, urudi, ni nini niliyokutendea?”
- Kujitoa kwa Elisha kulikuwa mara moja. Elisha bila shaka, bila vita alimfuata Eliya.
- Mungu atwitapo sharti kutii sauti yake mara moja.
Elisha alitoa sadaka-1st Wafalme 19:21.
- Elisha aliwachinja jozi ya ng’ombe wake akatokosa nyama zao kwa ile miti ya nira akainuka, akamfuata Eliya akamhudumia.
- Katika mwaka wa 1519, Hernando Cortez aliwachukua watu 600 kwenda Mexico kupigana na Wahindi wa Aztec waliokuwa na jeshi ya maelfu wa askari vita.
- Hernando Cortez alichoma moto meli walizokuja nazo.
- Hivyo askari wake hawakuwa na kimbilio, ilikuwa ni kupigana vita au kifo!!
- Ikiwa utadumu katika kazi na mwito wako kwa Yesu Kristo lazima kuchoma kila kitu ambacho kingekuwa tegemeo na mvuto wa kurudi nyumbani.
- Lazima muelewa na mwito wako kwa Bwana.
- Choma moto vyote ambavyo ni tumaini ya kurudi nyuma.
- Mtumaini Mungu kwa maisha yako ya mbele.
KUTAFUTA UPAKO WA MUNGU-2 WAFALME 2:1-8.
- Upako ni nguvu za Mungu kwa kazi aliyokuitia.
- Sasa Elisha alikuwa ametumikia Eliya kwa miaka saba (7).
- Eliya sasa anamaliza kazi yake, hivyo anaendelea kumwandaa Elisha kushika kazi ya unabii.
- Wakati umefika kwa Eliya kumwachia kazi Elisha.
Vikwazo vya huduma-2 Wafalme 2:1-8.
- Hapo Elisha amefuata Eliya katika safari yake.
- Inaonekana kwamba Eliya, Elisha na pia wana wa manabii walijua kinachoendelea.
- Wana wa manabii katika kila mji walioupitia wamsihi Elisha kurudi.
- Eliya pia alimsihi Elisha kubaki, lakini Elisha alikataa, anataka kumtumikia Eliya mpaka mwisho.
- Eliya alifanya muujiza wake wa mwisho wa kugawanya maji ya Yordani.
- Katika maisha yako, utakutana na vikwazo vingi, lakini lazima ukastahimili ukitaka kuona upako wa Mungu kwa maisha yako.
Tafuta yaliyo bora zaidi-2 Wafalme 2:9-10.
- Eliya alimpenda sana Elisha, alipanda sana kumtendea yaliyo bora zaidi.
- Elisha hakuuliza mambo makuu, pesa, mali, nyumba na mashamba.
- Elisha aliomba mara dufu ya upako uliokuwa juu ya Eliya!!
- Kupokea mara dufu si jambo rahisi hivyo.
- Kupokea upako wa Roho Mtakatifu si kazi ya Eliya kupeana, lakini Mungu pekee.
- Wengi leo wanataka kupokea hashima, sifa, nguvu, kufahamika, mali na fedha.
- Lakini Mungu anataka sana kutupa sisi upako wa Roho-nguvu zake.
Upako wa Mungu-2 Wafalme 2:11-14.
- Eliya aikuwa kama baba kwa Elisha. Eliya alitumia miaka saba kumfunza Elisha kazi ya unabii.
- Lakini upako hauwezi kufundishwa mtu, unapeanwa na Mungu.
- Hivyo, Mungu amechagua nabii wake, nabii anakubali wito, Mungu anampaka mafuta kwa huduma.
- Baada ya kumlilia Eliya, Elisha alichukua lile vazi ya Eliya na kurudi mpaka mto wa Yordani!!
- Sasa Elisha amejaa imani, akapiga yale maji kwa lile vazi la Eliya na kusema “wapi Mungu wa Eliya?”
- Hivyo Elisha akaingia kazi ya nabii wa Mungu.
- Tazama:-
- Mungu alimwita Elisha-Elisha akaitika mwito.
- Elisha alimtumikia Eliya na Mungu kwa unyenyekevu mpaka Mungu akampandisha cheo-1 Petro 5:6.
- Elisha alitembea kwa imani.
HUDUMA ZA KWANZA ZA ELISHA-2 Wafalme 2:19-25.
- Mara moja baada ya Elisha kuingia huduma Elisha alipata changamoto mbili.
- Hizi changamoto mbili ni kuwafajiri walio katika dhiki na kuwapa dhiki waliostarehe.
- “comfort the afflicted, afflict the comfortable.”
- Baada ya miaka elfu moja Yesu Kristo alikuja duniani kuwafajiri walioonewa na kuwapa dhiki waliokuwa katika starehe zao.
Kuwafajiri waliokuwa katika dhiki-2 Wafalme 2:19-22
- Tangu wakati wa Yoshua mji wa Yeriko ulikaa katika laana na Yoshua.
- Maji ya mji, mchanga wao na watoto wake walikaa katika laana-Yoshua 6:26.
- Yoshua alilaani Yeriko kwa sababu ya dhambi zao.
- Sasa Elisha ataenda kuvunja ile laana kwa neno la Mungu.
- Chumvi ni ishara ya utakaso, Mungu alitumia neno lake kwa kinywa cha Elisha kuivunja na kubariki mji wa Yeriko.
- Uponyaji unatoka kwa Mungu-Zaburi 107:19-20.
- Sasa utakaso wetu unatujia kwa neno na damu ya Yesu Kristo!!
- Mwenye dhambi anazaliwa upya na kutakaswa katika damu ya Yesu Kristo.
Kuwapa dhiki waliostarehe-2 Wafalme 2:23-25.
- Elisha alipofika Betheli, mahali pa ibada, “nyumba ya Mungu.”
- Kikundi cha vijana wa mji wa Betheli walimdhihaki na kumtusi Elisha, kwa sababu ya upaa wake “Upaa, wewe mwenye upaa.”
- Mungu aliwatuma dubu wawili wa kike kwa wale vijana, wakawararua vijana 42.
- Vijana hawa walikosa heshima kwa mtumishi wa Mungu.
- Mungu anajali heshima za watoto wake.
- Kulipiza kisasi ni kazi ya Mungu.
- Kukosa heshima kwa mtumishi wa Mungu ni kukosa heshima kwa Mungu.
- Elisha hakupigana vita bali Mungu anapigana vita vyake mwenyewe.
MWISHO.
- Pokea mwito wa Mungu juu ya maisha yako.
- Tafuta upako wa Roho Mtakatifu.
- Tumika katika karama uiliyopewa na Mungu.
- Pokea baraka kwa kuvunja laana juu ya maisha yako.
The following two tabs change content below. Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.