MFULULIZO: RUTHU
SOMO: RUTHU 1:1-22.
Katika ujumbe wa kwanza tulitazama jinsi jamii inaweza kufanya makosa kubwa kwa kutoomba mwongozo kutoka kwa Mungu na kwa kutomtegemea Mungu mahitaji yao.
Ilikuwa wakati waamuzi walitawala Israeli, kulikuwa na njaa katika nchi hivyo Elimeleki, Naomi na watoto wao wawili walihama kutoka Bethlehemu ya Yuda na kwenda nchi ya Moabu.
- Bethlehemu Maanake ni “Nyumba ya mikate.”
- Yuda Maanake ni “Bwana asifiwe.”
- Moabu Maanake ni “washbasin” chombo cha kuogea.
Hivyo jamii ya Elimeleki ilihamia nchi ya Moabu walienda kuishi katika “karai” wakaishi na watu wenye dhambi.
Wakati waamuzi walitawala Israeli ulikuwa wakati wa kuasi Mungu-Waamuzi 17:6, “siku hizo hapakuwa na mfalme katika Israeli, kila mtu alifanya hayo aliyoyaona kuwa ni mema machoni pake mwenyewe.”
Nchi ya Israeli ilikuwa katika dhambi siku za waamuzi.
Ni hatari sana kuishi katikati ya watu wa dhambi ka maana dhambi iitakupata.
Kenya ni nchi ya dhambi, ufisadi, mauaji, ulevi. Ni rahisi sana kuambukizwa dhambi hizi zote hapa Kenya.
Ilikuwa shida kuishi huko Moabu kwa Elimeleki, Naomi na watoto wao.
- Shida za Kenya ni nyingi, lakini wahubiri hawataki kuhubiri kwa sababu wanatafuta kujaza makanisa yao.
- Hivyo Naomi aliishi siku hatari, wakati waamuzi walitawala Israeli.
- Hebu tujifunze:-
HEBU TUTAZAME TENA JAMII YA ELIMELEKI.
- Baba aliitwa Elimeleki, maana jina lake ni “Mungu wangu ni mfalme wangu” (my God is my king).
- Mama aliitwa Naomi Maanake ni “anayependeza, mrembo” (pleasantness).
- Haya ni majina ya kupendeza kwa watu wameoana.
- Maloni Maanake ni “Hana afya” (unhealthy).
- Kilioni Maanake ni “dhaifu” (puny/weak).
- Hatujui kwa nini Elimeleki na Naomi wanazaa watoto dhaifu, hatujui udhaifu wa miili yao.
- Maaloni na Kilioni pamoja na kupata wake wao kutoka Moabu hawakupata watoto, waliishi bila kuzaa!!
- Tunahitaji kufahamu kwamba kutakuwa na wakati wa njaa.
- Njaa ni hali ya laana kutoka kwa Mungu. Laana inakuja kwa sababu ya dhambi.
- Dhambi ndiyo ilileta:-
- Njaa na ukosefu.
- Mauti.
- Magonjwa na shida za kila nama.
- Somo aliyosoma Naomi imeandikwa katika Ruthu 1:21, “Mimi nalitoka hali nimejaa naye Bwana amenirudisha sina kitu…..”
- Mara tunaona jamii zinateseka tunasema ni bahati mbaya, lakini ni kwa sababu ya mshahara wa dhambi.
- Tunapoenda mbali na Mungu wetu, kunao gharama. Tukitubu dhambi zetu Bwana anao urejesho-Ruthu 1:22, ‘Basi Naomi akarudi Bethlehemu mwanzo wa mavuno ya shayiri.”
NAOMI ALIRUDI NYUMBANI.
- Naomi alirudi nyumbani Bethlehemu ya Yuda, lakini kwa nini Naomi alirudi?
- Hukumu za Mungu-1:3-5.
- Mtu wa Mungu anapofanya dhambi ni lazima kungojea hukumu.
- Dhambi inamalipo yake.
- Mtu anapofanya dhambi hajui gharama atakayo lipa baadae!!
- Mkristo anaporudi nyuma na kwenda mbali na Mungu, kwa kweli hajui gharama atakayolipa kwa dhambi zake.
- Kama Naomi angalijua gharama za kwenda Moabu, pengine hangeenda Moabu.
- Ni baadaye, Naomi alijua gharama za kwenda mbali na Mungu.
- Naomi alioteza kwa mauti mume wake, na wana wawili, hio ndio gharama ya dhambi za Naomi!!-Ruthu 1:21.
- Mungu aliwapa Israeli chakula-Ruthu 1:6.
- Mungu aliwapa chakula watu wake.
- Watu wengi kila siku wanaongozwa na chakula.
- Naomi alivutwa na chakula kurudi Bethlehemu ya Yuda.
- Naomi alienda Moabu kwa sababu ya chakula. Sasa anarudi Bethlehemu ya Yuda kwa sababu ya chakula.
- Tazama alipofika, Mungu alimpa Naomi vitu viwili-
- Chakula cha mwili-1:6.
- Naomi alirudi Bethlehemu kwa sababu Mungu amewapa watu wake chakula.
- Kunao sababu nyingi watu wanamjia Mungu na kanisa lake-Luka 14:23.
- Watu walimfuata Yesu Kristo kwa sababu ya chakula na mikate.
- Siku moja aliwalisha watu 4,000 na siku nyingine watu 5,000.
- Naomi amerudi Bethlehemu kwa sababu ya chakula cha mwili.
- Chakula cha roho-1:16.
- Naomi amerudi Bethlehemu pamoja na Ruthu.
- Ruthu alikuwa na sababu ya kumfuata Naomi.
- Ruthu alitafutiwa sana na Mungu wa Israeli-1:16; 1 Petro 2:2-3.
- Ruthu alijiunga pamoja na watu wa Mungu, Ruthu alichukua imani ya Mungu wa Israeli bila kurudi nyuma.
- Kujitoa kwa Ruthu kwa Naomi kuna nguvu nyingi kiasi watu wengi wanayaweka maneno ya Ruthu kwa mwaliko wao au kwa pete zao za ndoa.
- Mungu naye anachukua kujitoa. Kwa Ruthu kwa Naomi kama msingi wa upendo wa kweli.
- Ona imani ya Ruthu.
- Sitakuacha kamwe.
- Sitarudi nyuma kukufuata.
- Nitaenda uendako, nitaishi uishipo.
- Utakapo kufa, hapo nami nitakufa.
- Utakapo zikwa ndipo nami nitazikwa.
- Kujitoa kwa namna hii ndio kujitoa Mungu anapenda.
- Ruthu alivutiwa na upendo wa Mungu wa Israeli na watu wake pia.
MWISHO
- Katika wakati wa giza nyingi Mungu angali katika kiti cha enzi-1:1-5.
- Uchaguzi wako unahusu Mungu sana-1:6-15.
- Mungu wa Israeli anaongoza na kuwabariki wote wanao mtumaini-1:16-22.
The following two tabs change content below. Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.