Categories: Swahili Service

NAWE UTALITAJA NENO, NALO LITATHIBITIKA KWAKO

SOMO: AYUBU 22:27-29

 

Watoto wa Mungu wamepewa uwezo wa kulitaja na kukusudia neno, kuambatana na neno la Mungu na Mungu anadhibitisha lile neno. “Nawe utakusudia neno, nalo litadhibitika kwako”-Ayubu 22:28.

Kutaja au kukusudia neno Maanake ni kutumia uwezo na nguvu za Mungu kuamrisha neno kulingana na sheria za Mungu.

  • Mungu ametufanya kuwa wafalme na makuhani, tabia moja ya ufalme ni nguvu na malaka ya kutaja neno (Ufunuo 1:6).
  • Kama makuhani na Wafalme katika ufalme wa Mungu, tumepewa nguvu na mamlaka ya kutaja na kukusudia chochote kile, kuambatana na neno na makusudi ya Mungu katika maisha yetu na maisha ya wengine-Mhubiri 8:4.
  • Kama Wafalme katika ufalme wa Mungu tumeitwa kuyaishi maisha ya nguvu ya kiungu tumepewa uwezo na mamlaka ya kutaja na kuamrisha tunachotaka kufanya-Yohana 10:19-20.
  • Tunachohitaji basi ni kuelewa na kuangaziwa, tukafahamu sisi ni nani na nafasi yetu katika Mungu, kupitia kwa Yesu Mwokozi wetu-Waefeso 1:19-22.
  • Imetupasa basi kusimama kwa uadilifu katika neno la Mungu na kutaja, kutangaza, kuazimia tunachotaka na kuamini kwamba kitatendeka katika maisha yetu na kwamba Mungu mwenyewe atadhibitisha neno letu.
  • Hebu tuone mambo tatu:-

NASAFI NA MSIMAMO WAKO KATIKA UFALME WA MUNGU.

  • Tangu siku ulipookooka kwa kumpokea Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wako, ulipewa nafasi, msimamo na cheo cha kuwa mwana katika ufalme wa Mungu, pamoja na nguvu katika ufalme wa Mungu pamoja na nguvu na mamlaka yanaolingana na ufalme wa Mungu-Yohana 1:11-13.
  • Ufalme wa mkristo si kulingana na uchaguzi wa mwanadamu bali ni uchaguzi wake Mungu na ukuu na mamlaka yake.
  • Kwa sababu ulichaguliwa na Mungu mwenyewe kuwa mwana wa ufalme wake, hakuna mwanadamu au nguvu za mwanadamu zinaweza kukutoa kwa ufalme wake-Warumi 8:37-39.
  • Dunia yote ilikaa katika giza kuu mpaka amri aliyotoa Mungu kwa neno lake-Mwanzo 1:2-5.
  • Kwa neno lake Mungu nuru ilikuweko “Na iwe nuru.”
  • Mungu aliumba vyote kutoka kwa ukiwa-uwezo na mamlaka ya kuumba vitu kutoka kwa ukiwa, tumepewa kama watoto wa ufalme wa Mungu.
  • Nguvu na mamlaka ya kusema, kutaja na kukusudia umepewa kama mtoto wa ufalme kulingana na neno la Bwana.

AZIMIO LAKO NA UFALME WA MUNGU.

  • Ni katika ufalme wa Mungu pekee, na unapokaa na kudumu katika ufalme wa Mungu wewe unaweza kukusudia kutaja na kutangaza azimio litakalo shikwa mkono na nguvu za ufalme-Wakolosai 1:13.
  • Mambo na neno utakalotaja na kukusudia na utakalotaja na kukusudia na kutangaza ni lazima liwe katika orodha ya ahadi za ufalme wa mbinguni. Hili azimio na neno lako lipate kuungwa mkono na nguvu za mbingu-Mathayo 16:18-20.
  • Kila uamuzi utakayofanya kulingana na kanuni na ahadi za ufalme wa Mungu zitakuwa mamlaka yanayovutia nguvu na mamlaka ya mbinguni kudhibitisha neno lako.
  • Hivyo si kutaja tu, si kuazimia tu, si kusudia tu, lakini kwenda sambamba na nguvu za ufalme wa mbinguni.
  • Azimio na kutaja neno lolote na askari wa ufalme wa mbinguni itakuwa mamlaka au azimio ambalo watu, mamlaka na hali yote inahitaji kutii mara moja.
  • Kwa azimio lako na kutangaza, wewe unaamua kitakacho tendeka na kufanyika duniani-Mhubiri 8:7.
  • Sisi tuliookoka tu Wafalme kwa uchaguzi wa Mwenyezi Mungu. Hivyo azimio, uamuzi na mapenzi yetu na mamlaka ni ya kuingu.
  • Hivyo, hatuitaji kuomba mamlaka ya shetani kuwafungulia mateka, bali twamlisha shetani na pepo na maagenti yake kuachilia.
  • Sisi hatuko hapa kufanya amani na shetani au kutii maagizo yake lakini ni kunena, kufanya vita na kuamrisha nguvu za shetani kutii mara moja.
  • Kwa kawaida wachawi na shetani wanaweka masharti ngumu sana ya kuwafungulia watumwa na mateka wao. Lakini sisi tulio wana wa ufalme wa Mungu tunaamrisha na kudharao masharti ya ufalme wa giza. Iwe ni sadaka, matambiko na masharti yoyote ulioweka na ufalme wa giza.
  • Tunapotangaza, tunapozimia, kutaja na kukusudia neno, hatuwezi kupingwa au kubaguliwa na ufalme wowote, kiumbe chochote na mamlaka yoyote au mtu yeyote-Mathayo 11:23.
  • Hivyo kuambatana na mbingu unahitaji kukusudia kutamka, kuazimia na kunena neno kinyume cha nguvu na mamlaka ya giza, watu na hali yote leo.
  • Mungu anatazamia neno lake kulifanyisha kazi na kutenda.
  • Mamlaka na nguvu hizi zimepewa wote wanaoitimu kupitia neema ya Mungu katika Yesu Kristo.
  • Ikiwa hatutatumia mamlaka tuliopewa, shetani ataendelea kuwa kikwazo kwa baraka zile Mungu amekusudia kwako.
  • Hivyo lazima kuendelea kutaja, kukusudia na kuazimia neno na Mungu ataendelea kudhibitisha neno lako.
  • Tunapoendelea kunena, kutaja na kukusudia neno, Mungu naye ataendelea kudhibitisha lile neno na kudhibitisha kwake Mungu ni jambo la kudumu milele.
  • Tunapoendelea kutaja neno, tunaendelea kutimiza mapenzi ya Mungu duniani kama ilivyo mbinguni.
  • Leo, amua kuwa mtu wa kutaja, kuazimia na kukusudia neno la Mungu juu ya maisha yako, jamii, hali, changamoto zote na neno la Mungu litadhibitika kwako.
  • Kama mtu wa Mungu, mwana wa upande wa Mungu, kumbuka Mungu aliumba vitu vyote kwa neno lake. Kutaja, kuazimia, kukusudia na kutangaza ni kuwa kama Mungu katika nguvu za kuumba kupitia kwa neno lake na nguvu zake.

MILKI (MALI) YAKO KATIKA UFALME WA MUNGU-Obadia 1:17.

  • Hili upate kumiliki milki na mali yako katika Bwana ni lazima uwe kinyume na kupingana na mambo fulani na pia kuazimia mambo fulani.
  1. Mambo ya kupinga.
  • Biblia inasema “nyenyekea mbele za Mungu, mpinge shetani naye atakimbia”-Yakobo 5:7.
  • Hivyo lazima kutoa azimio kumpinga shetani kabisa, na ufalme wa giza-Waefeso 6:10-12.
  1. Pingana na roho ya ubaya na mashetani ya nyumbani kwenu.
  • Kaini kwa uovu wake alimuua ndugu yake Abeli. Mauaji yaliingia kwa nyumba ya Adamu (uovu wa nyumbani).
  • Chuki, uchoyo na wivu, uchungu ziliingia.
  • Yusufu aliteseka kupitia kwa roho ya ubaya wa nyumba ya Yakobo-uchoyo, fitina, uchungu, chuki na uchawi.
  1. Azimia kumaliza roho ya vita na sarakasi za kwenu-Mwanzo 16:11-12.
  • Roho za kukimbia nyumbani, ndoa za kuvunjika, kifo na umaskini, umalaya, udanganyifu na upweke.
  1. Pingana na roho za nyumbani kwenu, roho za kukuzuia kuingia katika nchi ya ahadi za Mungu kwako.
  • Musa hakuingia katika nchi ya ahadi kwa sabau ya roho ya kuzuia baraka.
  • Roho ya kutofaulu wakati wewe uko karibu na baraka zako.
  • Roho inaokufanya kukaribia kufaulu, bila kufaulu.
  • Pingana na roho ya uchawi, nguvu za giza zinazofanya usiweze kupenya katika maisha.
  1. Pingana na roho na watoto wa kigeni (spirit of strange children)-2 Samweli 15:14.
  • Roho na watoto wa kigeni wanapigana na jamii.
  • Roho ya watoto wa kigeni ni watoto au mtoto anayepingana na kila mtu katika jamii.
  • Watoto wa kigeni utawasikia wakiungama kwamba uchawi, roho za shetani, pombe na madawa ya kulevya.
  • Kuna watoto wanaoaribu jamii zao kabisa na kukosesha jamii zao amani na baraka.
  1. Pingana na roho za washauri waovu-2 Samweli 16:23.
  • Hawa washauri wanatoa ushauri wa jinsi ya kuvunja jamii, ndoa na baraka-2 Samweli 15:31.
  1. Pingana na roho ya kupinga Ufunuo wa Mungu-Isaya 6:1.
  2. Pingana na roho ya kufuatwa na maadui (stubborn pursuers).
  • Hizi ni roho za shetani, uchawi, magonjwa.
  • Wengi wetu tumeandamwa na pepo toka tumboni mpaka leo, wengine vita inawangoja katika uzee wao.
  • Wanapowafuata wakifa wanawaachia wengine kuendelea kukufuata.
  1. Vitu vya kuazimia kutaja, kukusudia.
  1. Azimia na tangaza urejesho wa baraka zilizo ibwa-Yohana 10:10.
  • Dai miaka uliyopoteza katika dhambi, dai nafasi zilizopotea-omba urejesho.
  1. Tangaza na azimia kuinuliwa kichwa chako.
  • Umetazama sana chini kwa mavumbi-Zaburi 3:1-3.
  1. Omba kibali kikufuate-Zaburi 5:12.
  2. Omba muongozo wa Mungu juu ya maisha yako-Mithali 3:5-8.
  3. Omba maisha marefu yenye afya.
  • Hautakufa, bali utaishi, utangaze wema wa Mungu katika nchi ya walio hai.
  1. Omba ulinzi wa usalama-Isaya 54:17.
  2. Omba utoshelevu kutoka mbinguni-Zaburi 1:1-3; Wafilipi 4:19.

MWISHO

  • Kwa kinyume chako tangaza, azimia, taja, kusudia mema juu ya maisha, jamii, kanisa, nchi yako.
  • Jiweke katika position ya kujiliwa na Mungu, ishi kwa utakatifu, ungama dhambi zote.
  • Omba furaha, amani, kufaulu, utauwa na ushindi juu ya adui.
  • Tangaza, azimia, kusudia, taja, decree, kwa neno lake Mungu siku zote.
  • Dumu katika damu ya Kristo kila saa na kila wakati.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Rev, DR. Willy Mutiso

Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Recent Posts

MSAADA WA MUNGU WAKATI WA MATESO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: ZABURI 46:1.   Biblia inatuakikishia kwamba Mungu wetu ni “Msaada…

2 weeks ago

GOD GUIDES OUR DESTINIES.

SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: PROVERBS 3:5-6.   Every destiny is a divine…

3 weeks ago

PUT OFF AND PUT ON

SERIES: THROUGH THE BOOK OF COLOSSIANS. TEXT: Colossians 3:5-10   We have put off the…

3 weeks ago

GOD OF THE BREAKTHROUGHS

SERIES: THE GOD WE SERVE TEXT: 2nd SAMUEL 5:17-20   Breakthroughs are divine interventions that…

4 weeks ago

WHO IS SPEAKING TO YOU?

SERIES: DRAWING NEAR TO GOD TEXT: LAMENTATIONS 3:37 It reminds believers that God's word alone…

1 month ago

CHECHEA MSHINDI ALIYE NDANI YAKO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: 1 YOHANA 5:4.   Wakristo wengi wanaishi maisha ya kushindwa…

1 month ago