SOMO: MARKO 16:1-8.
Pasaka inatupa fursa kila mwaka kutazama tena upya kaburi tupu ya Yesu Kristo. Kila mwaka tunakumbushwa upya juu ya nguvu za Mungu wetu. Ni yeye pekee anayeweza kufanya mambo makuu na ya ajabu kuliko jinsi tuwezavyo kuwaza na kuliko tuombavyo.
Marko anatueleza kwamba sabato ilipopita, Mariamu Magdalene, Mariamu mamake Yakobo na Salome walinunua manukato wapate kwenda kuupaka mwili wa Yesu Kristo kaburini.
Ilikuwa Jumapili mapema asubuhi. Hii ni kwa sababu pale Ijumaa hapakuwa na wakati wa kutayarisha mwili wa Yesu Kristo, maana sabato tayari ilikuwa imefika.
Lakini hawa wanawake walikuwa na swali kubwa mioyoni mwao, “Ni nani atakayevingirisha lile jiwe kutoka mlango wa kaburi lile?
Kwanza, jiwe lilikuwa kubwa, pili jiwe lile na kaburi liliundwa na askari wa jeshi la Roma! Tatu, lile jiwe lilikuwa na mhuri wa utawala wa Roma.
Lakini walipofika mle kaburini, tayari lile jiwe lilikuwa limevingirishwa kwa nguvu za Mungu.
Malaika kutoka mbinguni tayari alikuwa amelivingirisha lile jiwe nzito kubwa!! Hivyo, shida yao wanawake ilikuwa tayari imetatuliwa. Hivyo, hofu yao na masumbufu ya mioyo yao ilikuwa ni bure!!
Mungu tayari ameshughulikia mambo yanayo tufadhaisha!!
Machozi yao, huzuni yao, wasiwasi wao, hofu zao, ilikuwa bure kabisa.
Yesu Kristo hakuwa maiti, “Amefufuka, kama jinsi alivyosema.” Malaika wa Mungu aliwaeleza.
Mungu wetu ni yeye yule jana, leo na hata milele. Pasaka inatukumbusha kila mwaka jinsi ukuu wa Mungu ulivyo.
Shetani alifikiri Yesu Kristo amemalizika na mpango wa ukombozi umekwisha, lakini siku hii ya Jumapili ilipata kuwa ndio siku ya nguvu za Mungu, siku ya nguvu, siku ya ushindi mkuu kwa mwanadamu, siku ya ushindi hodari kwa Mwokozi wetu Yesu Kristo. Hebu tujifunze leo;-
UAMUZI MKUU.
- Tunamshukuru Mungu kwa hawa wanawake walikuwa wanawake wa imani kuu-Waebrania 11:35.
- Hawa wanawake waliamua kwenda kujaribu badala ya kukaa kitako nyumbani kama wanaume walivyofanya!!
- Hawa wanawake watatu, yaani Mariamu Magdalene, Mariamu mamake Yakobo na Salome walimfuata Yusufu alipomzika Yesu Kristo kaburi Ijumaa jioni.
- Walimtazama jinsi alimvalisha Kristo ile sanda, walipaona pale alilazwa.
- Walitazama jinsi askari wa Roma waliweka lile jiwe kubwa, jinsi mhuri wa ufalme wa Roma uliwekwa.
- Walihesabu jinsi kikosi cha askari wa Roma walishika doria mle kaburini.
- Hawa wanawake walikuwa na huzuni nyingi, walikuwa wamelia macho yakavimba!!
- Walikuwa wameona jinsi mwalimu wao mpenzi aliumizwa, jinsi walichukua nguo zake na mavazi, na jinsi Mwokozi wao aliuliwa kinyama bila huruma, waliona aibu aliyoona Yesu Kristo.
- Waliona madharau mengi aliyopokea pale msalabani.
- Kwa hawa wanawake, asubuhi mapema iliwadia haraka sana.
- Kwa sababu ya sabato, duka na biashara zote zilikuwa zimefungwa, wasipate nafasi ya kununua manukato ya kuupaka mwili wa Yesu Kristo kwa maziko yake.
- Lakini shida yao kubwa ilikuwa lile jiwe kubwa na ule mhuri na kikosi cha jeshi la Roma.
- Lile jiwe lilikuwa ni ishara kwamba mambo ya Yesu Kristo imekwisha.
- Lile jiwe lilikuwa ni ishara kwamba hamna tumaini tena.
- Lile jiwe lilikuwa na mhuri Maanake kikwazo kikubwa zaidi.
- Lakini pamoja na hayo yote, hawa wanawake walianza safari ya kwenda kaburini.
- Kama hawa wanawake, sisi pia tunao vikwazo njiani.
- Leo uenda unao vikwazo kwa maisha yako, fedha, kazi, ndoa, jamii, ukosefu, ndoa, umasikini.
- Pengine unauliza kama wao, ni nani atanivingirishia jiwe langu?
- Mungu wetu tayari amevingirisha jiwe ya mauti na kifo, mahali pake Mungu ameweka uzima wa milele-Yohana 3:16.
- Mungu atatusaidia kuvingirisha mawe yote.
- Hakuna jiwe kubwa na nzito kuliko nguvu za Mungu wetu.
- Hakuna jiwe la kuudhi ambayo Bwana wetu hawezi kuitoa na kutuonyesha upendo wake.
SHIDA NA VIKWAZO.
- Mawe ni ishara kubwa ya vikwazo.
- Mawe makubwa yanafunga njia na kufanya safari kuwa ngumu.
- Kila jiwe lililo kikwazo kwako leo, Bwana alivunja au atalifanya lile jiwe kuwa jukwaa ya ushindi wako.
- Jiwe lile lilivingirishwa mbali, malaika aliketi juu yake, Akawahubiria wale wanawake watatu!!
- Pamoja na lile jiwe kuwa kikwazo, askari wa kikosi cha Roma kilitisha, lakini wanawake walipofika pale, askari wote walikuwa wameanguka chini kama wafu!!
- Pamoja na jiwe na wale jeshi wa Roma, mhuri wa ufalme wa Roma, tayari ulivunjwa!! Askari wengine walikimbia zao.
- Lao hii wanao kwandama, adui wanaokuzingira wataachwa wafu, wengine watakimbia zao.
- Wanaokupangia maovu, wataacha mipango yao kwa haraka ya kukimbia waokoe maisha yao.
- Chochote kinacho chelewesha maendeleo yako na hatima ya maisha yako, Bwana amevunja sasa.
- Vizuizi vinakuja kwa njia nyingi katika maisha yetu.
- Mawe haya yanatoka ufalme wa giza.
- Lakini ni Mungu pekee anayaondoa mawe kutoka mapito yako.
- Nguvu zile zilimfufua Yesu Kristo kutoka kwa wafu ndizo nguvu zinavingirisha jiwe lako.
- Mungu aliwafunguliwa wana wa Israeli bahari ya Shamu-Kutoka 14.
- Mungu aliwapa chakula mji wa Samaria-2 Wafalme 7:1-20.
- Kulingana na mpangilio wa Samaria na bahari ya Shamu, Mungu atakufungulia njia na mapito yako-Leo.
- Goliathi ni jiwe la vizuizi, lakini alishindwa.
- Lazaro alifufuka kwa wafu-Hakuna jiwe ambalo Mungu wetu hawezi kulivingirisha.
USHINDI NA UTAWALA MKUU.
- Hawa wanawake walipokaribia lile kaburi waligundua kwamba shida yao kubwa tayari imetatuliwa!!!
- Kinacho kusumbua sana ndani ya maisha yako, Bwana tayari ametatua!!
- Kaburi yote ilikuwa wazi. Jiwe lilikuwa mbali, mlango wa kaburi ulikuwa wazi.
- Kwa njia hio hio, shida yako imevingirishwa mbali!!
- Aibu zako zote zimevingirishwa-Mika 7:8.
MWISHO
- Leo Bwana amevingirisha jiwe lako.
- Leo Bwana amekuondolea aibu yako.
- Leo adui zako wamekimbia mbali nawe.
- Leo pata ushuhuda, mhubiri Kristo juu ya jiwe.
The following two tabs change content below. Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.