MFULULIZO: PASAKA
SOMO: YOHANA 12:9-19
Yesu Kristo alianza safari ya kwenda msalabani kwa kuingia Yerusalemu. Njia hii ya kwenda msalabani ilikuwa ni njia ya huzunu na mateso mengi lakini Yesu Kristo alichagua kuipitia njia hiyo. Watu wengi walimlaki Kristo, huku wakitoa mavazi yao na kutandaza matawi ya mitende. Waliimba wimbo wa Hosana, hosanna “tuokoe sasa.” Unabii wa Zakaria 9:9, ulitimia siku hii ya Jumapili ya mitende, miaka 2000 iliyopita. Hebu tujifunze:-
NJIA YA KWENDA MSALABANI ILIKUWA NJIA YA HATIMA-Yohana 12:12-13.
Yesu Kristo alikuja duniani kuokoa sasa wakati huo ulifika.
Watu waliamini sana Yesu Kristo alitoka kwa Mungu.
NJIA YA KWENDA MSALABANI ILIKUWA NJIA YA KUJITOA-Yohana 12:14-15.
Kule kuingia Yerusalemu kulitangaza kujitoa kwake kwa kazi iliyokuwa mbele zake Mwokozi.
Kuja kwake Yesu Kristo duniani kulikuwa ni kujitoa kwake kwa Baba yake.
NJIA YA KWENDA MSALABANI ILIKUWA NJIA YA UVUMBUZI-Yohana 12:16
Watu hawa walitambua kwamba mawazo yao juu ya masihi yalikuwa makosa.
Wanafunzi wa Yesu Kristo na wao walitambua mpango wa Mungu kwa ulimwengu.
NJIA YA KWENDA MSALABANI ILIKUWA NJIA YA UKOMBOZI-Yohana 12:17-19.
MWISHO
MFULULIZO: MJUE MUNGU WAKO. SOMO: ISAYA 8:18. Mungu wetu ni YEHOVAH. Yehovah si Mungu…
SERIES: “NEARER MY GOD TO THEE.” TEXT: PSALM 42:7. Many believers settle for shallow…
SERIES: THE POWER OF PRAYER AND FASTING TEXT: ISAIAH 58:3-9 God desires that we…
MFULULIZO: MJUE MUNGU WAKO. SOMO: 1 WAFALME 20:23-28. Mabonde si mahali pa kuachwa lakini…
SERIES: NEARER MY GOD TO THEE.” TEXT: PSALM 91:1-2. The secret place is not…
SERIES: THE POWER OF PRAYER AND FASTING. TEXT: JOEL 2:12. Prayer and fasting has…