MFULULIZO: SIONI HAYA.
SOMO: 2 TIMOTHEO 3:1-17; YUDA 3-5
Somo letu leo ni juu ya unabii juu ya nyakati za mwisho. Maovu yatazidi. Tunapotazama nyakati hizi zetu tunatambua kuwa huu ndio wakati wa mwisho. Nyakati zetu ni hatari zaidi.
Hatari kubwa zaidi kwa ufalme wa Mungu na kwa kanisa la Yesu Kristo ni Ukristo wa mwilini (Carnal). Ukristo wa kimwili na kidunia ni ukristo ambao shetani amebuni kuharibu imani tuliyopewa kama Watakatifu- Yuda 3-4. Hivyo sisi nasi tunaishi katika siku hizi za mwisho. Siku nazo ni hatari zaidi.
Sababu ya somo letu leo ni kukaza sana kujitoa na utakatifu wa binafsi na ukristo wa kibiblia. Kumbuka ni lazima kufanya vita vikali na dunia hii na mafundisho yake. Vita hivi ni lazima kupigana katika roho zetu, maisha, jamii, umma, shule, kanisa na katika kila eneo ya maisha.
Hebu tujifunze yafuatayo:-
ONYO DHIDI YA NYAKATI ZA HATARI
- Kuna dalili tatu zinazotuonyesha kwamba hizi ni nyakati za mwisho, nyakati hatari sana.
- Kukaza majibu- 3:1. Hakuna mtu duniani anayo majibu kwa maswali makuu duniani na katika nchi ya Kenya.
- Maswali ya uchumi, maswali ya elimu, maswali ya jamii, ndoa, kulea na kazi.
- Maswali ya siasa, sheria, mwelekeo.
- Kukosa sheria katika nchi zetu- 3:2-4.
- Uavyaji mimba, ndoa za mume- mume, mke-mke, kanisa na serikali, sheria ya jamii.
- Kanisa vugu-vugu (Lukewarm church) 3:5.
- Leo kanisa ni kama jinsi club, kioski. Leo tunayo makanisa, vyombo vya sauti na mataa yao ni club.
- Leo kuwa pasta ni kujinufaisha mwenyewe.
- Hizi ni nyakati hatari zaidi. Nyakati za hatari zilianza pentekosti na zitaendelea mpaka Kristo arudi tena.
- Nyakati za mwisho zina tabia zifuatazo;-
- Maovu kuongezeka na kuwa makali zaidi duniani kote- 2nd Petro 3:3; 1st Yohana 2:18.
- Maovu katika jamii na umma kwa jumla.
- Majaribu makuu kwa wana wa Mungu na watumishi wake.
- Maisha ya unafiki na dini za uongo.
- Neema ya Mungu kuzidishwa duniani kote, nguvu za Mungu juu ya kanisa na wote walio okoka- Matendo 4:33; Warumi 5:20.
MASHABIKI WA NYAKATI ZA HATARI- 3:1-4
- Maisha na Matendo ya watu wa nyakati hizi.
- Kujipenda wenyewe.
- Ubinafsi umezidi, watu kujipenda nafsi zao ndio Mwanzo wa tabia mbaya.
- Kupenda fedha- kiburi cha maisha, utajiri na kupenda vitu.
- Mwenye kujivuna, kujisifu.
- Kutotii wazazi kiroho na kimwili- 3:2-4.
- Wenye mfano wa utauwa (godliness) lakini wenye kukana neno la Mungu na nguvu zake.
- Wana dini na kiroho lakini wameshindwa na dhambi.
- Nje wanaonekana wema lakini ndani ya mioyo yao wameoza.
LAANA ZA NYAKATI ZA HATARI- 3:5-9.
- Ni lazima tupokee unabii huu na onyo zake na kila wakati tuweze kuishi tukijua nyakati hizi.
- Ni lazima tujitenge na watu wanaojiita wakristo na wandugu katika Kristo lakini wanazo tabia hizi mbaya.
- Tujiepushe na ukristo wa mwilini na mafundisho yao.
- Wahubiri wa kweli nao wajitenge na wahubiri na walimu wa uongo- 1st Timotheo 6:3-5; Tito 3:10-11.
- Lazima kusimama imara na imani ya mitume, imani hii ilitolewa mara moja tu- Yuda 3.
- Lazima kusimama wima tukiwa macho na wenye kukesha.
- Tujiachilie kwa Roho Mtakatifu na kukubali kuongozwa naye kila wakati.
HIMIZO YA NYAKATI HIZI HATARI- 3:10-15
- Paulo anamhimiza Timotheo kama mchungaji kujihoji nafsi yake na kufuata mfano mwema alioweka Mtume Paulo.
- Elimu ya kweli na mafundisho (Doctrine).
- Tabia ya maisha ya kikristo.
- Lengo na shabaha ya huduma.
- Imani, uvumilivu, upendo, kuvumilia Matendo na dhiki- 2nd Timotheo 3:14-15; Matendo 2:42.
MWISHO
- Hizi ni nyakati za mwisho, ni nyakati za hatari. Tukitaka kuingia mbinguni lazima kufuata onyo na himizo za Mtume Paulo.
- Lazima kujitenga na wenye tabia na maisha ya ndugu wasioishi kweli ya Mungu.
- Je, tutashinda nyakati hizi hatari? Kwa neema Yake pekee.
The following two tabs change content below. Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.
View Comments
Naomba haya mahubiri kwa pdf whatsap number
+255748006555