Categories: Swahili Service

PANUA PAHALI PA HEMA YAKO

SOMO: ISAYA 54:1-17

 

Bwana asifiwe. Saa inayoyoma upesi, kwa saa chache tutaingia mwaka mpya 2024. Tunatazamia kuingia mwaka mpya kwa maana Mungu amekuwa mwaminifu kwa mwaka huu wa 2023. Basi tunyanyue mikono yetu na kumpa Bwana shangwe na shukrani kwa uaminifu wake mwaka wa 2023.

Leo ndio Jumapili ya mwisho ya mwaka!! Kwa Jumapili zote 52 Mungu amekuwa mwaminifu kwetu.

Mungu anapenda leo tuangazie juu ya kupanua mahali pa hema zetu. Mungu anaenda kutupanulia mipaka yetu katika kila eneo ya maisha- Isaya 54:2-3.

Mungu anapenda maisha yako yaendelee mbele. Hivyo Mungu anao mpango wa ajabu kukubarikia katika kila eneo ndani ya maisha yako.

Pengine umepitia maovu na magumu katika mwaka huu wa 2023, pengine hukuona mabadiliko yoyote katika mwaka huu lakini leo Mungu anakupa ahadi ya kwamba anakupangia mema na atakuleta mahali pa nguvu na uwezo na ufanisi.

Natabiri kwamba maisha yako yanaenda kuingia katika nyakati mpya na msimu wa raha na nguvu zake.

  • Upepo wa Mungu unapita juu ya maisha yako na kukuelekeza upya.
  • Katika mwaka mpya, kibali chake Mungu kitakuwa juu yako.
  • Mungu anenda kukuweka katika viwango vya juu zaidi, Mungu anakufanyia jambo jipya.
  • Mungu anaenda kukuweka katika hali mpya na kukufungulia milango ambayo hujawahi kuona hapo mbele.
  • Hebu tuone jinsi Mungu atakupangia kukupanulia pahali pa hema yako.
  • Ninaomba ukapokee upanuzi wake leo.
  • Hebu tutazame:-

TAMBUA MAISHA YAKO YA SASA

  • Kumbuka Mungu aliwakomboa wana wa Israeli kutoka mkono wa Farao.
  • Kwa miujiza yake walipita katikati ya Bahari ya Shamu.
  • Kwa miujiza Mungu aliwaongoza jangwani mpaka nchi ya ahadi.
  • Lakini wana wa Israeli hawakuwa waaminifu kwake, waliomba wapewe mfalme.
  • Wafalme waliwaongoza wana wa Israeli kwa ibada ya sanamu, hivyo wakaishi maisha ya dhambi mbele zake.
  • Katika 2 Wafalme 17:7-8, Mungu aliwaacha kuchukuliwa mateka na uhamisho.
  • 2 Wafalme 17:18- Mungu hakupendezwa nao.
  • Hali yao kwa sasa ilikuwa ni hali ya uhamisho (exile).
  • Wana wa Israeli wakawa mateka wa uhamisho huko Babeli hivyo,
  1. Wakawa tasa- Isaya 54:1.
  2. Wakaaibika, wakapata aibu, wakashuka chini zaidi- Isaya 54:4.
  3. Wakaachwa, wakahuzunishwa rohoni, wakakataliwa- Isaya 54:6.
  4. Wakaachwa kabisa- Isaya54:7.
  5. Wakateswa, wakarushwa, tufani ikawapeperusha kila mahali- Isaya 54:11.
  • Dhambi iliwapeleka wana wa Israeli mbali na Mungu wao.
  • Je, unapotazama mwaka huu wa 2023, maisha yako yalikuwa aje?
  • Pengine ulikosa kila mahali, maisha ya ubinafsi, jamii, kanisa.
  • Lakini pia kuna wale walifanya kila jambo vyema lakini- haukufanikiwa.
  • Pengine ndoto zako ziliharibika, pengine afya, biashara, kazi- pengine kwa mwenye haki kama wewe ulipata aibu nyingi.
  • Lakini Bwana sasa asema hivi; utasa wako si wa kudumu- Mungu anavunja utasa wako leo.
  • Sasa Bwana anasema- panua mahali pa hema yako!!
  • Mungu anaenda kupanua mahali pa hema yako 2024!!

AHADI YA MUNGU- UPANUZI

  • Tafuta eneo zaidi kwa upanuzi wake- Isaya 54:2-3.
  • Bwana asema hivi, panua mahali pa hema yako, tandaza mapazia ya maskani yako.
  • Ongeza urefu wa kamba zako.
  • Vikaze vikingi vya hema yako.
  • Utaenea upande wa kuume na upande wa kushoto!!
  • Msimu huu wa 2024, Mungu ataenda kukupanulia- utasa wa fedha, nguo na hekima umekwisha.
  • Tazama maombi ya Yabezi- 1 Mambo ya Nyakati 4:9-10.
  • Mungu alimwahidia Ibrahimu- Mwanzo 12:14.
  • Haijalishi jinsi ulivyo leo, usijione bure na fukara.
  • Mungu hajamalizana na wewe- Mungu anaenda kukupanulia mahali pa hema yako leo.

JINSI YA KUPOKEA UPANUZI WA MAISHA YAKO

  1. Tubu dhambi zako- Isaya 1:18; Matendo 8:22-23; 1 John 1:9.
  • Usiingie katika mwaka mpya na dhambi za 2023!!
  • Unapotubu dhambi na makosa yako, Mungu atafanya jambo jipya.
  1. Amini- Isaya 54:1- sikiliza sauti ya Mungu.
  • Shida zako zimekwisha leo.
  1. Panua- Isaya 54:2 mahali pa hema yako.
  • Tengeneza njia zako, barabara za kupitia Baraka zake.
  • Omba chupa za mafuta kutoka kwa jirani zako.
  • Mungu anaenda kukupanulia hema yako- Mathayo 6:33.

MATOKEO YA KUPANUA MAHALI PA HEMA YAKO

  1. Siku za furaha na ufanisi- Isaya 54:1.
  2. Mungu anakuletea urejesho- Isaya 54:6.
  3. Mungu anakulinda- Isaya 54:17.

 

MWISHO

  • Je, utapanua mahali pa hema yako?
  • Je, utatubu dhambi na makosa yako?
  • Je, utatembea na Mungu wako 2024?
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Rev, DR. Willy Mutiso

Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Recent Posts

MSAADA WA MUNGU WAKATI WA MATESO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: ZABURI 46:1.   Biblia inatuakikishia kwamba Mungu wetu ni “Msaada…

3 weeks ago

GOD GUIDES OUR DESTINIES.

SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: PROVERBS 3:5-6.   Every destiny is a divine…

3 weeks ago

PUT OFF AND PUT ON

SERIES: THROUGH THE BOOK OF COLOSSIANS. TEXT: Colossians 3:5-10   We have put off the…

3 weeks ago

GOD OF THE BREAKTHROUGHS

SERIES: THE GOD WE SERVE TEXT: 2nd SAMUEL 5:17-20   Breakthroughs are divine interventions that…

4 weeks ago

WHO IS SPEAKING TO YOU?

SERIES: DRAWING NEAR TO GOD TEXT: LAMENTATIONS 3:37 It reminds believers that God's word alone…

1 month ago

CHECHEA MSHINDI ALIYE NDANI YAKO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: 1 YOHANA 5:4.   Wakristo wengi wanaishi maisha ya kushindwa…

1 month ago