MFULULIZO: DANIELI-MUNGU NDIYE HAKIMU.
SOMO: DANIELI 9:1-27 (23-27)
Danieli mlango wa tisa ni unabii wa maana sana katika neno la Mungu. Katika mlango huu Mungu anatwambia kitakachofanyika na wakati na ratiba ya mipango yake.
Danieli mlango wa sita una zungumza juu ya mtu, yaani Yesu Kristo. Hapa Mungu mwenyewe anajifunga kwa ratiba ya mpango wake katika historia ya ulimwengu huu. Danieli 9 ni moja yao ya ushahidi kwamba Biblia ni neno la Mungu na kwamba kila andiko linao pumzi ya Mungu.
Watu wengi wanajaribu kulinganisha Ukristo na dini zingine, lakini Ukristo si dini, bali Ukristo ni uhusiano wa binafsi na Mungu wa mbinguni. Dini ni njia ya wanadamu kumtafuta Mungu, lakini Ukristo ni Mungu akimtafuta mwanadamu-Yohana 3:16.
Maandiko ya dini za dunia hii kama jinsi Islamu, Budha, Hindu na dini zote za Kiafrika hamna Ufunuo na unabii wa mambo yajayo!! Vitabu vyao ni hadithi, mafundisho na kanuni za mwanadamu. Lakini Biblia ni unabii wa kudhibitika. Danieli 9 ni unabii kutoka kwa Mungu mwenyewe kupitia malaika Gabrieli aliyetumwa kutoka kwa Mungu kumpa Danieli yatakayo jiri. Mlango wa 9, ni jibu ya maombi aliyoomba Danieli. Hebu tujifunze:-
MPANGO WA MUNGU KWA MATAIFA NA ISRAELI-9:24.
- Danieli alikuwa juu ya magoti yake akisali.
- Danieli alikuwa katika hali ya kumwaga roho yake mbele za Mungu wa mbinguni.
- Maombi ya Danieli yalikuwa maombi ya kuungama, kutubu na kuomba (confession, repentance and petition).
- Mungu alimtuma malaika Gabrieli na jibu 9:23, “Mwanzo wa maombi yako ilitolewa amri, nami nimekuja kukupasha habari, maana wewe unapendwa sana; basi itafakari habari hii na kuyafahamu maono haya.”
- Gabrieli anasema ujumbe huu ni ujumbe wa kuaminika na kuelewa.
- Ujumbe huu unaeleza hatua sita (6) za ukombozi.
- 24, Gabrieli anaeleza hizi hatua sita za ukombozi kamili. Hatua hizi ni mambo sita Mungu aliahidi kufanya, “Sabini mara saba” yaani Muda wa majuma sabini umeamrisha juu ya watu wako na juu ya mji wako mtakatifu hili-
- Kukomesha makosa.
- Kuishiliza dhambi.
- Kufanya upatanisho kwa ajili ya uovu.
- Kuleta haki ya milele.
- Kutia muhuri maono na unabii.
- Kumtia mafuta yeye aliye mtakatifu.
- Tazama na kuelewa ujumbe huu ni kwa Israeli (yaani watu wako Danieli na mji wa Yerusalemu).
- Unaposoma Biblia ni vizuri kuelewa utofauti wa Israeli na kanisa, Israeli na mataifa.
- Mpango wa Mungu ni pamoja na kifo cha Yesu Kristo msalabani.
- Yesu Kristo alimaliza mambo ya dhambi na upatanisho kwa ajili ya uovu.
- Pamoja na hatua hizi sita, Gabrieli alimweleza Danieli juu ya miaka elfu ya utawala wa Yesu Kristo duniani.
- Utawala wake Yesu Kristo utakuwa utawala wa haki duniani kote.
- Wakati kila unabii umetiwa muhuri (kukamilika) Mungu alimpa Danieli maono ya historia ya ulimwengu, mpaka tamati ya dunia hii kama tunavyo ifahamu.
- Shida za dunia hii ni nyingi, lakini shida zilizo kubwa zaidi ni dhambi na mauti.
- Halijalishi wewe ni nani na unapoishi duniani lakini dhambi na mauti lazima kushughulikiwa.
- Mpango wa Mungu wa ukombozi ni pamoja na kutatua shida hizi mbili za mwanadamu, dhambi na mauti.
- Shida zangu/zako kubwa zaidi ni dhambi na mauti!!
WAKATI WA MUNGU KUELEZWA (Danieli 9:25-26).
- Huu ndio unabii wa ajabu zaidi katika Biblia.
- Katika unabii huu Mungu anaeleza yatakayojiri na wakati kamili wa mambo haya kufanyika.
- Tazama tena kifungu cha 24, “Muda wa majuma sabini umeamriwa.” Maanake “Umeamriwa” ni “umepimwa” au “Umegawanywa” (“Measured” or “divided”).
- Tazama kifungu cha 25-27.
- Majuma 70 ni majuma ya miaka wala si majuma ya wiki. 70×7=490 miaka. “Wiki” kwa Kiebrania ni neno “Shabuwa” Maanake “saba”-Mwanzo 29:15-30.
- Yakobo alipotumika kwa miaka saba ilikuwa ni “wiki moja” (miaka saba).
- Hii miaka 490 au wiki 70 zimegawanywa sehemu tatu. Saba, sitini na mbili, na moja yaani (7+62+1=70).
Miaka hii 490 ilianza 444 BC. Malaika Gabrieli alisema, amri ya kujenga na kurejesha Yerusalemu lazima kutimiza.
- Mfalme wa Uajemi (Persia) Artaxerxes alitoa amri mwezi wa Nisan katika mwaka wa ishirini (20) wa utawala wake (444 BC). Nehemiah 2:1. 7 mara 7 ni 49 miaka-Yerusalemu ilianza kujengwa upya, mpaka mwaka wa 395 BC kazi ilimalizika.
- Malaika Gabrieli alisema kule kujenga upya Yerusalemu kutafanyika wakati wa dhiki.
- Ilibidi Nehemiah na watu wake kujenga kuta za Yerusalemu wakiwa na upanga mkono moja na kazi mkono wa pili!!
- Kazi ya kujenga upya Yerusalemu ilipo malizika ndipo ile miaka 400 ya kimya cha Mungu ilianza. Hii ni miaka 400 katikati ya malaki na Mathayo.
62×7=Miaka 434; (49+434)=483 miaka 483.
- Unapoongeza miaka 49, awamu ya kwanza, na miaka 434 awamu ya pili unapata miaka 483.
- Sasa kwa miaka 490 ukitoa miaka 483, panabaki miaka saba (7).
- Miaka saba inayobaki ndio miaka ya ile dhiki kuu ya Ufunuo 6-19.
- Malaika Gabrieli alisema katika Danieli 9:26 kwamba baada ya wiki zile 62. 62×7=miaka 434 Masihi (Mpakwa mafuta) atakataliwa mbali, naye atakuwa hana kitu, Maanake ni Yesu Kristo (Masihi) atakataliwa na kuuawa.
- Kuna mambo mawili makubwa yatakayo fanyika baada ya awamu hii ya pili (Miaka 434).
Masihi atakataliwa (33 AD).
- Masihi Maanake ni “Mashiyach” au “Messiah.”
- Messiah wa Wayahudi atakataliwa (cut-off) na atakuwa “hana kitu” yaani hatakuwa na mrithi.
- Myahudi, mwanamume kufa bila watoto au warithi ilikuwa laana-unabii ulisema hivyo.
Yerusalemu kubomolewa (70 AD).
- Malaika Gabrieli alimwambia Danieli Yerusalemu itajengwa upya, lakini Masihi atakapokataliwa Yerusalemu itabomolewa tena.
- Katika mwaka wa 70 AD, majeshi ya Roma chini ya uongozi wa Jemedari Tito waliingia Yerusalemu na kuibomoa kabisa, ikatimiza unabii wa Yesu Kristo katika Luka 19:41-44.
- Kumbuka malaika Gabrieli alimwambia Danieli unabii huu miaka 500 kabla ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo.
- Unabii wa Yesu Kristo juu ya Yerusalemu na watu wake (Luka 19:41-44) ulitimia miaka 40 baada ya Yesu Kristo kupaa mbinguni.
- Basi tupate kuona, sasa hivi leo tuko wapi katika unabii wa malaika Gabrieli.
UNABII WA MUNGU NI DHABITI-Danieli 9:27.
- Kutoka 444 BC Nehemiah 2:1 mpaka 33 AD ni miaka 483 (miaka ya Kiyahudi).
- 444 BC mpaka 33 AD ni (69×7) 483, unabii ule ulisimama katika saa ya Israeli.
- Kalenda yetu ni ya siku 365 na robo (Gregorian calendar) lakini kalenda ya Wayahudi ni siku 360.
- Saa ya unabii wa Danieli 9, sasa umesimama mpaka wakati huu wa kanisa ya Kristo ukamilike.
- Wakati huu wa kanisa ulianza 33 AD mpaka kunyakuliwa kwa kanisa, wakati tulio nao unaendelea na unaitwa wakati wa “NEEMA.”
- Hivyo hesabu ya Mungu ya miaka 490 imesimamishwa kwa sasa.
- Hivyo saa ya wa Israeli imesimamishwa na sasa ya Neema (kanisa) inaendelea.
- Hivyo tumesimama katika wiki ya 69 (7) ile saba ya mwisho tunaingojea mpaka siku ya dhiki kuu. Sasa tunaishi wakati Yesu Kristo aliuita “Nyakati za mataifa”-Luka 21:24; Warumi 11:25.
- Idadi ya watu wa mataifa kuingia katika ufalme utatimia hivi punde.
- Tafadhali soma sana Warumi 9-11, kuelewa na wakati huu wa mataifa.
- Wakati wa ile wiki ya 70 mpinga Kristo (Vs. 27) ataingia uwandani wa historia hili unabii wa Gabrieli kwa Danieli utimie.
- Kulingana na unabii huu na ishara zilizo duniani sasa Yesu yu karibu mlangoni.
- Inatubidi kuwa tayari sana.
- Dunia yote iko tayari kwa “kiongozi anayekuja duniani”-Mathayo 24.
MWISHO
- Baada ya mambo yote, Yesu Kristo atakuwa mshindi.
- Sisi tulio wa Yesu Kristo hatuko gizani juu ya historia na yote yatakaojiri hivi baadaye.
- Tukeshe, tuwe tayari ajapo Bwana Yesu Kristo.
- Kuwa tayari ni pamoja na kuokoka, kuishi takatifu na kumtumikia Yesu Kristo usiku na mchana. Amina.
The following two tabs change content below. Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.