Categories: Swahili Service

SHUHUDIA KWA KILA MTU TUMAINI LAKO

MFULULIZO: TUMAINI HAI

SOMO: 1ST PETRO 3:14-16

 

Wakristo wa Karne ya kwanza  waliteseka sana kwa ajili ya imani yao ndani ya Yesu Kristo. Pamoja na kuteswa sana hawa Wakristo walikuwa na tumaini kubwa. Petro anawaandikia kwamba wawe na moyo mkuu na kushuhudia tumaini lao kwa kila mtu. Leo tunatazama njia za kushiriki na kuwashuhudia watu wote tumaini lililoko ndani yetu. Kila wakati na tuwe tayari kushuhudia watu wote tumaini letu.

Hebu tuone:-

MTAKASENI KRISTO BWANA MIOYONI YENU-(1st PETRO 3:14).

  • Maanake “Bwana” ni “kiongozi” mkuu anaye tawala anaye miliki.
  • Wacha Yesu Kristo atawale ndani ya maisha na moyo wako kwa ukamilifu wote.
  • Ikiwa tutawashuhudia watu wote juu ya tumaini lililo ndani yetu ni lazima tukamtakaseni Kristo Bwana mioyoni yetu.
  • Tusiwe na unafiki wowote, sisi ni barua inaosomwa na kila mtu.
  • Wacha watu wote wakashuhudie upendo wa Yesu Kristo kutoka kwetu.
  • Wacha tukawe wenye huruma na fadhili.
  • Wacha watu wote wakavutiwe na maisha na mwenendo wetu.
  • Ikiwa tutamtakasa Kristo Bwana mioyoni mwetu watu watavutwa kwa Yesu. Tumaini letu litakuwa dhahiri kwa wote.
  • Katika Agano la Kale watu walitakasa vyombo maalumu vilivyo tumika kwa ibada kwa Mungu. Vifaa mbali mbali vilitengwa iwe ni viti, meza, nguo na chakula.
  • Pia siku fulani zilitakaswa hai wakati fulani katika siku kama jinsi sabato, sasa ni Jumapili hai “siku ya Bwana”(Lord’s Day)
  • Mungu anakuuliza kutenga siku moja kila juma kwa ibada na kupumzika.
  • Katika nyumba zetu tunatenga vyombo maalumu, zinatumika wakati wa wageni mashuhuri.
  • Pia tunatakasa nguo fulani kuvaa wakati maalumu, mbele ya watu wa heshima.
  • Hapa katika Agano jipya Petro anatueleza cha maana kutakasa kwa Mungu wetu ni mioyo yetu. Yaani Yesu Kristo atawale kamilifu mioyo yetu.
  • Ili maisha yetu yakawavute watu kwa Mwokozi lazima kutakasa moyo wako.
  • Wacha tukamtawaze Yesu Kristo kuwa mfalme wa maisha na mioyo yetu ndiyo watu wataona sisi ni tofauti wa walimwengu.
  • Mioyo yetu ndiyo makao ya hisia zetu (emotions), mioyo yetu ndio hasa kilindi cha maisha yetu. Upendo unatoka kwa moyo.
  • Hivyo hatua ya kwanza ya kushuhudia tumaini na imani yetu ni kumpa Yesu Kristo mioyo yetu yote, yaani kumtawaza Kristo, kumtakasa Kristo mioyoni yetu.
  • Kitakacho wavutia watu kwetu, ni Yesu Kristo anapotakaswa mioyoni yetu.
  • Yesu Kristo ni kivutio kwa watu wanaotafuta tumaini.
  • Mfanye Yesu Kristo Bwana ndani ya moyo wako – ndiposa watu wa kwenu watakapookoka (Set apart Christ as Lord in your heart).

UWE TAYARI KUWAELEZEA WATU WOTE KIINI CHA TUMAINI LILILO NDANI YAKO-(1st PETRO 3:15).

  • Muwe tayari siku zote kumjibu kila mtu aulizaye habari ya tumaini lililo ndani yenu.
  • Wakristo wengine, kweli wamemtawaza Kristo kuwa Bwana ndani ya mioyo yao lakini, wanapoulizwa kiini cha lile tumaini hawajui la kusema!!
  • Wanaulizwa, je ni kwa nini unafurahia na kutabasamu wakati wengine wako katika dhiki?-( Matendo 4:13).
  • Petro na Yohana hawakuwa watu wa elimu ya juu lakini walikuwa na Yesu aliye wapa ujasiri mkuu, hata mbele ya wakuu-(Matendo 4:18-20).
  • Uwe tayari kila siku kutoa ushuhuda wa tumaini lililo ndani ya moyo wako kwa maana Kristo ni Bwana ndani yako.

MUWE NA UPOLE, HOFU NA DHAMIRI NJEMA-(1st PETRO 3:16).

  • Tunapo mtakasa Yesu Kristo kuwa Bwana na tunapo kuwa tayari siku zote kuwajibu watu juu ya tumaini letu ni lazima kuwajibu watu kwa upole, heshima, hofu na dhamiri njema.
  • Pamoja na kuwa na juhudi na motisha ya kushuhudia ni lazima tuwe wapole wenye kuheshimu watu wote.
  • Usiwashurutishe watu kupokea tumaini lako.
  • Watu wanataka kiini hasa cha lile tumaini ulilonalo yaani Yesu Kristo.
  • Yesu Kristo alimpokea Zakayo kwa heshima hata ingawa Zakayo alimtoza ushuru aliye dharauliwa na watu wote-(Luka 19:5).
  • Wacha tukuwe kama Yesu Kristo na pia tukuwe kama ule mti wa Mkuyu.
  • Tukawe Mkuyu, watu wapande, wapate kumwona Mwokozi Yesu Kristo.

MWISHO.

  • Mtakaseni Kristo Bwana mioyoni mwenu.
  • Muwe tayari siku zote kuwajibu watu waulizaye juu ya tumaini lililo ndani yenu.
  • Muwe wapole, wenye heshima na muwe na dhamiri njema.
  • Watu watapata kuokoa!!

 

The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Rev, DR. Willy Mutiso

Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Share
Published by
Rev, DR. Willy Mutiso

Recent Posts

LEVELS OF THE ANOINTING.

SERIES: THE ANOINTING. TEXT: EZEKIEL 47:1-5   There are levels of the anointing and each…

2 days ago

UMETAKASWA KUPOKEA KIBALI.

MFULULIZO: AGANO LA UTAKASO. SOMO: ESTA 2:15-18.   Kibali cha Mungu ndicho kinacho watenga watoto…

6 days ago

THE GOD WHO SHIFTS THE HEAVENS IN YOUR FAVOR.

SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: HAGGAI 2:6-9.   God has the power to…

6 days ago

SINGING PSALMS, HYMNS AND SPIRITUAL SONGS.

SERIES: THROUGH THE BOOK OF COLOSSIANS. TEXT: COLOSSIANS 3:16   Christianity is a singing religion.…

6 days ago

GOD DEFENDS HIS CHILDREN.

SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: ISAIAH 54:17   JEHOVAH God does not abandon…

2 weeks ago

CHRISTIAN LIFE IS LIKE EAGLE’S LIFE

SERIES: THEY THAT WAIT HAVE EAGLE'S ANOINTING  TEXT: ISAIAH 40:31   The eagle symbolizes the…

1 month ago