Categories: Swahili Service

SIFA TANO ZA ASKARI WA KRISTO

MFULULIZO: SIONI HAYA

SOMO: 2 TIMOTHEO 2:3-4; 4:7-8

 

Yesu Kristo alikuwa askari wa sifa katika jeshi la mbinguni. Siku moja maisha yetu yatakwisha hapa duniani. Yesu itakapofika wakati wako, je, utakumbukwa kwa njia gani? Je, utakumbukwa kama askari wa sifa? Mtume Paulo alipomaliza kazi yake duniani alichukua wakati wa kuyaangalia maisha na kazi yake, alimwandikia mchungaji Timotheo na kumwonyesha jinsi ya kuwa askari wa sifa, askari mwema. Ulipookoka, mara hio uliingia katika jeshi la Bwana Yesu Kristo. Hivyo tangu siku hiyo unaishi katika vita. Alama moja ya askari jeshi ni majeraha yake. Tunapofika mbinguni, Kristo atataka sana kuyaona majeraha yetu. Majeraha ya askari mwema yanaonekana kwa uso, kifua, tumbo. Ikiwa majeraha yetu yamo kwa mgongo, tulikuwa askari hoi. Hebu tutazame sifa tano za askari mwema:-

ASKARI WA SIFA NI MFUASI (FOLLOWER)-2 Timotheo 2:3.

Uhusiano (relationship)

  • Hatua ya kwanza kuwa askari ni kuingia jeshi.
  • Hakuna yeyote anaweza kuwa askari bila kwanza kuingia jeshini.
  • Huwezi kuwa askari wa Kristo bila kuokoka.
  • Hii inafanyika kwa njia ya kumpokea Yesu Kristo katika maisha yako ya kibinafsi-Yohana 3:3; Waefeso 2:8-9; Matendo 16:31.

Cheo (Rank)

  • Katika jeshi lazima kuwe na mtu mkuu juu yako.
  • Kila askari wa Yesu Kristo yuko chini ya komanda-Yesu Kristo, hiyo huyo askari wa sifa ni mfuasi wa Yesu Kristo anafuata amri na mapenzi ya Mungu-1 Wakorintho 6:19-20.

Utawala (Rule)

  • Kukata amri ni kifo.
  • Katika jeshi la Kriso lazima utii, mpaka kifo-Matthayo 16:24.
  • Tunapokataa kuishi maisha haya kama Bwana apendavyo, tutakuwa wasaliti-Yakobo 4:17.
  • Askari wa sifa wa Kristo ni mfuasi.
  1. ASKARI WA SIFA NI MWAMINIFU (FAITHFUL)-2 Tim. 3-4; 4:7.

Uvumulivu wake-2:3 (faithfulness).

  • Anavumilia magumu yote, hawezi kutokea.
  • Askari wa Yesu Kristo anaelewa kwamba taabu, mabaya na shida zinatokea njiani.
  • Askari wa Yesu Kristo anaelewa kutakuwa wakati wa machungu-Yohana 16:33.

Mambo ya muhimu (priorities) 2:4.

  • Anampendeza aliye mwandika.
  • Askari wa jeshi la Kristo anapenda kumpendeza Yesu Kristo-1 Wakorintho 10:31; 1 Wakorintho 6:20.

Mazoezi yake (practice)-2 Wakorintho 4:7.

  • Anapigania kweli na amani.
  • Anaishi maisha yaletao sifa na heshima kwa Bwana-Wafilipi 2:7; Wakolosai 1:10; Wathesalonike 2:11-12.

ASKARI WA SIFA WA KRISTO ANAFAHAMU (familiar)

Anafahamu sauti ya komanda wake-Yohana 10:3-5.

  • Anatumia wakati mwingi kujizoeza sauti ya mkuu.

Anafahamu jinsi ya kutumia silaha zake-Waefeso 6:10-18.

  • Anafahamu kwamba anahusika katika vita vikuu.

Anafahamu mbinu za adui-2 Wakorinho 11:14; 1 Petro 5:8.

  • Askari wa sifa anafahamu kwamba adui hawezi kulala-Waebrania 13:5; 1 Wakorintho 10:13.
  • Mkristo mwema anaelewa sana mbinu za shetani-1 Yohana 4:4.

Askari wa Kristo anafahamu kivuli cha askari wenzake-Waebrania 11:25.

  • Askari mwema anajali sana askari wenzake-Wagalitia 6:2.

ASKARI MWEMA WA KRISTO NI MWENYE VITA-2 Wakorintho 4:7.

  • Paulo anaeleza mambo matatu yanaonyesha askari mwema.

Amejitoa-haogopi vita.

  • Wakristo wengi wametokea vita-1 Tim. 1:19-20.

Anavutiwa na vita na kuzipenda.

  • Askari mwema anapenda vita kiasi kuzililia.

Anatimiza kiapo chake cha askari kila wakati.

ASKARI WA SIFA ANAMALIZA VITA VYEMA-2 Tim. 4:7-8.

  1. Askari mwema anajikaza sana kumaliza vita.
  2. Askari mwema anao sababu ya kukaa katika jeshi.
  3. Askari mwema anao dhawabu yake-Matthayo 25:21-23.

MWISHO

  • Je, wewe ni askari wa sifa?
  • Kama bado hujajiunga na jeshi la Bwana, leo ni siku yako.
  • Unapomaliza vita vyako na maisha yako yakiisha duniani, je, utakumbukwa aje?
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Rev, DR. Willy Mutiso

Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Recent Posts

MSAADA WA MUNGU WAKATI WA MATESO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: ZABURI 46:1.   Biblia inatuakikishia kwamba Mungu wetu ni “Msaada…

3 weeks ago

GOD GUIDES OUR DESTINIES.

SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: PROVERBS 3:5-6.   Every destiny is a divine…

3 weeks ago

PUT OFF AND PUT ON

SERIES: THROUGH THE BOOK OF COLOSSIANS. TEXT: Colossians 3:5-10   We have put off the…

3 weeks ago

GOD OF THE BREAKTHROUGHS

SERIES: THE GOD WE SERVE TEXT: 2nd SAMUEL 5:17-20   Breakthroughs are divine interventions that…

4 weeks ago

WHO IS SPEAKING TO YOU?

SERIES: DRAWING NEAR TO GOD TEXT: LAMENTATIONS 3:37 It reminds believers that God's word alone…

1 month ago

CHECHEA MSHINDI ALIYE NDANI YAKO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: 1 YOHANA 5:4.   Wakristo wengi wanaishi maisha ya kushindwa…

1 month ago