SOMO: LUKA 19:28-45. (ZABURI 118)
Leo ni siku iitwayo “Jumapli ya mitende” yaani “Palm Sunday.” Juma hili ndiyo juma la mwisho ya maisha ya Yesu Kristo katika mwili hapa duniani. Ilikuwa siku ya furaha, na pia siku ya machozi.
Siku hii ya leo, miaka 2,000 iliyopita Yesu Kristo aliingia Yerusalemu kwa nderemo na shangwe kuu. Waliimba wimbo katika Zaburi 118, Hosanna “Tuokoe sasa” “Ee Bwana utuokoe, twakusihi, Ee Bwana utufanikishe twakusihi. Na abarikiwe yeye ajaye kwa jina la Bwana.” Zaburi 118:25-26 amani juu ya mbinguni na utukufu juu zaidi.
Shangwe ilikuwa nyingi kiasi Mafarisayo wakamsihi Kristo awanyamazishe wafuasi wake. Yesu Kristo akawaambia “Ninyi mkinyamaza haya mawe yatapiga kelele.”
Yesu alipokaribia mji wa Yerusalemu na kutazama, aliulilia akisema “Laiti ungalijua hata wewe katika siku hii, yapasayo amani. Lakini sasa yamefichwa machoni pako. Kwa kuwa siku zinakuja.”
Siku mbaya noma!! Zilikuwa karibu na Israeli. Mwaka wa 70AD miaka 40 baada ya kunena Yesu Kristo, Yerusalemu ilivamiwa na Tito kutoka Roma.
Hebu leo hii tutazame mambo mawili juu ya siku hii ya mitende, furaha na machozi.
FURAHA YA KUNDI NZIMA YA WATU.
- Kila mtu anapenda paredi, iwe ya majeshi, polisi au jeshi la wokovu!!
- Paredi hii ya Yesu Kristo iliudhuriwa na watu yapata 30,000-200,000.
- Katika kitendo hiki, Yesu Kristo alitimiza unabii na kutangaza unabii ambao bado huko mbele yetu.
Wakati uliopita (past); Yesu Kristo aliingia Yerusalemu kama mfalme wa unyenyekevu.
- Wakati mfalme alirudi nyumbani kutoka vita ailiingia akipanda juu ya farasi au kitu cha dhamani zaidi.
- Kaisari Julius aliporudi Roma mwaka wa 45 BC aliingia huku amepanda juu ya gari ya dhahabu ilivurutwa na ndovu 40!!
- Lakini mfalme alipopanda juu ya punda ilikuwa ni ishara ya amani.
- Watu hawa walitandaza mavazi yao na matawi ya mitende-leo Wafalme na marais wanatembea juu ya mikeka nyekundu yaani Red carpet.
- Hapa Yesu Kristo alitimiza unabii wa nabii Zakaria miaka 500 awali.
- Zakaria 9:9 “Furahi sana Ee Binti Sayuni, piga kele Ee Binti Yerusalemu; tazama mfalme wako anakuja kwako. Ni mwenye haki naye ana wokovu. Ni mnyenyekevu amepanda punda, naam mwana-punda, mtoto wa punda.”
- Vizazi vinne nyuma, Judas Maccabees , aliyekuwa akiitwa nyundo “Hammer” alifanya vita na Washamu (Syrians) waliokuwa wameitenga Yerusalemu kwa miaka mingi.
- Katika mwaka wa 163 BC Judasi aliingia Yerusalemu amepanda juu ya farasi, watu wa Yerusalemu walifurahi wakatandaza mavazi yao, huku wakipeperusha matawi ya mitende wakiimba “Hosanna, amebarikiwa yeye ajaye kwa jina la Bwana.” Aliitakasa hekalu na kufukiza uvumba akatoa sadaka na kuwakisha taa kwa siku nane.
- Judasi alikuwa shujaa wao (Wayahudi). Siku hizo waliamini Yuda alikuwa masihi.
- Mpaka leo Wayahudi usherekea sikukuu ya mataa (festival of lights)-Hanukhah.
- Baada ya mikaka michache Yudasi alikufa vitani, akazikwa, huo ulikuwa mwisho wa Yudasi (Hammer).
- Baada ya miaka 200, Yesu Kristo aliingia Yerusalemu, Uyahudi ilikuwa imekaliwa na Waroma.
- Wayahudi walidhani Yesu Kristo atawakomboa na Waroma lakini Yesu Kristo akaingia Yerusalemu amepanda juu ya punda-isahara ya amani!!
- Yudasi alikuwa mtu wa mageuzi (revolutionist).
- Lakini Yesu Kristo alikuja kama Mwokozi (Redeemer).
- Mageuzi yanaua watu, ukombozi unaokoa watu.
Wakati ujao (future) Yesu Kristo atakuja kama mfalme wa ushindi.
- Hivyo Yesu Kristo alitimiza sehemu ya unabii wa Zakaria.
- Atakapo kuja mara ya pili Kristo atatimiza sehemu ya pili ya unabii huu.
- Baada ya dhiki kuu, mataifa ya dunia yote watajitokeza kupigana naye, lakini Kristo atawashinda katika vita vya Armageddon-Ufunuo 16:12-16.
- Kristo ataingia kupitia mlango wa mashariki (East gate).
- Leo mlango wa mashariki umefungwa tangu siku hio-Ezekieli 44.
- Leo mlango wa mashariki, Yerusalemu umefungwa na waislamu wakajenga makaburi yao pale-lakini Kristo atapita pale pale!! Kristo hatajali makaburi!!
Somo kwetu.
- Hata unapojiona mdhaifu bila ukamilifu Kristo anaweza kukutumia-(punda)-1 Wakorintho 1:27.
- Usiwache mtu yeyote akuzuie kuabudu Mungu wako-Vs. 38 (Zburi 24:7).
- Mfalme Daudi walimsifu na kuabudu Mungu wake bila shaka-2 Samweli 6:14.
ILIKUWA SIKU YA MACHOZI KWA KRISTO.
- Watu walifurahi sana, lakini Yesu Kristo alilia!! (GK-“Klaio”).
- Kule Bethania kwa Lazaro Yesu Kristo alilia (Dakruo)-alilia bila sauti kuu. Lakini alipokuwa karibu na Yerusalemu, Yesu Kristo alilia (Klaio) kwa sauti kuu!!
- Leo hii mahali Yesu Kristo alilia wamejenga chapel inaitwa (Dominois Flevit) Latino Maanake (Machozi ya Bwana).
- Kwa nini Yesu Kristo alilia?-
Yesu Kristo alilia kwa sababu ya imani yao potovu.
- Aliwaona mioyo yao, walisisimuka sana. Lakini hawakumtambua kama Masihi wao.
- Baada ya siku tano, hawa watu ndio walisema msulubishe, msulubishe.
- Lao hii Kristo anaangalia ibada zetu za furaha lakini bila kutambua Mwokozi ndiye mfalme.
- Alilia kwa maana mioyo yao ilikuwa bila kujitoa (lack of commitment).
Yesu Kristo alilia kwa sababu ya upofu wa roho zao.
- “Kama leo ungalijua yaletao amani.” Lakini imefichwa mbele ya macho yako.
- Yesu Kristo aliona hukumu inayokuja duniani.
- Watu hawa hawakutambua siku ya kujiliwa kwao. Siku ya neema waliikataa.
- Mwaka wa 70AD Generali Tito aliingia kutoka Roma na kuwaua wote.
- Mpaka mwaka wa 1948, hakukuwa na taifa ya Israeli tangu 70AD-Zakaria 12:10; 13:6.
Somo la binafsi
Hatuwezi kujua amani mpaka tujisalimishe kwa Yesu Kristo (Amani katika moyo, maisha, jamii, ndoa, kazi).
- Amani inakuja tu tunapompokea Yesu Kristo ndani ya maisha yetu-Yohana 14:27.
Kumkataa Yesu Kristo matokeo yake ni hukumu.
- Mwaka wa 70AD hukumu iliwajia wote Yerusalemu na hekalu lake zilichomwa moto.
Chochote kinachomfanya Yesu Kristo kulia kinahitaji kuvunja mioyo yetu.
- Je, ni lini ulilia kwa mji wako, taifa lako, jamii yako, watoto wako?
- Je, mzigo wako ni nini? Machozi yako yako wapi?
MWISHO
- Mstari (vungu) la 44 ni huzuni nyingi-hawakutambua siku yao, siku ya kuokoka, siku ya neema kwao.
- Je, umetambua na kumpokea Yesu Kristo aliye amani yako na Mwokozi wako?
The following two tabs change content below. Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.