SIMEONI– ALITARAJIA FARAJA YA MUNGU

LUKA 2:25-35

UTANGILIZI

Simeoni alikuwa moja ya wale Mungu          aliwaficha, wakati wa giza kuu ulimwenguni.   Miaka 400 ya kimya cha Mungu. Mbingu     ilifungwa kutoka Malaki mpaka mathayo. Lakini katika hayo yote Simeoni alitembea na Bwana katika nguvu za roho mtakatifu. Lakini sasa Mungu amemleta Simeoni katika nuru, Simeoni aliomba kwa siri, lakini sasa Mungu amemzawadi adharani. Simeoni alimtumikia Bwana kwa kungonja, matarajio ya faraja ya Mungu. Yesu Kristo ndiye faraja ya watakatifu. Hebu tuone:-

I.   ONA UTAKATIFU WA SIMEONI

  1. Simeoni alikuwa mwenye haki na mcha Mungu (V.25)
  • Simeoni alikuwa mwenye haki kwa kuwatendea watu na mcha Mungu katika kumtendea Mungu.
  • Pande mbili za Mkristo ni kuwatendea watu haki na kumcha mungu
  • Ni lazima tuwe wakweli mbele ya watu na wa kweli mbele za Mungu
  1. Simeoni alitarajia faraja ya Israeli.
  • Simeoni alitarajia akagoja kwa maombi kwa maana kwa Imani alimwamini Mungu wa Israeli.
  • Simeoni hakuwa na Imani katika mwingine isipokuwa Mungu na kuja kwa Masihi aliye mfalme.
  • Simeoni alisimama kwa maandiko kwamba “Mungu amefariji Sayuhi” (Isaya 51:3)
  • Kungoja na kutarajia kwa Simeoni kulipata dhawabu ya Mungu, tumaini lake lilitimia (Isaya 49:23) wanaomngojea Bwana hawataaibika kamwe.
  • Wewe kamngojea Bwana kwa subira (Isaya 40:28-31)
  1. Simeoni—Roho mtakatifu alikuwa juu yake.
  • Kumngojea Mungu na kujazwa Roho mtakatifu kunaenda pamoja (Matendo 2:1-4)
  • Kwa maana Simeoni alijazwa Roho Mtakatifu mambo mawili yalitendeka kwake.
  1. Alifundishwa na Roho Mtakatifu – alikuwa ameonywa na Roho mtakatifu kwamba hataona mauti kabla ya kumwona Kristo wa Bwana.
  2. Aliongozwa – akaja hekaluni akiongozwa na Roho mtakatifu (Warumi 8:14)
  • Tunapojazwa Roho Mtakatifu, tunamngojea Bwana, tunaishi katika haki na kumcha Bwana huku tukifundishwa na kuongozwa na Roho mtakatifu.

 

II.  SIKIA USHUHUDA WA MZEE SIMEONI

  • Simeoni alinyosha mikono ya imani na maombi akampokea Yesu Kristo.
  • Simeoni alikuwa tayari kwenda mbinguni maana macho yake yamemwona aliye     wokovu – yaani Kristo
  1. Yesu Kristo ndiye wokovu wa Mungu “macho yangu yameuona wokovu wako” (V.30)
  • Kumuona Kristo ni kuwa tayari kwenda mbinguni kukaa na Kristo (Isaya 52:10-12)
  1. Yesu Kristo ndiye nuru ya kuwa mwangaza wa mataifa (V.32)
  • Kristo ndiye nuru ya mataifa – hamna nuru nyingine duniani (Isaya 9:2, I Yohana 1:7)
  1. Kristo ni utukufu wa Israeli (V.32)
  • Kristo kwanza atawaokoa mataifa halafu awe utukufu kwa Israeli (Yohana 1:12)
  • Kristo ni wokovu wetu, Kristo ni nuru yetu Kristo ni utukufu wetu – sifa kwa Mwana Kondoo.

 

III. SIKIA UNABII WA SIMEONI (V.34-35

  1. Misioni (SHABAHA) YA KRISTO (MISSION OF CHRIST) V.34
  • “Huyu mtoto amewekwa kwa kuanguka na kuinuka wengi walio katika Israeli”
  • Wanafunzi wake walimuacha.
  • Wengi walianguka na kuinuka Israeli, Sauli, Zakayo.
  • Israeli kama taifa wameanguka (Warumi 9:12)
  • Israeli kama watu wa Mungu, watainuka (Warumi 9:26)
  1. Tabia ya Kristo.
  • Kristo atakuwa “ishara itakayonenewa”   (Isaya8:14, Mathayo 21:42, I Wakorintho 1:23)
  1. Mawazo ya mioyo mingi yatafunuliwa (V.35)
  • Msalaba ni asili ya mema kwa wale wanaokoka lakini msalaba ni asili ya mabaya kwa wale wamepotea (I Wakorintho 1:18, Warumi 2:4, Isa 5:24, Yeremia 6:10, 8:9, Zekaria 7:12)

 

 

MWISHO

  • Je, kama Simeoni umemwona Mwokozi na wokovu wa Mungu kwako, binafsi?
  • Je, Kristo ni faraja zako katika dunia hii?
  • Je, umeokoka? Leo mjie aliye faraja.

 

 

The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Rev, DR. Willy Mutiso

Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Recent Posts

MSAADA WA MUNGU WAKATI WA MATESO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: ZABURI 46:1.   Biblia inatuakikishia kwamba Mungu wetu ni “Msaada…

3 weeks ago

GOD GUIDES OUR DESTINIES.

SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: PROVERBS 3:5-6.   Every destiny is a divine…

3 weeks ago

PUT OFF AND PUT ON

SERIES: THROUGH THE BOOK OF COLOSSIANS. TEXT: Colossians 3:5-10   We have put off the…

3 weeks ago

GOD OF THE BREAKTHROUGHS

SERIES: THE GOD WE SERVE TEXT: 2nd SAMUEL 5:17-20   Breakthroughs are divine interventions that…

4 weeks ago

WHO IS SPEAKING TO YOU?

SERIES: DRAWING NEAR TO GOD TEXT: LAMENTATIONS 3:37 It reminds believers that God's word alone…

1 month ago

CHECHEA MSHINDI ALIYE NDANI YAKO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: 1 YOHANA 5:4.   Wakristo wengi wanaishi maisha ya kushindwa…

1 month ago