Categories: Swahili Service

TUENENDE KWA MAPITO YA ZAMANI

MFULULIZO: SIONI HAYA KWA BWANA.

SOMO: YEREMIA 6:16; 2 TIMOTHEO 4:1-4

 

Tunahitaji mapito ya zamani kwa sababu mapito ya zamani ndio yale tuliyapokea kutoka kwa Mungu Baba na ndiyo yatakayo timiza kazi ya Yesu Kristo. Tunaishi katika nyakati hatari. Nyakati ambazo watu wamekataa mapito ya zamani.

Mapito ya zamani aliyapitia Habeli, Sethi, Methusela, Nuhu, Ibrahimu, Isaka, Yakobo, Daudi, Isaya, Yeremia, Petro, Paulo, Yohana na Mitume.

Mapito ya zamani ni mapito ya wokovu, ubatizo wa Roho Mtakatifu, msamaha wa dhambi na kiyama ya wafu.

Mapito ya zamani ni kukana dhambi, kutembea katika utakatifu, kumwishia Yesu Kristo, kukaa katika kumgojea Kristo mpaka ajapo.

  • Madhehebu mengi yameacha njia na mapito ya zamani. Juzi Papa Francis amesema masonga ni sawa, hakuna dhambi kewa mwanaume kumwoa mwanaume, mwanamke kumwoa mwanamke. Huo pia ndio msimamo wa Anglican na madhehebu mengine mengi.
  • Mapito ya zamani ni mapito ya utakatifu.
  • Wabaptist pia wamegawanyika kwa wengine kuacha mapito ya zamani.
  • Paulo anamwandikia Timotheo anamshauri kufuata mapito ya zamani- 2 Timotheo 2:2.
  • Hebu tuone mashauri ya Paulo kwa Timotheo juu ya kutembea mapito ya zamani:-

MAAGIZO KWA WATU WA MUNGU- 2 Timotheo 4:1-2

Hii ni Amri ya kijeshi. Hivyo ni amri ya Paulo kwake Timotheo.

Siku ya hukumu yaja- 2 Wakorintho 5:10; Warumi 14:12.

  • Kwa sababu kila mmoja wetu lazima kusimama mbele za Mungu, tunahitaji kuwa waaminifu mbele za Mungu.
  • Tunahitaji kuwa bila hofu mbele za mwanadamu, kutafuta utukufu wa Mungu pekee.

Maagizo ya Paulo kwa Timotheo.

  • Hubiri neno- dumu katika Biblia pekee.
  • Uwe tayari wakati ukufaao na wakati usiokufaa.
  • Tumia kila wakati na nafasi.
  • Kila wakati fanya mwaliko wa kuokoka na kauli ya kuacha dhambi.
  • Karipia (Reprove)- oyesha watu dhambi zao.
  • Kemea- (Rebuke).
  • Watu wanahitaji kuelezwa dhambi ni mbaya na dhambi inayo matokeo yake.
  • Onya- (Exhort)- waonyeshe watu dhambi zao na njia ya kuepuka dhambi na hukumu zake.
  • Vumilia- huenda watu hawatatii neno hapo hapo, lakini endelea kuhubiri.
  • Mafundisho mema ni kueleza na kutekeleza. Watu lazima kufundishwa neno.

CHANGAMOTO YA UJUMBE WA MUNGU- 2 Timotheo 4:3

Watakataa neno la Mungu.

  • Hata wengine watakataa- Yohana 6:66.

Utajipatia walimu makundi makundi.

  • Watu wataamua kile wanataka kusikia.
  • Watu watakuwa na masikio ya utafiti.

Mapenzi ya mioyo yao.

  • Hawatapenda neno la kweli.
  • Watasikiza wanayopenda.

Siku na nyakati hizo ni siku za leo.

  • Watu wameshika dini sana lakini hawamjui Yesu Kristo- 2 Timotheo 3:1-7.

WATAGEUZA MAPITO YA MUNGU- 4:4

  1. Watachagua kwenda kwa mapito yao wenyewe, bali na kweli ya Mungu.
  2. Watageukia hadithi za uongo, lakini hakuna njia nyingine ya kuokoa- Yesu Kristo pekee- Yohana 14:6.
  3. Watu wataamini uongo na kukata kweli.

 

MWISHO

  • Leo tuamue mbele ya Mungu kutembea katika mapito ya zamani- Yeremia 6:16.
  • Sahau madhehebu na kukaa katika mpango wa Mungu- fanya mapenzi ya Mungu.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Rev, DR. Willy Mutiso

Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Share
Published by
Rev, DR. Willy Mutiso

Recent Posts

DAMU YA UTAKASO.

MFULULIZO: AGANO LA UTAKASO. SOMO: KUTOKA 12:12-13.   Damu ya Yesu Kristo ndiyo mhuri wa…

3 days ago

KEY TO DIVINE SPEED.

SERIES: SUPERNATURAL ADVANCEMENT. TEXT: HABAKKUK 3:19.   The journey of fulfilling your destiny does not…

3 days ago

BE YE THANKFUL TO GOD.

SERIES: THROUGH THE BOOK OF COLOSSIANS. TEXT: COLOSSIANS 3:15   Thankfulness is a great attitude…

3 days ago

LEVELS OF THE ANOINTING.

SERIES: THE ANOINTING. TEXT: EZEKIEL 47:1-5   There are levels of the anointing and each…

6 days ago

UMETAKASWA KUPOKEA KIBALI.

MFULULIZO: AGANO LA UTAKASO. SOMO: ESTA 2:15-18.   Kibali cha Mungu ndicho kinacho watenga watoto…

1 week ago

THE GOD WHO SHIFTS THE HEAVENS IN YOUR FAVOR.

SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: HAGGAI 2:6-9.   God has the power to…

1 week ago