MFULULIZO: 1 PETRO-YESU KRISTO, TUMAINI LETU.
SOMO: 1 PETRO 1:1-12, WAEBRANIA 11:1
Yesu Kristo yu hai, basi uwe na hakika na furaha hata wakati wa shida na mateso. Furaha hata wakati wa shida na mateso. Mtume Petro aliandika kwa wakristo waliokuwa katika uamisho, wametapakaa kote katika Asia Minor (Asia Ndogo). Mahali sasa ni Uturuki kaskazini. Maanake Neno “utawanyiko” V. 1 ni kwamba hawa wateule Wayahudi wakristo walikuwa mbali na nyumbani kwao (Israeli). Kwa sababu ya mateso kutoka serikali ya ufalme wa Roma hawa wateule katika Kristo walijikuta katika utawanyiko, walijikuta katika hali ya ugeni katika Ponto, Galatia, Kapodokia na Asia na Bethania.
Mfalme Niro alianza kuwatesa wakristo wateule, hivyo wengi wakatawa nyika kwa kuhofia maisha yao.
Hata hivyo kulikuwa na tumaini kwao na kwetu pia, kwa maana hata ingawa tunaishi Kenya, mara twajiskia wageni katika ulimwengu huu kwa yale yanaendelea-(1 Petro 1:1-2).
Kufufuka kwa Yesu Kristo kunatupa “Tumaini hai” Katikati ya majaribu na mateso.
Tumaini tulio nalo ni tumaini la hakika, tumaini la ukweli, tumaini linalobadilisha maisha yetu.
Mahali pote Yesu Kristo amehubiriwa na kupokelewa matokeo mengi na tumaini limepatikana.
- Wanawake wamepewa heshima na Watoto walio katika mimba wameheshimiwa. Ukalinganisha na mahali kote Injili ya Yesu Kristo, bado hubiriwa.
- Hospitali zimejengwa na matibabu yametolewa bila Ubaguzi wa Rangi au jinsia.
- Wagonjwa hata wale wa ukoma, ukimwi na maradhi yote wameifadhiwa vilivyo.
- Uchumi na Elimu zimepatikana katika nchi. Injili ya Yesu Kristo imehubiriwa.
- Utawala bora na haki za wanadamu zimepatikana Yesu Kristo alipo.
- Kufufuka kwa Yesu Kristo ni tumaini la uzima, tumaini hili limeleta mabadiliko (1 Petro 1:3). Hebu tujifuze:-
UWE NA HAKIKA KWA SIKU ZIJAZO HATA MAMBO YAWE NAMNA GANI LEO-(1 Petro 1:4).
- Uwe na hakika kwa matumaini yako.
- Kufufuka kwa Yesu Kristo ni tumaini Kwetu sisi tuliookoka.
- Ikiwa Yesu Kristo alifufuka kutoka kaburini, haijalishi shida zako leo, utatoka kwa shida zako leo.
- Kwa sababu Yesu yu hai leo, umepata tumaini la kesho.
- Uwe na hakika juu ya nafasi yako mbinguni, maana umezaliwa upya kwa “tumaini hai.”
- Kumbuka upata urithi Usioharibika, usio na uchafu, usionyauka ilivyotuzwa mbinguni kwa ajili yako-(V. 4).
- Urithi na mali ya dunia hii unaharibika kulingana na miaka yake.
- Kwa sababu Kristo amefufuka kwa wafu tumepata Urithi Usio weza kwaribika.
UWE NA HAKIKA JUU YA WOKOVU WAKO, MUNGU ATAKULINDA NAFSI YAKO MPAKA MILELE-(1 Petro 1:5).
“Nanyi mnalindwa na Nguvu Za Mungu. Kwa Njia ya Imani hata mpate wokovu ulio tayari kufunuliwa wakati wa mwisho.”
- “Tunalindwa” hii ni Neno la Kijeshi.
- Tumezingirwa na jeshi la mbinguni kutokana na Adui.
- Wokovu wako katika Kristo huwezi kupotea hata kamwe, shetani, daimoni, magonjwa na hata mauti haiwezi.
- Tumelindwa na nguvu za Mungu.
- Kama ni sisi tunajilinda basi hatuna nguvu wala Neema Ya Kutosha.
- Petro alipojaribu kujilinda na nguvu zake alishindwa, lakini sasa anakiri amelindwa na Nguvu za Mungu (Eternal Security). Hizi nguvu za Mungu zinaitwa DUNAMIS kwa Kigiriki!!
- Tumaini Nguvu za Mungu Kulinda wokovu wako na pia maisha yako.
- Yesu Kristo amefufuka kwa wafu hivyo uwe na hakika kwa utukufu wako kwake hata mambo yawe namna gani.
UWE NA FURAHA HATA WAKATI WA MAGUMU (1 Petro 1:6).
- Furaha hata wakati wa mashaka na uchungu, sherekea wakati wa kilio (1 Petro 1:6).
- Kwa sababu tunafahamu ya kesho yatakavyo kuwa, tunafurahi katika majaribu na mateso!!
- Tumaini lako linapokuwa ndani ya Yesu Kristo unaweza kufurahi katika chochote maisha inarusha kwa njia yako!!
- Yesu Kristo amefufuka kwa hivyo furaha siku zako zote.
MSIFU MUNGU KWA MATUNDA BORA YATAKAYOZALIWA NA IMANI-1 Petro 1:7.
- Majaribu yanakuja kuonyesha kama imani yetu ni dhabiti na ya kweli.
- Mungu anaachilia majaribu kwa maisha yako, si hili uanguke, lakini kuonekane kama imani yako na ya kweli.
- Ikiwa imani yako iko katika kingine isipokuwa Yesu Kristo pekee, majaribu yatakuchoma!!
- Ikiwa imani yako iko katika Yesu Kristo imani yako itasafishwa kuwa safi.
UWE NA FURAHA KWA SABABU YA SIFA ZITAKAZO TOKEA-1 Petro 1:8-9.
- Utashukuru kwa sababu majaribu kwako yanakuleta karibu na sababu ya imani yako-Wokovu.
- Mwisho wa imani yetu ni wokovu wa roho zetu.
- Hatujamuona Kristo kwa macho hii ya mwili lakini twampenda.
- Hata sasa hatumwoni Yesu Kristo, lakini twamwamini-Waebrania 11:1.
- Lengo hasa ya imani yetu ni wokovu wa mwisho-yaani kukombolewa kutoka kwa uwepo wa dhambi.
FURAHINI KWA MAANA YA HESHIMA KUU NA NEEMA KUBWA ZAIDI TULIOPOKEA KATIKA KRISTO YESU-1 Petro 1:10-12.
- Sisi tumepokea mambo mema na makuu zaidi kuliko manabii na malaika.
- Manabii wa Agano la Kale hawakujua tunayojua leo.
- Manabii na pia malaika walifanya utafiti juu ya wokovu huu tulionao.
- Lakini hawakupata neema ya kuelewa kama sisi wateule wa baada ya kufufuka kwa Yesu Kristo.
- Manabii wote, toka Adamu, Henoko, Nuhu, Ibrahimu, Musa, Isaya, Eliya, Ezekieli, Danieli, Yeremia na wenzao.
- Malaika Mikaeli, Gabrieli na Maserafi hawakujua wala kufahamu wokovu kama jinsi sisi, lakini walitafuta-tafuta na kuchunguza-chunguza.
- Hawakujua ni wakati gani na kwa njia gani-Injili hii tulionayo.
- Lakini wewe na mimi tumepata neema kuu-kuokoka na kufahamu Yesu Kristo.
MWISHO.
- Tunahitaji kuwa na hakika ya mambo haya yote. Tuwe na hakika juu ya wokovu wa binafsi.
- Usitazame dunia hii, bali umtazame Yesu Kristo.
- Usitegemee ahadi za watu, siasa, na jamii.
- Tazamia na kushika ahadi zake Mwokozi wako-Yesu Kristo.
The following two tabs change content below. Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.