Categories: Swahili Service

TUMAINI KWA JAMII.

MFULULIZO: TUMAINI HAI .

SOMO: 1 PETRO 3:1-7.

 

Ni jambo la kushangaza kwamba ndoa za Wakristo zinaendelea kuvunjika kama vile ndoa za wapagani. Je, kuna tofauti dhidi ya ndoa za Wakristo na ndoa za dini zingine? Sisi kama Wakristo tunahitaji kuwa tofauti, lakini ni huzuni ndoa zetu kama Wakristo ziharibike sawa kama tunaposhuhudia leo. Mtume Paulo, ambaye alikuwa na mke na jamii, pamoja  na kuwa na shughuli nyingi kama Mtume mkuu anapata kuwaandikia wanawake Wakristo na mume zao na zaidi wanawake waliokuwa na waume wasiookoka kama wao.

Petro anawaandikia akiwaeleza jinsi ya kuwavuta waume zao kwa Yesu Kristo pasipo kuwahubiri neno lakini kuwavuta kwa Yesu Kristo kwa mienendo yao nzuri.

Pia mtume Petro anawaandikia waume huku akiwaelimisha jinsi ya kuishi na wake

zao. Hata ingawa Mtume Petro anatumia vifungu 6 (sita) kuwahimiza wanawake na

fungu moja (1) tu kwa wanaume, kile kifungu kimoja kwa wanaume kimejaa

mashauri makuu kwa wanaume.

Leo hii, haijalishi kama wewe umeoa, umeolewa, bado wewe ni pekee (single), mjane,   umeachwa ndoa, talaka au umejitenga au bado unatafuta ndoa, ujumbe huu ni kwetu sisi sote.

  • Kwanza ninaomba tuelewe na mambo mawili ambayo tusipoyaelewa kibiblia yataleta sura mbaya juu ya ndoa.
  1. Ikiwa tutaenda zaidi ya mapenzi na kuingia katika ukweli na kujenga maisha ya kudumu katika ndoa, ni lazima kuwa na mtizamo wa kibiblia juu ya ndoa.
    • Ndoa za kujichagulia mchumba (mme/mke) zinajengwa zaidi juu ya kuvutiwa na urembo, tabasamu, akili, umbo, elimu, pesa, jamii na mambo mengi ya nchi (physical attributes). Lakini umbo na urembo vinabadilika na miaka ya umri.
    • Baada ya miaka kupita mambo yanabadilika, nyumba haisafishwi kama zamani, farakano juu ya ngono na tendo la ndoa na mengine mengi-kama magonjwa ya uzee, afya kudhoofika, kuingiliwa na jamii, na pressure ya watoto na wajukuu, kazi, kustaafu, uchumi.
    • Ndoa za kupangiwa (arranged marriages) zinakuwa nafuu zaidi kwa sababu hizi ndoa hazikusimama juu ya sura, urembo, fedha na elimu, hizi ndoa zinadumu zaidi.
  2. Ndoa kudumu zinahitaji kujengwa juu ya Biblia. Badala ya kujiuliza “Je, huyu ndiye anayefaa?” tutajiuliza “Je, mimi ninamfaa huyu mke au mume?”
    • Badala ya “Je huyu ndiye atakaye tosha mahitaji yangu?” tujiulize, “Je, huyu ndiye tutaweza kujenga ndoa pamoja?”

Neno la maana sana katika sura hii ni neno NYENYEKEA.

Tayari tumeona kwamba neno, “Nyenyekea” haipendwi na watu wengi duniani, hata kanisani.

Kunyenyekea, kama jinsi heshima si utumwa.

  • Kunyenyekea Maanake ni kutambua mamlaka ya Mungu juu ya maisha yetu.
  • Kunyenyekea ni neno la kijeshi, Maanake ni kusalimu amri na mamlaka chini ya mtu mwingine.
  • Kunyenyekea ni kuchukua nafasi yako chini ya mamlaka yaliyowekwa (chain of command).
  • Mtume Petro na Mtume Paulo wanatumia neno kunyenyekea kumaanisha kujitiisha chini ya mamlaka na amri ya mwingine.
  • Kunyenyekea ni kujiitisha chini ya mtu mwingine katika nia ya kumpendeza yeye.
  • Kunyenyekea ni jambo la kuchagua.
  • Mbele ya Mungu mwanaume na mwanamke ni sawa kidhamana, lakini Mungu ameamrisha mwanamke kunyenyekea mume wake kwa hiari yake.
  • Mungu hajapendekeza mume amtiishe mke wake kwa nguvu, fujo au kwa kumsurutisha mke wake.
  • Ndiposa, hatimaye Biblia inaamuru mume na mke kunyenyekea katika kicho cha Kristo.
  • Mtume Petro chini ya mwongozo wa Roho Mtakatifu ametupa mpangilio kamili juu ya kujenga ndoa zenye furaha, amani, tumaini, takatifu na afya.
  • Biblia haifundishi wanawake kukaa katika ndoa zinazotisha maisha yao na ya watoto wao. Kunyenyekea si kukaa ndani ya ndoa mbaya.
  • Mtume Petro ametoa amri tatu. Amri hizi ni za maana, ni rahisi kutekeleza na zinafanya kazi katika kila tamaduni. Hebu tujifunze:-

MWANAMKE ANGALIA, TUNZA NA LINDA MATENDO YAKO-1 Petro 3:1-2.

  • Mahitaji makuu ya mwanaume ni kupewa heshima na mke wake.
  • Wanaume wanahitaji sana heshima hata kuliko kupendwa. Dharau ni chukuizo kwa kila mwanaume.
  • Mwanaume anahitaji kusifiwa na kuabudiwa.
  • Mwanaume hili ajisikie mwanaume ni lazima kujua kwamba anahitajika.
  • Mtume Petro anasema, “Enyi wanawake, kama jinsi Yesu Kristo alivyokuwa kielelezo chema cha kunyenyekea Mungu Baba, sasa hata nyinyi nyenyekeeni mume wako.”
  • Nyenyekea mume wako, wala si kunyenyekea mume wa mwingie.
  • Kila mwanamke anao kipawa cha unyenyekevu na hawezi kuwa na amani na furaha bila kunyenyekea mwanamume.
  • Unyenyekevu wako kwa mume wako usiwe na masharti.
  • Vifungu hivi havikuandikiwa wanawake ambao mume zao ni wakamilifu.
  • Vimeandikiwa wanawake mume zao bado kuokoka. Mume hawa wako mbali na Mungu, walevi, wasumbufu.
  • Wanawake hawa hata ingawa walikuwa kanisani walikuwa wanatumia njia za kuwasurutisha mume zao (manipulation).
  • Wanawake wengi wanatumia njia nyingi pamoja na kuhubiria mume zao (pouting, sulking, scheming, bargaining, nagging, coercing, humiliating).
  • Wanawake wanaotumia njia hizi-ni wanawake wasio mtumaini Mungu wao kubadili mume zao. Huwezi kubadilisha mume wako awe kitu ambacho si yeye-Mungu pekee anaweza kubadilisha watu.
  • Wanawake, muwe wake wema kwa mume zenu, huku mkiwatumikia mahitaji yao.
  • Petro anasema huenda hutamvuta mume wako kwa Yesu Kristo kwa kumhubiria kila wakati, lakini kwa Matendo mema (silent life).

MWANAMKE TAZAMA SANA MAVAZI YAKO, KUJIPODOA KWAKO NA NIA NA MOYO WAKO-1 Petro 3:3-6.

  • Petro anatumia neno (adorning) kujipodoa kwa nje-neno hili kwa kigiriki ni neno (KOSMOS), kingereza ni neno Cosmos, kinyume cha CHAOS.
  • Petro anawaeleza wanawake Wakristo wasiyaangalie mambo ya nje (mwili) tu lakini walinde sana tabia zao (mwanamke ni tabia).
  • Tuelewe kwamba hawa wanawake walikuwa na desturi ya kiroma (Roman women). Hata leo wanawake Waitaliano wanajipodoa sana, kama jinsi wanawake wa Kihindi na Kiarabu.
  • Walipenda sana mashindano ya mavazi na nywele.
  • Walipenda sana dhahabu, fedha kwa pete na mania ya masikio, kitovu, ndimi.
  • Walipenda sana mavazi ya bei, lengo ilikuwa wajipendekeze kwa wenzao.
  • Unapotazama OSCARS katika T.V unaona jinsi wanawake matajiri wanavyo vaa mavazi ya dhamani.
  • Hivyo ndivyo wanawake wa Karne ya kwanza mle Roma waliovaa.
  • Neno la Mungu kwa wanawake Wakristo ni kujitunza na kulinda mioyo yao kama jinsi wanavyojipodoa nje. Lakini hii si kusema mwanamke asivae vizuri. Urembo wa nje ni vyema, lakini isiwe kila watu wanaona kwako ni mavazi pekee bila kuona mtu wa yale mavazi.
  • Nyumba ikiitaji rangi, lazima kupaka rangi!!

MWANAMKE NA MWANAUME KAGUA SANA MWENENDO WAKO-1 Petro 3:5-7.

  • Petro anasema, Sara alimtii Ibrahimu na kumwita “Bwana”, yaani Sara alimdhamani sana Ibrahimu.
  • Sara alimtii Ibrahimu na kumpa heshima.
  • Sara ndiye mfano wa kila mwanamke wa imani ndani ya Yesu Kristo.
  • Kwa sababu ya heshima ya Sara kwa Ibrahimu, Ibrahimu alifanya chochote Sara alipendekeza!!
  • Ukinyenyekea mume wako, mume wako atafanya mapenzi yako dada!!
  • Kwa wanaume Petro anawaambia wote, kunyenyekea mke wao!! “Likewise” kadhalika.
  • Wanaume pia na wao wafuate mfano wa Yesu Kristo katika utii na unyenyekevu.
  • Kifungu hiki cha saba (7) ni kwa wanaume na kina amri tatu kwao:-
  1. Ishi pamoja na mke wako.
  • Kaa karibu na mke wako. Ishi pamoja naye, nyumba moja naye. Ishi chumba kimoja naye, ishi kitanda moja naye-Waefeso 5:31.
  • Ndoa ni uhusiano wa mwili na roho kwa mume na mke wake.
  • Mume na awe nyumbani na mke wake.
  1. Mfahamu mke wako.
  • Mjue mke wako kabisa, fahamu jinsi ameundwa.
  • Kumfahamu manamke ni kibarua kikubwa sana.
  • Kila mwanamke ni kiumbe pekee katika chapa na sura ya Mungu.
  • Unahitaji wakati na subira nyingi sana.
  • Tafuta ufahamu kwa maombi. Mahitaji makuu ya mwanamke ni kupendwa kwa neno na kwa Matendo (love).
  • Mahitaji ya pili ni usalama, ulinzi na hifadhi (security).
  • Mahitaji ya tatu ni kutoshelezwa (provision).
  • Je, wewe ni mwanaume anayeweza kutumainiwa kutimiza mahitaji ya mwanamke?
  • Mwanamke pia aliumbwa na sura na chapa ya Mungu, hivyo anahitaji kipindi cha sifa na ibada (praise and worship) pamoja na uwepo wa mume wake.
  1. Mheshimu mke wako.
  • Mpe mke wako heshima (honor), mdhamini sana.
  • Mdhamini mke wako juu ya yote, isipokuwa Mungu wako!! (Mungu kwanza, mke namba mbili).
  • Ikiwa wewe hutafanya mambo haya matatu, maombi yako yatazuiliwa.
  • Ikiwa hutasikizana na mke wako, maombi yako haitafika mbinguni.
  • Wewe na mke wako ni waridhi pamoja (kitu moja)-Mathayo 5:23-24.

MWISHO

  • Je, wewe na mke au mume wako, nyinyi ni washindani au marafiki (partners)?
  • Je, wewe na mke wako mnasidishana kuwa kama Yesu Kristo?
  • Je, mnajuana kindani, Je, maombi yenu yanajibiwa?
  • Je, mnapenda kuwa pamoja au furaha yenu ni mkiwa mbali mbali, au unaishi bila neema?
  • Mungu atupe neema yake.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Rev, DR. Willy Mutiso

Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Share
Published by
Rev, DR. Willy Mutiso

Recent Posts

LEVELS OF THE ANOINTING.

SERIES: THE ANOINTING. TEXT: EZEKIEL 47:1-5   There are levels of the anointing and each…

2 days ago

UMETAKASWA KUPOKEA KIBALI.

MFULULIZO: AGANO LA UTAKASO. SOMO: ESTA 2:15-18.   Kibali cha Mungu ndicho kinacho watenga watoto…

6 days ago

THE GOD WHO SHIFTS THE HEAVENS IN YOUR FAVOR.

SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: HAGGAI 2:6-9.   God has the power to…

6 days ago

SINGING PSALMS, HYMNS AND SPIRITUAL SONGS.

SERIES: THROUGH THE BOOK OF COLOSSIANS. TEXT: COLOSSIANS 3:16   Christianity is a singing religion.…

6 days ago

GOD DEFENDS HIS CHILDREN.

SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: ISAIAH 54:17   JEHOVAH God does not abandon…

2 weeks ago

CHRISTIAN LIFE IS LIKE EAGLE’S LIFE

SERIES: THEY THAT WAIT HAVE EAGLE'S ANOINTING  TEXT: ISAIAH 40:31   The eagle symbolizes the…

1 month ago