DANIELI 8 :23-27
UTANGULIZI
Biblia ni kitabu kigumu kuelewa. Zaidi sana kuelewa ni sehemu ya Biblia juu ya unabii. Kila mhubiri anayotafsiri yake, hivyo wakristo wengi wanakaa katika hali ya kuchanganyikiwa. Leo tujifunze juu ya mtu wa shetani atakayeitwa mpinga Kristo (Antichrist)
Wengi katika kanisa hawaelewi kitakacho wadia, hivyo si wengi wako tayari kumlaki Kristo arudipo. Kwa maana wakati ni mfupi sana tunahitaji kujua ukweli wa Mungu. Mpaka leo watu billioni 40 wameishi duniani tangu Adamu na Hawa katika bustani ya Edeni. Kutoka wakati huo mpaka sasa dunia imeshuhudia watu wengi wenye juhudi, vipawa, werefu, wenye nguvu na uwezo. Lakini katika hawa wote hakuna wa kulinganisha na huyu mtu atakayeitwa mpinga Kristo (The Antichrist).
Mpinga Kristo atakuwa mwenye nguvu na uwezo,mdanganyifu sana, mwerefu, mbaya sana, mkatili zaidi, mwenye kutekeleza. Mpinga Kristo atakuwa kilele cha enzi ya mwanadamu bila Mungu, (Yaani humanistic secularism). Mpinga Kristo atakuwa mtu wa shetani.
Hebu tuone:-
I. KUTOKEA KWA MPINGA KRISTO– MTU SHETANI (8:23)
- Baada ya ufalme wa watu wa mataifa, mfalme mkali sana atasimama juu ya dunia hii.
- Hali ya dunia wakati huo.
- Dunia itakuwa katika hali ya makosa (Impunity)
- Dhambi itakuwa imetimia kabisa. Luka 17:26-27, 2 Tim 3:1-5)
- Dunia tayari hiko katika hali ya dhambi na uasi mkuu.
- Mchafuko wa dini (II Wathes.2:3)
- Ukengeufu- (A falling away) Apostasy
- Kanisa litakuwa limeacha ukweli wa neno la Mungu (Doctrines)
- Madhehebu yajiuza kwa shetani.
- Saa hii, madhehebu mengi Kenya yameuzwa kwa ibada za shetani, maasifu wengi wamejiunga na mpinga Kristo.
- Wachungaji wengi wamejiunga na vyama vya wachungaji wanao tumikia shetani.
- Wachungaji kama waalimu wako karibu na sadaka anazotaka shetani (Yaani kafara za wanafunzi na washiriki)
- Sasa doctrine na mafundisho ya msingi ya ijili yameachwa- (Virgin birth, substitutionary death, resurrection, second coming of Christ, salvation etc)
- “Ukengeufu” (Apostasy) umeifika kanisani. Wachungaji wengi sasa wana wake zaidi ya moja na wanaendelea kuhubiri zaidi!!
- Ukristo wa kweli huko katika vita na serikali, umma na madhehebu.
- Ukamilifu wa kanisa (II Wathesalonike 2:6-7)
- Kanisa la kweli ni lazima kwanza liondolewe duniani.
- Roho ya mpinga Kristo tayari himo duniani na kanisani.
- Azuiaye uasi ni (1)Roho mtakatifu na (2) Kanisa la kweli.
- Roho mtakatifu yuko kazini ya kuzuia (Yohana 16:8-11)
- Kanisa la kweli linazuia maana ya chumvi na nuru (Mathayo 5:13-14)
- Kanisa la kweli lazima kwa kuondolewa duniani ili mpinga Kristo apate nguvu zote (Rapture, Yeremia 30:7, Dan 9:27, Ufunuo 6:16-17, 3:10)
II. UWEZO WA MPINGA KRISTO (8:23)
- Atakuwa mtu wa kupendwa– popular (ufunuo 6:2)
- Yeye alipewa taji ya ushindi mwingi sana.
- Watu wa ulimwengu wote watapenda.
- Mpinga Kristo ataleta Amani duniani.
- Mpinga Kristo ataleta uchumi bora.
- Dunia yote iko tayari kwa mpinga Kristo, maana tunahitaji Amani, uchumi bora, bidhaa, uhuru na ustawi sasa.
- Atakuwa mtu wa Amani (Ufunuo 6:2)
- Yeye atapanda farasi mweupe, atakuwa na uta bila mishale !!
- Yeye atafanya agano la Amani na Israeli miaka saba (Danieli 9:27)
- Dunia hiko tayari kupata Amani, uchumi na ufanisi, maendeleo na salama– Mpinga Kristo ataahidi haya yote– lakini– Amani ni Kristo (Yohana 14:27)
- Atakuwa Mtu wa Ustawi- (Propserity) Danieli 11:43, Ufunuo 13:16-17)
- Mpinga Kristo ataleta utajiri duniani, walio masikini watakuwa matajiri !!(Mambo yatabandilika)
- Mpinga Kristo atamaliza njaa na kumaliza viwango katikati ya watu (Class societies will end!!)
- Watu wanapenda kustawi kiuchumi. Watu wanapenda kustawi (Bill Clinton, Obama, Trump, Kibaki etc)
- Atakuwa mtu wa nguvu (Power) Ufunuo 13:7-8
- Nguvu zake zitatoka kwa shetani (8:24)
- Atakuwa mkuu sana mbele za watu duniani kiasi, wote watamuabudu yeye kama mungu.
III. HILA YA MPINGA KRISTO (ABOMINATIONS) 8:24-25)
JJJ. Atafanikisha hila mkononi mwake.
- Ataangamiza watu wa Mungu (Dan.7:25)
- Atafanyika kama jini Hitler na Stalin, yeye atafaulu.
- Leo dunia inataka kanisa kuvumilia (tolerate) wasoga, malualua, abortion etc.
- Atashidana na aliye mkuu wa wakuu yaani Kristo (8:25)
- Atapinga sana utakatifu, uungu na Kristo.
- Mungu naye atawainua wahubiri wayaudi 144,000 kuhubiri dunia yote (Rev.14)
- Atachafua mahali pa ibada (8:25;11:36-37)
IV. MWISHO WA MPINGA KRISTO (DAN.8:25)
- Atavunjika bila kazi ya mikono. (Ufu.19:20) haraka sana.
- Ataingizwa katika ziwa la moto hai (Ufu.19:20)
- Baada ya miaka 1000– hukumu ya milele na milele (Final state of satan)
MWISHO
- Dunia hii itapitia shida nyingi sana!
- Inatengemea kile utafanya na Mtu Yesu Kristo!
- Mbingu zipo na pia jianamu ipo. Wewe upo upande gani?
- Danieli aliugua siku kadha alipoona hayo– nawe utafanyaje?
The following two tabs change content below. Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.