MFULULIZO: KURUDI KWA YESU KRISTO
SOMO: DANIEL 8:1-27 (23-27)
Jumapili iliyopita tulianza mafundisho juu ya kurudi kwa Yesu Kristo duniani. Tulitazama hasa juu ya kunyakuliwa kwa kanisa na kufufuliwa kwa wote walio lala mauti katika Yesu Kristo. Leo tunatazama ukweli juu ya mtu aitwaye mpinga Kristo.
Kwa kweli Biblia ni kitabu ajabu sana. Ajabu yake inaonekana katika unabii wake. Karibu kila mwalimu wa unabii anao tafsiri yake binafsi juu ya unabii-matokeo ni kuchanganyikiwa na kupoteza watu wengi zaidi.
Mimi nitajaribu sana kueleza Biblia isemavyo. Tulianza na somo juu ya kunyakuliwa kwa kanisa hewani (mbinguni). Leo tunatazama juu ya mtu aitwaye mpinga Kristo (the anti-Christ) maisha na kazi yake.
Wengi wa Wakristo kanisani hawaelewi na yale yajayo duniani hivi punde. Lakini wakati uliobaki ni mfupi zaidi tunahitaji kufahamu kweli.
Watu zaidi ya bilioni 45 wameishi duniani tangu Adamu na Hawa mle Edeni. Dunia imeshuhudia watu mashuhuri-elimu, akili, nguvu na wenye vipawa vya kutisha sana, lakini kwa wote walio hodari hakuna mwenye kutisaha zaidi kuliko mpinga Kristo.
Mpinga Kristo (anti-Christ) atakuwa mwenye nguvu, mdanganyifu zaidi, akili kupata kiasi, katili, m’baya na mwenye kutekeleza mipango yake.
Mpinga Kristo atakuwa mambo yote ambayo mwanadamu anaweza kufanya bila Mungu. Mpinga Kristo atakuwa shetani mwenyewe lakini katika mwili. Hebu tuone Biblia inasema nini juu ya mpinga Kristo (anti-Christ).
KUTOKELEZEA KWA MPINGA KRISTO.
- Biblia inatueleza katika siku za mwisho mfalme hodari na hatari atasimama juu ya dunia.
- Lakini ni nini ishara za kutokea kwake?
- Je, wanadamu wanaweza kufahamu hasa kutokea kwake?
- Jibu ni ndio na la. Ndio tumepewa ishara zake, La-hakuna nayejua kutokea kwake ni mwaka gani.
- Ishara za mpinga Kristo ndizo hizi:-
Hali ya ulimwengu.
- Dunia itakuwa katika hali ya dhambi nyingi, LGBTQ, mauaji, kukosa sheria-Luka 17:26-27; 2 Timotheo 3:1-5.
- Ulimwengu uko tayari kwa mpinga Kristo, kutokea.
Ufisadi wa kanisa na dini-2 Wathesalonike 2:3.
- Mpinga Kristo atatokea wakati wa upotovu wa dini na Ukristo (apostasy).
- Wengi wakristo wataacha imani (“a falling away”).
- Dini au kanisa litapotea njia na kufuata mafundisho ya uongo-cults.
- Dini, madhehebu, makanisa yataacha mafundisho ya kweli na kufuata filisofia na mapokeo ya watu.
- Mafundisho ya kweli yatakoma, watu watafundishwa wanayopenda.
- Mafundisho ya Biblia ya msingi hayatafuatwa, jama jinsi:-
- Kristo alizaliwa na bikra.
- Kristo alikufa mahali petu.
- Kristo alikufa, akazikwa, akafufuka kwa wafu.
- Kristo yuarudi tena (mwili, utukufu na kwa nguvu).
- Biblia ni neno la Mungu, haina makosa, ni takatifu.
- Kuokoka ni kwa neema, kwa njia ya imani.
- Dini za uongo zinakua kwa haraka zaidi, kanisa la kweli liko katika shida na serikali, umah na dini.
- Wabatisti wamegawanyika mara nyingi juu ya mafundisho ya Biblia.
- Karibu kila dhehebu sasa wamekubali ushoga. Mashoga sasa wanatawazwa makanisani-Warumi 1:18-31.
Basi kwa nini mpinga Kristo asidhihirishwe mara hii?
- Kwa sababu kanisa bado kudhihirishwa na kukamilika-2 Wathesalonike 2:6-7.
- 6-kuna kitu “kinachozuia.”
- 7-“yuko azuiaye.”
- Roho ya mpinga Kristo tayari iko duniani-lakini “kanisa” na “Roho Mtakatifu” ndio nguvu mbili zinazo zuia-Yohana 16:8-11.
- Lakini kanisa litakapo nyakuliwa, Roho Mtakatifu pia atatoka duniani.
- Mpinga Kristo atapata fursa ya kufanya kazi yake tunaponyakuliwa.
- Dhiki kuu si kwa kanisa, lakini ni wakati wa shida kwa taifa ya Israeli-Yeremia 30:7; Danieli 9:27.
- Dhiki kuu ni ghadhabu ya Mungu juu ya ulimwengu-Ufunuo 6:16-17; 16:1.
- Watoto wa Mungu tayari wamepona dhiki kuu-Warumi 5:9; Ufunuo 3:10.
- Kanisa la kweli waliookoka) lazima kuamishwa dunia hii mbele ya dhiki kuu.
NGUVU NA UWEZO WA MPINGA KRISTO-Danieli 23.
Mpinga Kristo (anti-Christ) atakuwa mtu wa kupendwa sana, mtu wa sifa, mtu wa kuvutia watu wote-Ufufnuo 6:2.
- Mpinga Kristo “atapewa taji”-watu wa ulimwengu watampa roho zao zote.
- Mpinga Kristo ataahidi dunia yote “amani”
- Minga Kristo atakuwa na jibu ya kueleza ulimwengu wote juu ya kunyakuliwa (rapture).
- Mpinga Kristo atakuwa na tabia zote ambazo watu wanatafuta kwa kiongozi mwema na mkamilifu.
- Mpinga Kristo atakuwa kama-
- Rais Washington au Abraham Lincoln.
- Atakuwa na usemi ajabu kama Franklin Roosevelt, Obama au Ruto.
- Atakuwa na ulimi tamu kama Theodore Roosevelt.
- Atakuwa na karama (charisma) kama J.F. Kennedy.
- Atapendwa sana kama Rais Dwight Eisenhower.
- Atakuwa na siasa tamu kama Lyndon Johnson au Julius Nyerere.
- Atakuwa na akili nyingi kama Rais Thomas Jefferson, mfalme Suleiman.
- Dunia yote inangoja mtu, mpinga Kristo (popular).
Mpinga Kristo atakuwa mtu wa amani (man of peace)-Ufunuo 6:2.
-
- Atapanda farasi mweupe-amani.
- Atakuwa na uta bila mishale!!
- Atakuja kuleta amani si vita.
- Atakuja na mkataba wa amani ya miaka saba (7) na Israeli-Danieli 9:27.
- Dunia hii imechoka vita.
- Uchumi wa ulimwengu umezorota. Mpinga Kristo ataleta suluhisho ya uchumi m’baya!!
- Watu sasa wanataka amani, uchumi bora, pesa mfukoni, ustawi, raha na usalama.
- Dunia iko tayari kumpokea mtu yeyote atakaye leta aukuahidi amani, nyumbani, kanisani na nchi. Lakini dunia hii haitajua amani bila Yesu Krisro, mfalme wa amani-Yohana 14:27
- Ikiwa wewe watafuta amani, basi ni kwa Yesu Kristo pekee.
Mpinga Kristo atakuwa mtu wa ustawi na maendeleo (prosperity)-Danieli 11:43; Ufunuo 13:16-17.
- Mpinga Kristo atawala na kuleta utajiri duniani.
- Mpinga Kristo ataleta utajiri kwa wale wameishi katika umaskini.
- Mpinga Kristo atakuja kumaliza njaa duniani.
- Mpinga Kristo atakuja kumaliza viwango vya watu (class-society-upper, middle, lower).
- Maskini watastawi chini ya mpinga keristo, matajiri watakuwa tajiri zaidi.
- Watu wanapenda kustawi!! Kiongozi anayeahidi ustawi atafuatwa!!
Mpinga Kristo atakuwa mtu wa nguvu-Ufunuo 13:7-8.
- Ahadi za mpinga Kristo zitatimizika, (hustler) atastawi-Danieli 8:24.
- Mpinga Kristo ataabudiwa kama jinsi Mungu.
- Lakini baada ya miaka tatu na nusu, atabadilika na kuwa shetani-hivyo dhiki kuu itaanza.
- CHUKIZO ZA MPINGA KRISTO-Danieli 8:24-25.
Atavamia watu wa Mungu-Danieli 7:25.
- Mpinga Kristo atavunja mkataba wake na Israeli.
- Mpinga Kristo atakuwa mbaya zaidi kuliko Hitler na Stalin, atapenda sana kuwa maliza Wayahudi wote duniani.
- Hata saa hii, tazama Israeli katika vita vyake na Palestine!!
Mpinga Kristo atavamia Yesu Kristo-Prince of peace-Danieli 8:25.
- Mungu atawainua wahubiri Wayahudi 144,000 watahubiri duniani kote.
- Mpinga Kristo hataweza kuwazuia kuhubiri-Ufunuo 14.
Mpinga Kristo atavamia mahali patakatifu pa Mungu-Danieli 8:25; 11:36-37; 9:25.
- Mpinga Kristo atafanya kama jinsi Antiochus Epiphenes, alifanya (175BC-164BC), alichukia Wayahudi zaidi-Mathayo 24:15.
MATESO YA MPINGA KRISTO-Danieli 8:25.
Hukumu juu yake itafanyika upesi, bila nguvu za mwanadamu.
Hukumu juu ya mpinga Kristo zitakuwa kali zaidi-Ufunuo 19:20
MWISHO
- Yesu Kristo yuaja upesi, lakini dunia hii lazima kupitia dhiki kuu zaidi.
- Kitakacho fanyika juu yako, kinategemea utakachofanya na Yesu Kristo.
- Ikiwa umeokoka-tangaza Injili kwa wote.
- Ikiwa haujaokoka dawa ni kuokoka leo.
- Je, utakuwa wapi ajapo mpinga Kristo na dhiki kuu kuanza?
The following two tabs change content below. Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.