Categories: Swahili Service

UMETAKASWA KUPOKEA KIBALI.

MFULULIZO: AGANO LA UTAKASO.

SOMO: ESTA 2:15-18.

 

Kibali cha Mungu ndicho kinacho watenga watoto wake kupokea baraka, kupenya na heshima.

Zaburi 5:12, “Kwa maana wewe utam’bariki mwenye haki; Bwana utamzungushia radhi kama ngao.”

Radhi ni kibali, hivyo kibali ni baraka za Mungu kwa watoto wake kila siku.

  • Kibali ndio mali na urithi ulio mkuu zaidi katika maisha ya waliokoka.
  • Kibali si kitu tunaweza kununua au kupata kupitia mbinu za mwanadamu.
  • Kibali kinatoka kwa Mungu. Kibali kinapoangukia mtu, milango inafunguliwa, itikadi zote zinavunjwa na hatima ya mtu inakamilika upesi.
  • Kibali cha Mungu Maanake ni kwamba Mungu anataka upate baraka ambazo wengi hawawezi kueleza.
  • Mahali watu wengi wanajaribu sana, kibali cha Mungu kinakuweka mahali unapokea mapokeo mema hata pasipo kuitimu, pasipo ujuzi haijalishi ulipotoka na maisha ya kale.
  • Kibali cha Mungu kilimteua Yusufu kule Misri, Esta kule Uajemi na Danieli kule Babeli.
  • Kama watoto wa Mungu hatujaitwa kuishi kwa kazi pekee, lakini kwa kibali cha Mungu.
  • Kibali cha Mungu kitakupeleka mbali bila elimu na juhudi nyingi.
  • Kibali cha Mungu kitakuleta karibu mbele za Wafalme.
  • Kibali cha Mungu kitakutoa kwa aibu na kukuweka katika utukufu.
  • Katika ujumbe wa leo, tutaona jinsi Mungu anawapa watu baraka. Tutaona jinsi Mungu anawaweka watu wake mahali pa kibali kila mara.
  • Hebu tutazame:-

KIBALI NI KIPAWA KUTOKA KWA MUNGU.

  • Kibali hakiwezi kufanyiwa kazi, kalini kibali kinapeanwa na Mungu kupitia neema na rehema zake.
  • Kibali ni kazi ya mapenzi ya Mungu na ahadi za Agano lake na watu wake.
  1. Kibali ni uchaguzi wa Mungu-Warumi 9:15.
  • Mungu anawaonyesha watu wake rehema na kibali kulingana na mapenzi yake.
  • Kibali cha Mungu hakiwezi kueleweka na wanadamu.
  1. Kibali kinakutenga na umati wa watu.
  • Nuhu alipata kibali na neema kwa Mungu, hivyo Nuhu hakuangamia na watu wa kizazi chake-Mwanzo 6:8.
  1. Kibali ni ngao ya ulinzi-Zaburi 5:12.
  • Mungu anawazingira watu wake na kibali huku akiwatenga na uaribifu na aibu.
  1. Kibali kinaleta baraka zaidi ya kazi-Mhubiri 9:11.
  • Wakati na bahati (kibali) zinafanyika kwa wote, kinawainua wengine juu ya dhiki zao.
  • Yusufu alipewa kibali katika nyumba ya Potifa mpaka kupandishwa kuwa waziri mkuu Misri-Mwanzo 39:21.

KIBALI KINAMPANDISHA MTU CHEO.

  1. Kibali kinamfanya na kumtenga mtu na kumpandisha cheo. Hata wakati hauna matumaini na pia wakati hauna ujuzi wakutosha-Mithali 22:29.
  • Ujuzi ni mzuri lakini kibali kinakupandisha na kukuweka mbele ya Wafalme na wenye nguvu.
  1. Kibali kinavunja itikadi zote—Esta 2:17.
  • Esta alikuwa mgeni lakini akapata kuwa malkia kwa kibali. Vikwazo vyote viliondolewa na kile kibali cha Mungu.
  1. Kibali kinakufanya utambulike na watu.
  • Danieli alipata kutambulika na mfalme na kupendwa na wakuu wa Babeli mpaka hatima yake ikatimia-Danieli 1:9.
  1. Kibali kina harakisha sana hatima ya watu-1 Samweli 16:22.
  • Daudi alipendwa na mfalme Sauli kwa sababu ya kibali.
  • Esta naye alipata kuwa malkia si kwa sababu ya urembo pekee lakini kibali cha Mungu kilimteua na kumleta mbele ya mfalme.

KIBALI KINALETA MAGEUZI YA MUNGU.

  • Kibali cha Mungu kinapokuwa juu yako Mungu anabadilisha historia yako na kuondoa Kumbukumbu ya mabaya yote uliyopata hawali.
  1. Kibali kinageuza kilio kuwa furaha-Zaburi 30:5, “Kilio huja kukaa usiku, lakini asubuhi huwa furaha.”
  2. Kibali urejesha miaka iliyopotea-Yoeli 2:25-26.
    • Kibali cha Mungu urejesha kilicho ibiwa, kilicho potea na kilicho haribika.
    • Kibali kinajaza mtu na uzima na mali tele tele.
  3. Kibali kinanyamazisha adui wote na upinzani-Kutoka 12:36.
  • Wana wa Israeli walitoka Misri na mali nyingi, Mungu aliwapa Wamisri hisani kuu, kuwapendelea Waisraeli.
  1. Kibali kinavunja vizuizi na kudhibitiwa-Luka 1:30.
  • Vidhibiti vilivyokuwa mbele ya Mariamu viliondolewa na kile kibali cha Mungu alichopokea.
  • Ruthu mzaliwa wa Moabu alipata kibali Israeli mbele ya macho ya Boazi-Ruthu 2:10.
  • Mungu alim’bariki Ruthu kutoka ujane na kuingia katika jamii na vizazi vya Mwokozi Yesu Kristo.

JINSI YA KUJIWEKA KATIKA PAHALI PA KUPOKEA KIBALI CHA MUNGU.

  • Hata ingawa kibali ni kipawa kutoka kwa Mungu ni lazima kujiweka katika mahali pa kupokea kibali cha Mungu kupitia imani, utii na uaminifu.
  1. Ishi katika haki-Zaburi 84:11.
  2. Uwe mwaminifu kwa mambo madogo, uaminifu utavuta kibali cha Mungu-Luka 16:10.
  3. Tembea katika utii siku zote-Kumbu Kumbu 28:1.
  4. Uwe mtu wa maombi na matarajio-Zaburi 102:1-4.
    • Kornelio kwa maombi, utii na kutoa sadaka na zaka kulivuta kibali cha Mungu kwa maisha yake na jamii yake-Matendo 10:1-4.

MWISHO

  • Kutengwa na kupokea utakaso ni pamoja na utii, uaminifu na imani.
  • Kibali cha Mungu ndicho kinaleta kutambulikana, kukumbukwa, kupandishwa cheo na maisha ya kupenya.
  • Kibali cha Mungu kinaputa kazi, ujuzi, kujulikana na kipawa na elimu.
  • Hivyo, tafuta sana kibali cha Mungu usitegemee kazi, watu, ujuzi na elimu pekee.
  • Mungu anapokutakasa anakutenga kupokea kibali chake. Hakuna mwanadamu, “system” au shetani anaye weza kupinga kuinuliwa kwako.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Rev, DR. Willy Mutiso

Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Share
Published by
Rev, DR. Willy Mutiso

Recent Posts

THE GOD WHO SHIFTS THE HEAVENS IN YOUR FAVOR.

SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: HAGGAI 2:6-9.   God has the power to…

3 days ago

SINGING PSALMS, HYMNS AND SPIRITUAL SONGS.

SERIES: THROUGH THE BOOK OF COLOSSIANS. TEXT: COLOSSIANS 3:16   Christianity is a singing religion.…

3 days ago

GOD DEFENDS HIS CHILDREN.

SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: ISAIAH 54:17   JEHOVAH God does not abandon…

1 week ago

CHRISTIAN LIFE IS LIKE EAGLE’S LIFE

SERIES: THEY THAT WAIT HAVE EAGLE'S ANOINTING  TEXT: ISAIAH 40:31   The eagle symbolizes the…

4 weeks ago

MSAADA WA MUNGU WAKATI WA MATESO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: ZABURI 46:1.   Biblia inatuakikishia kwamba Mungu wetu ni “Msaada…

1 month ago

GOD GUIDES OUR DESTINIES.

SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: PROVERBS 3:5-6.   Every destiny is a divine…

1 month ago