MFULILIZO: URITHI USIOHARIBIKA MILELE
SOMO: I PETER 1:1-5
Je,Nanga ya kushika wakati wa majaribio na mateso katika maisha yetu ni nini?Je imani yako ikoje wakati maisha yamekuwa magumu sana? Leo twajifunza kifunguo cha kustahimili wakati wa shida. Kumbuka uridhi wetu katika Yesu Kristo ni wa milele.
Petro aliandika kwa kanisa lililokuwa katika mateso, kuchukiwa na kukataliwa. Tarehe 19 Julai 64 A.D. Mji wa Roma uliwaka moto mkuu sana. Baada ya siku tatu moto huo ulimaliza Roma yote! Watu wa Roma waliamini kwamba mfalme, hau Kaisari Nero ,niyeye aliwakisha moto huo. Niro alipendezwa sana na moto huo kiasi alicheza kinanda chake moto ulipoendelea!!.
Lakini Kaisari Niro alifitini kwamba ni wakristo waliwakisha Roma moto huo!!.Wakristo walichukiwa kwa sababu wengi walikuwa wayahudi,na kwa sababu wakristo walikataa kuabudu mfalme Niro yaani (Emperor Worship). Pia kwa sababu walitangaza kwamba siku moja dunia itawaka moto, Niro alifitini.
Hivyo mateso na dhihaka, juu ya wakristo ilianza Roma, hivyo wakristo wengi wakachomwa moto, lakini wengine walikimbia mbali na kutawanyika katika mataifa ya Asia.
Mtume Petro anawaandikia kuwafariji huku akiwakumbusha wao ni wageni duniani, Nyumbani kwao ni Mbinguni, wao ni watoto wa Mungu na pia wao ni mawe hai, taifa takatifu na makuhani watakatifu, mali ya Mungu aliye hai. Petro anawajulisha kwamba wakamsifu Mungu katika majaribu yao.(1petro 1:3-5). Neno la katikati katika waraka huu ni URIDHI. Uridhi ni kile unachopokea kutoka kwa baba kama zawadi hau dhawabu kwa sababu wewe ni mzaliwa katika nyumba ya Baba.
Hebu na tuone:
I. JE,URIDHI WETU KATIKA BWANA NI NINI?
II. KIINI CHA URIDHI WETU. (1 PETRO 1:3)
III. JE, TUNATEKELEZA URITHI HUU WA MILELE AJE?
IV. JE, KITU GANI KIMETUPATIA TUMAINI LA MILELE? (I PETRO 1:3)
MWISHO
MFULULIZO: AGANO LA UTAKASO. SOMO: KUTOKA 12:12-13. Damu ya Yesu Kristo ndiyo mhuri wa…
SERIES: SUPERNATURAL ADVANCEMENT. TEXT: HABAKKUK 3:19. The journey of fulfilling your destiny does not…
SERIES: THROUGH THE BOOK OF COLOSSIANS. TEXT: COLOSSIANS 3:15 Thankfulness is a great attitude…
SERIES: THE ANOINTING. TEXT: EZEKIEL 47:1-5 There are levels of the anointing and each…
MFULULIZO: AGANO LA UTAKASO. SOMO: ESTA 2:15-18. Kibali cha Mungu ndicho kinacho watenga watoto…
SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: HAGGAI 2:6-9. God has the power to…