MFULULIZO: DANIELI-MUNGU NDIYE HAKIMU
SOMO: DANIELI 2:36-49; MATHAYO 13:25.
Kabla ya kuendelea na somo letu katika kitabu cha Danieli, nimeona vyema kufundisha juu ya ndoto na tafsiri zake. Hii ni kwa sababu kitabu cha Danieli ni kitabu cha unabii na unabii unaenda sambamba na ndoto na maono (dreams, visions and interpretations). Tunajifunza ndoto nzuri na ndoto mbaya.
Katika Mathayo 13:25, “Lakini watu walipolala, akaja adui yake akapanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake.”
Kwa nini adui anafanya kazi yake usiku watu wanapolala? Sababu yake ni watu wanapolala hawawezi kujilinda. Ndivyo shetani anafanya kazi yake zaidi usiku.
Kila wakati shetani yuko katika kazi ya kupanda magugu. Shetani anatumia miili ya watu kama shamba ya kupanda mbegu za kila haina. Wengine hapa miili yao imejaa chuma, plastiki, misumari.
Shetani anapopanda magugu hangojei kunyunyuzia maji anaenda zake. Lakini magugu yake yanamea mara moja-Ayubu 33:13-18.
Lakini unapolala, masikio yako yanaweza kufunguliwa kupokea maarifa kutoka mbinguni. Usidharau ndoto zako. Ndoto yako inaweza kuongoza na kukuondolea mitego ya adui. Elewa yafuatayo juu ya ndoto:-
- Nchi ya ndoto ni muhimu sana kama jinsi nchi ya asili.
- Ndoto ni njia moja ya mawasiliano na jinsi ndoto zako ndivyo maisha yako pia.
- Wewe ni mazao ya ndoto zako.
- Ni jambo hatari sana kudharau ndoto zako, kwa maana ndoto ni monitor kuonyesha yanayoendelea katika maisha yako.
- Ndoto zako haziwezi kukudanganya kamwe pengine ukose tafsiri yake lakini ndoto si danganyifu.
- Ndoto zako zinaweza kukuonyesha maisha yako ya kale na msiaha yajayo.
- Ndoto yako inaweza kukufichulia adui zako na mikutano yao juu yako.
- Kila ndoto inao ujumbe wake, hata ingawa unaweza kukosa kuolewa maana yake.
- Hii ndio inafanya shetani kupendezwa sana na ndoto zetu.
- Shetani anatumia sana ndoto za mgonjwa.
- Mungu anatumia ndoto na maono kuwaonya watu wake. Shetani anajua kuingilia ndoto yako. Kila ndoto hata ile imechanganyikiwa inao maana yake.
- Kuna watu hawaoti ndoto, na waombe sana kukomboa ndoto zao. Hebu tuone:-
HAINA KADHA ZA WAOTAJI.
- Kuna waotaji ndoto zao zinafutwa. Hawa hawakumbuki walichoota kama jinsi Nebukadreza.
- Kuna waotaji wanaoota ndoto za upuzi, ndoto zao hazina maana yoyote.
- Kuna waotaji fukara. Leo wanaota wakiwa Nairobi, Kampala, London, shambani, milimani, baharini.
- Kuna waotaji wanaoota mambo ya uchawi, mashetani. Hawa katika ndoto wanakutana na watu wasiofahamu, (occultic dreamers).
- Waotaji waotaji, (dream dreamers). Wanaota ndani ya ndoto zao. Shetani anawachanganya.
- Waotaji wanao sumbuka (troubled dreamers).
- Hawa wanasumbuliwa katika ndoto zao.
- Waotaji kinyume (reverse dreamers).
- Hawa wanaota kinyume. Ikiwa wanaota mtu akiwapa pesa, Maanake ni wanaibiwa pesa.
- Waotaji balaa (nightmares) ndoto za vita na mauaji.
- Waotaji nabii-omba uwe muotaji nabii.
- Waotaji waliotekwa nyara (manipulated) hawa wanawaona adui kama rafiki na rafiki ndiye adui.
- Waotaji wa kunyanyaswa (oppression) muotaji anaota akinyanyaswa kila wakati.
- Waotaji wachawi-kila wakati wanajiona katika mikutano na watu wasiojulikana.
- Waotaji wanaota wakikimbia (night sleep walkers).
- Waotaji wakudumu (permanent dreamers). Wanaota wakati wote-wawe macho, wawe wamelala.
- Waotaji wa kila saa-mchana (Day dreamers).
- Waotaji wa mwezi-kila mwezi unapong’ara.
- Waotaji wanaotembea katika mwili, ndoto zao ni za kimwili.
- Waotaji wanaotembea katika Roho Mtakatifu ndoto zao ni za kiroho.
- Kulingana na rafiki zako unaota.
- Kama unaishi katika laana ndoto zako zinatekeleza ile Agano la laana.
- Kulingana na adui zako, ndoto zako zitakuwa kama adui yako ni Farao-utakimbizwa.
- Kulingana na mazingira yako utaota kuna nyumba zamelaaniwa, ndoto zako zitakamatwa na roho na pepo anayeishi katika zile nyumba.
- Mila na desturi za mtu zitachangia ndoto zako.
- Kufanya ngono na watu wa shetani na waabudu shetani, marafiki wa kitambo pia.
NDOTO MBAYA ZISIZO ZA KUCHEZEA.
- Ngono katika ndoto, zaidi ni pepo chafu.
- Kula chakula katika ndoto-chakula katika ndoto kitakuletea ndoto.
- Kupigwa risasi katika ndoto, maanaye ni kuna wauaji katika maisha yako, washinde.
- Kuvamiwa na wanyama-ndoto hii inaleta kifo.
- Kupoteza Biblia yako katika ndoto ni ishara ya kurudi nyuma.
- Kuota ukiona maiti, geneza, watu waliokufa kukutokea, mtu wako wa roho ametekwa nyara-unaishi na kuhesabiwa na wafu.
- Pigana sana-maana hakuna uhusiano katika wafu na walio hai.
- Ukiota kama umerudi shule yako ya zamani na kuvaa uniform tena, ni roho ya umasikini na utumwa (retrogression).
- Kuota ukienda na nyayo bila viatu ni ndoto ya kurudi umasikini sugu hau shetani anaenda kuharibu ndoa yako.
- Kutembea, kuendesha gari hau kupanda bila kufika mwisho Maanake ni kufanyishwa kazi bila faida.
- Ukiota umevaa nguo zote nyeusi, shetani amekuvamia na mauti.
- Ukiota uko uchi mbele ya watu, bila nguo-maanake ni utapata aibu kubwa.
- Ukiota umevaa nguo zimechakaa na kuraruka ni ishara ya umasikini sugu.
- Ukiota unatangatanga sokoni pekee yako ni ishara ya kichaa.
- Ukiota umenyolewa hau nywele zimemwagika-heshima yako itakwisha.
- Ukiota unanyolewa bahari hau mto bila kutoka-pepo wa (marine) maji imechukua roho yako.
JINSI YA KUJILINDA.
- Dai uwepo wa damu ya Yesu Kristo juu ya maisha yako.
- Vunja laana na kurudisha laana kwa wenye kutuma.
- Anguka katika mikono ya Yesu Kristo, pata ulinzi wako.
- Ng’oa kutoka maisha yako chochote ambacho Mungu hakupanda ndani yako.
- Omba Mungu akupatie tafsiri ya ndoto zako.
MWISHO-OMBA
- Kila mbegu ya giza, imepandwa katika maisha yangu toweka, katika Jina la Yesu Kristo.
- Kila ndoto ya shetani niliyeota kitambo na sasa inachangia katika maisha yangu vunjika katika Jina la Yesu Kristo.
- Kila mshale wa mauti, unaotekelezwa kwangu shindwa katika Jina la Yesu Kristo.
- Kila ndoto kutoka kwa shetani na uchawi wote shindwa katika Jina la Yesu Kristo.
- Kila ndoto iliyo kinyume na hatima yangu toweka sasa katika Jina la Yesu Kristo.
The following two tabs change content below. Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.
View Comments
This is very insightful and helpful for every believer.God bless you and expand your territory in Jesus name.