Categories: Swahili Service

USIPOTEZE WIMBO WAKO

MFULULIZO: MAFANIKIO

SOMO: WAFILIPI 4:4-7

 

Watu wengi furaha yao inategemea vitu na mali walio nayo.  Inaonekana kama jinsi mtu alivyo na vitu vingi ndivyo anataka nyingi zaidi. Mtu anavyokuwa na nyingi ndiyo furaha yake inapungua. Lakini kuna watu walio na vitu vichache sana lakini furaha yao ni zaidi kwa nini? Kwa sababu furaha haitegemei vitu na mali. Furaha ni kuridhika, furaha ya ndani isiyotoka kwa vitu, watu na hali.

Mfalme Daudi alisema Zaburi 51:10- “Ee Mungu, uniumbie moyo safi, uifanye upya roho iliyotulia ndani yangu.”

Zaburi 51:12- “Unirudishie furaha ya wokovu wako, unitengeneze kwa roho ya wepesi.”

Mtume Petro katika 1st Petro 1:8 “Naye mwampenda ijapokua hamkumwona, ambaye ijapokuwa hamwoni sasa, mnamwamini na kufurahia sana kwa furaha isiyo neneka yenye utukufu.

Furaha tunayoipata wakati tumeokoka ni furaha isiyo neneka. Hii ni furaha dunia haiwezi kuelewa. Furaha hii inaptikana na waliokoka pekee. Hivyo hatua ya kwanza kuwa na furaha hii, amani na uzima ni kupokea Yesu Kristo katika mioyo yetu. Yesu Kristo ndiye kiini cha furaha isiyiyoneneka. Hivyo Mungu ametupa furaha isiyo neneka lakini shetani ni mwizi wa furaha. Shetani hapendi wakristo wawe na furaha hivyo shetani atayaleta mambo ya kila aina pamoja na kutukumbusha ya kale-Yohana 10:10. Hebu tuone.

WEZI WA FURAHA.

  1. Stress (kusongwa).
  • Kulingana ma masomo ya afya, kusongwa na mambo, watu na hali ya maisha ndio namba moja kuleta kifo.
  • Kila mtu analo jambo linalo mletea mawazo na hali ya kusongwa.
  • Stress inafanya mtu kukasirika upesi na kukosa usingizi. Ni lazima kila mmoja wetu kujua jinsi ya kupambana na stress.
  • Tusipopambana na stress, stress inapambana nasi.
  • “Siku moja mtu aitweye Michael alishinda pesa nyingi katika RIDERS DIGEST. Alishinda dola milioni nne (4 million dollars). Kwa sababu Michael alikuwa mgonjwa sana ugonjwa wa moyo, mke wake alishindwa kumweleza. Basi akamwita pastor wake amweleze mmewe. Pastor alifika akamwambia “Michael ninataka ushauri wako leo. Kama ungeshinda dola milioni nne, je, ungefanya nini na pesa nyingi hivyo.” Michael alimwambia pastor “Hio ni jambo rahisi sana. Kama ningeshinda hizo pesa, ningekupa nusu ya pesa hizo (2 million dollars) kwa maana wewe ni pastor wangu ninaye mpenda sana.” Pastor aliposikia hayo alianguka chini na kufa.
  • Stress inaweza kuletwa na mazuri au mabaya.
  • Hivyo stress inakuja kwa sababu ya ndoa, kupata mtoto, shida za ndoa, kupandishwa cheo, kazi nyingi, kupoteza kazi.
  • Farao huko Misri aliwatesa wana wa Israeli, waliteseka kiasi kupoteza furaha yao.
  • Hivyo stress inaweza kuja kwa mazuri au mabaya.
  1. Watu
  • Mwizi mwingine wa furaha ni watu. Kila mmoja wetu amepata kukosa furaha kwa sababu ya watu.
  • Watu wanatuibia furaha yetu kwa yale wametutenda, wanayosema na kwa jinsi walivyo.
  • Pengine kuna mtu anakusema uongo, hukumu na hayo yanaiba furaha yetu.
  1. Mambo yaliyopita na yajayo.
  • Wakati mwingine tunasumbuka kwa mambo yaliyopita, yawe mazuri au mabaya-Isaya 43:18.
  • Wakati mwingine tunasumbuka kwa mambo yajayo-Mhubiri 7:14.
  • Usiwache ya kale na yajayo kuharibu maisha yako leo.
  1. Hali (circumstances)
  • Kila siku tunakutana na hali tofauti tofauti inayotuibia furaha yetu.
  • Suluhisho yetu ni Wafilipi 4:4-7.

JE, TUTAISHIJE KATIKA FURAHA.

  1. Kaa na kudumu katika uwepo wa Mungu.
  • Zaburi 16:11 “Utanijulisha njia ya uzima, mbele ya uso wako ziko furaha tele na katika mkono wako wa kuume mna mema ya milele.
  • Katika uwepo wa Mungu ndio furaha tele.
  • Furaha inapatikana kwa kufuata njia ya uzima.
  • Jinsi tulivyo karibu na Mungu ndivyo furaha yetu itazidi kuwa nyingi-Zaburi 43:4.
  • Hata wakati wa ukame na ugumu wa maisha na uchumi, furaha yetu ipo katika Bwana-Habakuki 3:17-18.
  1. Kwa uaminifu wote vumilia majaribu.
  • Watu wengi wanapoteza furaha yao katika majaribu-Ayubu 3:25-26.
  • Wakati unayo Taraji hayaji na ndoto zako kuzimia.
  • Wakati kupenya kwako kumechelewa-Zaburi 30:5.
  • Vumilia katika Bwana-Yakobo 1:2-4.
  1. Dumu katika utakatifu-Zaburi 32:11.
  • Dhambi ni mwizi mkuu wa furaha.
  • Haki, utakatifu na furaha zinaishi pamoja.
  • Mfalme Daudi kila wakati alipofanya dhambi, furaha yake ilimalizika-Zaburi 51:8-10.
  1. Usikose kuhudhuria ushirika kanisani-Zaburi 42:4.
  • Daudi alifurahia pamija na wale waliosema “Twende nyumbani mwa Bwana-Zaburi 122:1.
  • Bwana ametuahidi kuwa nguvu zake zitatulinda katika kila aina ya dhiki-Zaburi 94:13.
  • Vumilia dhiki, majaribu, furaha siku zote-Mhubiri 7:9; 2 Timotheo 4:5.

MWISHO

  • Kufanikiwa ni kufurahi katika Bwana.
  • Katika maisha kuna mengi yatakayo kuibia furaha na amani.
  • Furaha ya Bwana ndio nguvu yako-Nehemiah 8:10.
  • Je, umeokoka? Leo ni siku ya kuokoka.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Rev, DR. Willy Mutiso

Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Share
Published by
Rev, DR. Willy Mutiso

Recent Posts

DAMU YA UTAKASO.

MFULULIZO: AGANO LA UTAKASO. SOMO: KUTOKA 12:12-13.   Damu ya Yesu Kristo ndiyo mhuri wa…

11 hours ago

KEY TO DIVINE SPEED.

SERIES: SUPERNATURAL ADVANCEMENT. TEXT: HABAKKUK 3:19.   The journey of fulfilling your destiny does not…

13 hours ago

BE YE THANKFUL TO GOD.

SERIES: THROUGH THE BOOK OF COLOSSIANS. TEXT: COLOSSIANS 3:15   Thankfulness is a great attitude…

15 hours ago

LEVELS OF THE ANOINTING.

SERIES: THE ANOINTING. TEXT: EZEKIEL 47:1-5   There are levels of the anointing and each…

4 days ago

UMETAKASWA KUPOKEA KIBALI.

MFULULIZO: AGANO LA UTAKASO. SOMO: ESTA 2:15-18.   Kibali cha Mungu ndicho kinacho watenga watoto…

1 week ago

THE GOD WHO SHIFTS THE HEAVENS IN YOUR FAVOR.

SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: HAGGAI 2:6-9.   God has the power to…

1 week ago