Categories: Swahili Service

UTABIRI WA MWISHO KUTOKA KWA MUNGU

MFULULIZO: DANIELI-MUNGU NDIYE HAKIMU.

SOMO: DANIELI 12:1-13.

 

Leo hii tunatamatisha mfululizo wa jumbe katika kitabu cha Danieli. Danieli sura ya 12 ndio

mwisho wa unabii aliyepewa nabii Danieli. Kuna ukweli tano katika sura ya 12. Huu ni ukweli 

wa Mungu juu ya mwisho wa historia ya mwanadamu duniani. Hebu tutazame:-

UKWELI WA MUNGU: KUNA KITABU CHA UZIMA. JE, JINA LAKO LIKO KATIKA KITABU CHA UZIMA?-Danieli 12:1.

  • Tunajulishwa kwamba kuko na kitabu mbinguni. Kitabu hiki kimeandikwa majina ya watu fulani.
  • Mungu anatembea na watu kibinafsi. Maisha yako binafsi ni ya maana sana mbele za Mungu.
  • Pengine jila lako liko katika vitabu vingi sana hapa duniani, pengine kitabu cha shule, chuo, kanisa, vyama na pia benki na ma ‘society.’
  • Lakini orodha ya majina inao maana kwa mambo ya milele ni kitabu ambacho Mungu mwenyewe anaweka mbinguni-kitabu cha uzima, kitabu cha Mwana-kondoo.
  • Biblia inasema Mungu ameandika majina ya wanawe, waliochaguliwa tangu jadi katika Kristo kabla kuumbwa dunia hii-Waefeso 1:4.
  • Je, mtu anaweza kujua kwa kweli kama jina lake limeandikwa katika kitabu cha uzima?
  • Ndio. Maanake Yesu Kristo alisema, “Lakini, msifurahi kwa vile pepo wanavyowatii, bali furahini kwa sababu majina yenu yameandikwa mbinguni”-Luka 10:20.
  • Pia kuna hukumu kubwa kama jina lako halijaandikwa katika kile kitabu cha uzima.
  • Ufunuo 20:15, “Na iwapo mtu yeyote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.”
  • Wewe unahitaji kujali sana, “Je, jina langu liko katika kile kitabu?”
  • Tunahitaji kujua ukweli kwamba kitabu cha uzima si sawa na kitabu cha kanisa au dini.
  • Dini na madhehebu zina njia ya kuwapumbaza washiriki na kuwapa usalama wa mioyo yao kwamba ushiriki wa kanisa si sawa na kuokoka-Mathayo 7:21-23.

UKWELI WA MUNGU: KUNA UFUFUO WA WAFU HAINA MBILI. JE, WEWE UTAKUWA KATIKA UFUFUO GANI?-Danieli 12:2.

  • Ufufuo au kiyama ya wafu ni mbili. Je, wewe umepanga kiyama gani?
  • Yohana 5:28-29

“Msistaajabu maneno hayo; kwa maana saa yaja ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake. Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu.”

  • Kuna ufufuo wa uzima, na kuna ufufuo wa hukumu. Yesu Kristo alisema-

Ufunuo 20:6, “Huo ndio ufufuo wa kwanza, heri na Mtakatifu, ni yeye aliye na sehemu katika wa kwanza, juu yao mauti ya pili haina nguvu; bali watakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo, nao watatawala pamoja naye hiyo miaka elfu.”

  • Hakuna mmoja wetu ataishi katika mwili huu wa nyama milele.
  • Miili hii ni ya muda na miili hii inazeeka, inagonjeka na baadaye inakufa na kumalizika.
  • Tunakufa; hata ukila vizuri, kufanya mazoezi ya kukimbia, kutembea, kuruka, gym, bado utakufa.
  • Lakini kifo na mauti sio mwisho wa kuishi. Nafsi na roho zetu bado zinaendelea kuishi, baadaye hii miili itafufuliwa.
  • Biblia inasema wazi kwamba kuna kiyama ya wafu haina mbili-Ufufuo 20.
  • Walio na Yesu Kristo, waliokoka watafufuliwa waingie uzima wa milele, wataishi na Kristo milele na milele.
  • Waliomkataa, waliokataa wokovu watafufuliwa na kuingia hukumu-wataishi katika ziwa la moto milele na milele.
  • Watadharauliwa daima na milele. Hii ndio mauti ya pili, yaani kutengana na Mungu milele na milele-Yohana 3.
  • Ikiwa ulizaliwa mara moja utakufa mara mbili. Ikiwa umezaliwa mara mbili utakufa mara moja tu!!

UKWELI WA MUNGU: “NYOTA” WA KWELI NI WALE WANAANGAZIA YESU KRISTO-Danieli 12:3. JE, UNAWALETA WATU KWA KRISTO?

  • Leo hii “Nyota” ni watu walio maarufu kwa jambo fulani. Nyota wa sinema, urembo, wasanii, wanariadha.
  • Kuna “nyota” wa kila namna, lakini nyota wa kweli ndio wale wamhubiri Yesu Kristo wakiwa na shabaha ya waokolewe-Wafilipi 2:15-16.
  • “Nyota” za mbinguni zinang’ara usiku, gizani, sisi nasi tunag’ara gizani ya ulimwengu huu.
  • Nyota zinang’ara kwa uaminifu.
  • Nyota zinapeana mwongozo kwa wasafiri.
  • Tulio na Kristo tutang’ara kama nyota milele na milele.
  • Wenye hekima watang’ara kama mwangaza wa anga.

UKWELI WA MUNGU; MAARIFA YANAONGEZEKA SIKU ZA MWISHO-Danieli 12:4. JE, WEWE UNATIZAMA ISHARA?

  • Danieli anapewa agizo ya kufunga ule unabii mpaka nyakati za mwisho.
  • Danieli anaelezwa kwamba, wengi waenda mbio huku na huku, Maanake ni usafiri. Elimu itaongezeka, habari zitachipuka mara moja.
  • Maarifa katika kila eneo la maisha yataongezeka.
  • Isaac Newton, baba wa masomo ya Physic (fisiki) alikuwa Mkristo wa kuokoka. Aliposoma kwa elimu yake aliona maajabu ya Mungu. Aliposoma sura 12 ya Danieli alisema, “Hakika siku zinakuja watu wataenda kwa mwendo wa kasi kiasi cha maili 50 kwa saa (80km) (1,680).
  • Naye Harold Wilmington alimkashifu Newton na kusema Newton ameenda kichaa kwa sababu ya kuokoka.
  • Leo hii Space Shuttle inaenda speed ya maili 18,000 (28,000) kwa kila saa!! Ndege za abiria ziaenda mwendo wa kilomita 1,000 kwa saa moja!!
  • Leo kwa computa na simu ya mkono tunaweza kupata elimu ya vitabu bilioni!!-Mathayo 24:33.
  • Danieli aliambiwa na Mungu Danieli 12:9, “Enenda zako Danieli, maana maneno haya yamefungwa na kutiwa mhuri, hata wakati wa mwisho.”
  • Maanake ni Danieli aendelee kufanya kama zamani-Omba, tumika, abudu Mungu wako.
  • Mwisho huu tulio sasa, wengi watajitakasa dhambi-ufufuo utakuwa duniani. Lakini watenda dhambi na dhambi itaendelea kuongezeka duniani kote.
  • Baadaye Danieli anaeleza siku ya mpinga Kristo itakuja-Danieli 12:11-12.

UKWELI WA MUNGU: KUTAKUWA NA STAREHE NA DHAWABU KWA WATOTO WA MUNGU-Danieli 12:13. JE, MIMI NINA UHUSIANO WA KARIBU NA MUNGU?

  • Hatujui hasa siku na mwaka Danieli alikufa, lakini huenda ni miaka kadhaa baada ya unabii huu wa mwisho.
  • Lakini Danieli aliishi siku zake za mwisho akiwa na hakika kubwa kwa Mungu alimwahidi starehe na dhawabu kuu!!
  • Je, wewe umebaki na miaka mingapi kuishi? Uenda haujui jibu lakini Je, utaendelea kuishi maisha yako yaliosalia katika hakika ya kustarehe ndani ya Yesu Kristo na kungojea dhawabu yako na kutamani sana kuishi na Mwokozi Yesu Kristo milele na milele mbinguni?
  • Danieli alifurahi uhusiano a binafsi na Mungu wake. Danieli hakuwa mtu wa dini, bali uhusiano na ushirika wa karibu na Mungu wa mbinguni-Ufunuo 13:14.

MWISHO

  • Je, umeokoka? Je, unafahamu Yesu Kristo kibinafsi?
  • Je, unastarehe na kungojea dhawabu ya Mungu kwa kazi njema unaofanya kwa ajili ya Mwokozi wako?
  • Leo endelea kutumika na kutumika katika kazi ya Mungu.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Rev, DR. Willy Mutiso

Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Recent Posts

MSAADA WA MUNGU WAKATI WA MATESO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: ZABURI 46:1.   Biblia inatuakikishia kwamba Mungu wetu ni “Msaada…

2 weeks ago

GOD GUIDES OUR DESTINIES.

SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: PROVERBS 3:5-6.   Every destiny is a divine…

2 weeks ago

PUT OFF AND PUT ON

SERIES: THROUGH THE BOOK OF COLOSSIANS. TEXT: Colossians 3:5-10   We have put off the…

3 weeks ago

GOD OF THE BREAKTHROUGHS

SERIES: THE GOD WE SERVE TEXT: 2nd SAMUEL 5:17-20   Breakthroughs are divine interventions that…

4 weeks ago

WHO IS SPEAKING TO YOU?

SERIES: DRAWING NEAR TO GOD TEXT: LAMENTATIONS 3:37 It reminds believers that God's word alone…

1 month ago

CHECHEA MSHINDI ALIYE NDANI YAKO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: 1 YOHANA 5:4.   Wakristo wengi wanaishi maisha ya kushindwa…

1 month ago