Categories: Swahili Service

UTIMILIFU WA WAKATI

UJUMBE: UTIMILIFU WA WAKATI

SOMO: WAGALATIA 4:1-7

 

Kwa nini Mungu alichagua mwaka wa 4 A.D. Kwa nini si mapema zaidi? Ni kwa sababu “utimilifu wa wakati” ulifika. Hebu tuone jinsi Mungu alitimiza wakati kuja kwa Yesu Kristo:-

WAKATI ULITIMIA KITAMADUNI-Culturally.

  • Dunia yote ilikuwa katika hali ya maendeleo.
  • Mwaka wa 350BC mwana wa mfalme Philipo alizaliwa.
  • Aliitwa kwa jina Alexander-au “Alexander the great.”
  • Alexander alishinda vita vyote duniani na kumiliki dunia yote.
  • Mwaka wa 12 alikuwa ameleta mabadiliko mengi duniani, Europa, Afrika, na mashariki ya kati.
  • Tamaduni ya Uingereza, philosophia, elimu, usanii, michezo, vitabu, majengo na mawazo yalikuwa ya Kigiriki. Lugha pia ilikuwa Giriki.
  • Watu wote wangetembea popote maana lugha ilikuwa moja tu. Biashara iliendelea vizuri pote duniani.
  • Mwaka wa 280BC, Agano la kale ilitafsiriwa kwa Kigiriki-GKLXX.
  • Watu walikuwa wasomi hivyo mawazo yao yalibadilika kwa haraka sana.

WAKATI ULITIMIA KISIASA.

  • Baada ya Wagiriki, watu wa Roma walichukua usukani duniani.
  • Warumi walileta amani kote duniani.
  • Hii amani iliitwa PAX ROMANA. Hakukuwa na wezi, alshabab, M23, al-Qaida njiani. Warumi walileta amani pote duniani.
  • Milango ya vita ilifungwa. Miungu ya vita “Janus” Mungu wa vita alisahaulika Maanake hakukuwa na vita duniani.
  • Barabara zilijengwa kote, barabara za lami.
  • Barabara zote zilielekea Roma (all roads led to Rome!!)
  • Hali ya huduma za posta ziliendelea kote.
  • Wasafiri wote walilindwa.
  • Kaisari Agusto alipotangaza kuandikishwa watu wote (universal census) hakujua alikuwa anafanya kazi ya Mungu.
  • Kumbe alikuwa ametumwa na Mungu hili Yusufu na Mariamu watoke Nazareti mpaka Bethlehemu alipozaliwa Mwokozi Yesu Kristo.

UTIMILIFU WA WAKATI-KIROHO

  • Wayahudi walipata muda wa kujenga sinagogi kila mji duniani.
  • Dunia ilikuwa tayari kwa kuzaliwa kwa Yesu Kristo.
  • Ahadi ya Mungu katika shamba la Edeni-Mwanzo 3:15 ilikuwa karibu kutimia.
  • Ahadi ya Mungu kwa Ibrahimu-Mwanzo 12:1-3 ilitimia.
  • Ahadi ya Mungu-Mwanzo 49:10 kwa Mwokozi atatoka Yuda ilitimia.
  • Ahadi ya Mungu-Isaya 7:14 ilitimia.
  • Ahadi ya Mungu-Mika 5:2 ilitimia.
  • Ahadi ya Mungu-Zakaria 9 ilitimia.
  • Ahadi ya Mungu-Danieli 9:24-27 ilitimia.
  • Wakati wa nabii wa Agano la kale ulitia kikomo na nabii Malaki.
  • Miaka ya kimya 400 ilitimia-Malaki-Mathayo.
  • Mungu alionekana kama amekimya na kumbe alikuwa kazini.
  • Mungu alitayarisha dunia yote kwa kuzaliwa kwa Yesu Kristo.
  1. Amani duniani-PAX ROMANA/International peace.
  2. Dini zote zilikuwa katika hali tatanishi.
  3. Dhambi zilizidi duniani kote-upagani, uasherati, usoga, mauaji.
  • Mungu hawezi chelewa-Zaburi 31:15; Zaburi 37:23.
  • Mugu alikuwa na mipango yake-Yeremia 29:11.
  • Wayahudi walikuwa katika matarajio makuu-Yohana 1:11.
  • Leo sisi nasi tunatarajia kurudi kwa Yesu Kristo.
  • Mungu anaendelea kutuandaa, je tutakuwa tayari?
  • Leo dunia yote iko tayari kwa kurudi kwa Yesu Kristo, kiroho, utamaduni, kisiasa, huenda hamna na Pax Romana-amani, Lex Romana-sheria ya Roma, Rio Romana-barabara za Roma lakini dunia yote inatarajia Mwokozi-Wagalatia 4:4-7.
  • Mioyo yetu inazidi kulia-Abba Baba-Warumi 8:16-25.

MWISHO

  • Utimmilifu wa wakati ulipofika Mungu alimtuma mwanaye.
  • Utimilifu mwingine ndio huo umefika.
  • Je, wewe uko tayari ajapo? Je, umeokoka?
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Rev, DR. Willy Mutiso

Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Recent Posts

CHRISTMAS: THE BIRTH THAT BROKE EVERY BONDAGE

TEXT: LUKE 2:1-14.   The birth of Jesus Christ shattered spiritual, social and eternal barriers,…

1 day ago

CHRISTMAS: WHY DID CHRIST COME?

TEXT: JOHN 3:16-17.   Christmas unveils the divine mission behind the birth of Jesus Christ;…

2 days ago

KRISMASI MAANAKE NI FURAHA KWA DUNIA YA DHIKI NA SHIDA

MFULULIZO: KRISMASI NI KUFUNULIWA KWA YESU KRISTO.  SOMO: LUKA 2:8-14.   Krismasi inafunua jibu la…

5 days ago

CHRISTMAS IS WHEN HEAVEN CAME DOWN TO EARTH.

SERIES: CHRISTMAS IS CHRIST. TEXT: JOHN 1:1-14.   Christmas is the divine moment when God…

5 days ago

FOR GOD SO LOVED THE WORLD

TEXT: ISAIAH 53:1-12.   The son of man came to seek and save that which…

5 days ago

JESUS OUR SAVIOR

SERIES: CHRISTMAS IS JESUS CHRIST. TEXT: MATTHEW 1:21   Jesus Christ is the savior of…

2 weeks ago