UZIA-ALIANGUKA KWA SABABU YA KIBURI CHAKE.

II MAMBO YA NYAKATI 26

UTANGULIZI

Uzia alikuwa kijana wa miaka 16 alipokuwa mfalme wa Yuda. Alitawala Yuda muda mrefu wa miaka 52. Uzia alifaulu sana kwa maana alikuwa chini ya uongozi wa ushauri wa   Zekaria, Nabii aliyekuwa Muonaji. Neno la   Zekaria kwa mfalme Uzia ilikuwa hii “mkimwacha Mungu, hamuwezi kufaulu” (II Mambo 24:20). Neno la Mungu lilipenya katika moyo wa uzia tangu ujana wake, Uzia alimtafuta Bwana wakati wa Zekaria (V.5). lakini Zekaria alipofariki, mfalme Uzia alianguka sababu ya kaburi. Hebu tuone:-

I.  USHUHUDA MWEMA (V.5)

“Akajitia nia amtafute Bwana Mungu katika siku za Zekaria, aliyekuwa na ufahamu katika maono ya Mungu, na muda alipomtafuta     Bwana, Mungu alimfanikisha” V.5

  • Mungu alipopata nafasi yake katika maisha na kazi ya Uzia, Uzia alifanikishwa sana
  • Ufanisi wa kweli unatokana na Mungu
  • Masharti ya ufanisi wa kweli ni kumtafuta Bwana.

II.  HAKIKISHO YA UFANISI WA MFALME UZIA (V.15)

  • Uzia- “alisaidiwa mno ajabu, hata akapata nguvu”
  • Mungu alimsaidia Uzia dhidi ya wafilisiti na waarabu (V.7)
  • Mungu alimsaidia Uzia sana akajenga minara, mabirika, akawa na ngombe wengi sana, na akapewa wakulima wengi sana. (V.10)
  • Tunaitaji kusaidiwa na Mungu, lakini ni lazima kumtafuta Mungu.

 

 

 

III.  KUELEWA NA MAONO YA MUNGU (26:5)

  • Maono yanatusaidia kujua mahali tumesimama na kuelewa tutasimamia nini. Kwa maana tusipojua maono ya Mungu tutasimamia yeyote yule na kuangukia popote pale.
  • Wasiwasi, majuto, stress na kuvunjika moyo, na kuangaika ni shida ya jamii moja.
  • Hizi zote zinatutokea kwa sababu ya kukosa maono.
  • Tunapokosa maono, tunakosa shabaha na kitambulisho katika maisha yetu.
  • Maono ni nguvu za kuona mbali, ni nguvu za kutarajia yale yanayokuja (sight and foresight) ni nguvu ya kuweza kuelewa na kiini cha mambo jinsi yalivyo (insight)
  • Maono ni nguvu za kuona yasiyooneka na wengi (Waebrania 12:2)

IV.  HAINA MBILI ZA MAONO

  1. MAFUNUO DHAHIRI (I Sam 3:1) Open vision
  2. MAFUNUO YA UONGO (Yeremia 14:14) False vision

V.  HATUA TATU ZA KUELEWA MAFUNUO;

  1. WANA WA ISAKARI (I MAMBO 12:32)
  • Wana wa Asakari walikuwa na uwezo wa kutumia ufahamu wa nyakati na kuelewa yalio mapenzi ya Mungu kwao.
  • Akili za kujua nyakati na kujua yanayopaswa Israeli kuyatenda.
  • Tunaitaji mafunuo ya Isakari leo hii (Yoeli 2:28)
  1. MAFUNUO YA ZEKARIA (II MAMBO 26:5)
  • Haya ni mafunuo ya juu zaidi kuliko ya Isakari. Zekaria alikuwa na uwezo wa kuona maono kutoka mbinguni, alikuwa na uwezo wa kutafsiri maono na kutekeleza mapenzi ya Mungu kwa kila jambo maishani.
  • Maono na mafunuo ya Zekaria yalimsaidia sana mfalme Uzia.
  • Mafunuo haya yanaleta ufanisi kwa mtu.
  1. MAFUNUO YA DANIELI (DANIELI 1:7)
  • Haya ndiyo mafunuo ya juu Zaidi. Danieli alikuwa na uwezo wa kuyajua mavunuo ya watu wengine, kuyatafusiri, kutekeleza na kuwhusisha watu wengi kuyafuata yawe ni maono, mafunuo na ndoto zote.

 

VI.  UKWELI WA MAFUNUO NA NDOTO

  • Mungu ananena kupitia mafunuo na ndoto (Hesabu 12:6, Mwanzo 46:2-3, 15:1)
  • Mafunuo ya Bwana kila mara huleta mabandiliko (Isaya 6:1-5, Matendo 9)
  • Mafunuo ya Mungu yanaonyesha mtu jinsi alivyo ndani yake (Isaya 6:1-5, Matendo 15:26)
  • Mafunuo ni utofauti wa kufaulu na kuanguka
  • Jinsi unavyoona mbali ndivyo utakavyo enda mbali
  • Pasipo na mafunuo watu wanaangamia (Mithali 29:18)
  • Mtu aliye na mafunuo atavumilia mpaka mwisho (Waebrania 12:2)

VII. MFALME UZIA ALIANGUKA (V. 16)

  • “lakini alipokuwa na nguvu moyo wake ulitukuka..” (16)
  • Ni Baraka nyingi kusaidiwa na Mungu na kupewa nguvu,lakini kila Baraka ni mtihani
  • Petro alipewa nguvu kutembea juu ya maji, lakini akayatazama maji akateketea.
  • Elija alipewa nguvu za kushinda Ahabu, lakini alikimbia mbele ya Jezebeli.

Uzia alianguka kwa nini?

  1. “moyo wake ulitukuka. Akafanya maovu, akamwasi Bwana” (26:16-21)
  2. Uzia alipata ukoma mpaka kufa kwake (V.21)
  • Utumishi wa Mungu si mahali pa kuchezea kwa wenye dhambi.
  • Dhambi ya Uzia ilimtenga na jamii na ufalme wa Yuda na Mungu mwenyewe (Isaya 59:2)

 

MWISHO

  • Kuna mtu anasimama kwa sababu yako na mafunuo yako
  • Unapobarikiwa na Mungu usitukuke moyo wako lakini mpe Bwana utukufu wote.
  • Je, umeokoka kweli? Leo ni siku yako kuokoka.

 

The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Rev, DR. Willy Mutiso

Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Recent Posts

MSAADA WA MUNGU WAKATI WA MATESO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: ZABURI 46:1.   Biblia inatuakikishia kwamba Mungu wetu ni “Msaada…

3 weeks ago

GOD GUIDES OUR DESTINIES.

SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: PROVERBS 3:5-6.   Every destiny is a divine…

3 weeks ago

PUT OFF AND PUT ON

SERIES: THROUGH THE BOOK OF COLOSSIANS. TEXT: Colossians 3:5-10   We have put off the…

3 weeks ago

GOD OF THE BREAKTHROUGHS

SERIES: THE GOD WE SERVE TEXT: 2nd SAMUEL 5:17-20   Breakthroughs are divine interventions that…

4 weeks ago

WHO IS SPEAKING TO YOU?

SERIES: DRAWING NEAR TO GOD TEXT: LAMENTATIONS 3:37 It reminds believers that God's word alone…

1 month ago

CHECHEA MSHINDI ALIYE NDANI YAKO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: 1 YOHANA 5:4.   Wakristo wengi wanaishi maisha ya kushindwa…

1 month ago