Categories: Swahili Service

VIKUMBUSHO KWA WASAFIRI NA WAGENI

MFULULIZO: TUMAINI HAI.

SOMO: 1 Petro 2:9-12.

 

Mtume Petro anawaeleza waumini kwamba sisi NI WASAFIRI NA WAGENI duniani. Mgeni maana ni mtu anayeishi kwa muda katika nchi isiyo yake. Huyu mgeni ameishi katika nchi ya kigeni kwa muda kiasi amehitaji kuwa na nyumba ya kuishi na kufanya kazi lakini katika nchi ya ugeni. Lakini yeye si mwananchi. 

Huyu mgeni hana haki ya kisheria na uwananchi.

Msafiri naye mpita njia, Yuko safarini kwenda kwingine.

Maneno haya mawili ndiyo mtume Petro anayatumia kueleza watoto wa Mungu walivyo hapa duniani.

Kwa kweli Dunia hii si kwetu, kwetu ni mbinguni-(Wafilipi 3:20)

“Kwa maana sisi wenyeji wetu uko mbinguni, kutoka huko tena tunatazamia Mwokozi Bwana Yesu Kristo.”

Tuko hapa duniani kiasi kuhitaji nyumba ya kukaa na kazi ya kutupatia riziki, Lakini makao yetu ya kudumu Yako mbinguni kwa Baba.

Sisi ni wageni, tunaishi katikati ya tamaduni za kigeni.

Sisi tunapita njia tukienda kwetu mbinguni.

Tabia yetu si ya ulimwengu huu, sisi tu watoto wa NURU ya Mungu.

Tunapoishi hapa duniani, tunaishi kama Wana wa mbinguni, tumezaliwa kimbinguni- (Wakolosai 3:1-3).

Kwa maana sisi ni wageni hapa duniani, kwa maana sisi ni wasafiri tabia zetu ni za mbinguni, si za Dunia hii.

Katika vifungu hivi Mtume Petro anatukumbusha mambo kadha. Hebu tutazame vikumbusho kwa wasafiri na wageni:-

UKUMBUSHO WA HALI YETU YA PALE KALE.

Maisha yetu ya kale yalikuwa Giza- (V. 9).

  • Tunakumbushwa kwamba Yesu Kristo alitukuta kwa Giza kuu.
  • Tulikuwa katika Giza ya dhambi- (Waefeso 2:1-3).
  • Yesu alitukuta wakati tukiwa katika dhambi tulikuwa kifungoni cha dhambi na mauti-(Mithali 16:25).

Maisha yetu ya kale yalikuwa aibu (V. 10).

  • Alipotujia Yesu Kristo tulikuwa mbali, hatukuwa sehemu ya watu wa Mungu-(Waefeso 2:12, Wakolosai 1:21).
  • Tulikuwa nje ya ufalme wa Mungu, tulikuwa tumeanguka mbali, tulikuwa adui za Mungu-(Warumi 8:7)

Tulikuwa wafu mbele zake-(V. 10).

  • Wakati Yesu Kristo alipotujia tulikuwa bure, hatukustahili Rehema na Neema yake.
  • Tukumbuke hatukuwa wadeni wake.
  • Tulistahili jehanamu, Lakini Neema ya Mungu alitukumbuka.
  • Kwa Neema kwa njia ya Imani tuliokolewa (Waefeso 2:8-9, I Wakorintho 15:10).

UKUMBUSHO WA HALI YETU YA SASA-(V. 10)

Sasa sisi ni viumbe wapya-(V. 9).

  • Sisi ni taifa teule, sasa sisi ni watoto wa Mungu.
  • Mungu alituchagua kwa wema wake.
  • Alichukua watu wa mbali akawafanya viumbe vipya.
  • Mungu alipomwita Ibrahimu, kupitia kwake Mungu alifanya taifa jipya la waebrania.
  • Sisi nasi Mungu ametuita na kuunda taifa jipya la wateule-(I Wakorintho 10:32, I Wakorintho 12:13).

Sasa sisi ni ushirika mpya- sisi ni makuhani wa kifalme (royal priesthood)

  • Tulikuwa mbali lakini sasa sisi ni Wana wa Mungu kwa damu ya Yesu Kristo- (Waefeso 2:13)
  • Kristo amevunja kila ngome na kuta zilizotutenganisha na Mungu muumba wetu- (I Timotheo 2:5, Waefeso 2:14-19, Waebrania 4:16).

Tumepewa tabia mpya.

  • Sisi tunaitwa Taifa Takatifu- (Holy Nation)
  • Kupitia kwa Yesu Kristo Mungu ametubadilisha tukawa viumbe vipya-(2 Wakorintho 5:17).
  • Kuokoka ni kubadilishwa (Isaya 64:6, 2 Petro 1:4, I Petro 1:16).

Tumewekwa kiwango kingine.

  • Sasa tunaitwa “Watu wa milki ya Mungu” (peculiar people)
  • Sisi ni tofauti na Dunia, sisi ni watu wa dhamani zaidi kwa bei tulionunuliwa nayo-(Malaki 4:17, 1 Wakorintho 6:19-20).

UKUMBUSHO WA JINSI TULIVYO KATIKA UTUMISHI

  • Sisi tu mabalozi wa Yesu Kristo-(2 Wakorintho 5:20).

V. 9-Tunahitaji kutangaza ukweli wa mwokozi wetu Yesu Kristo.

  • Tunatangaza fadhili zake kote duniani.
  1. Mwenendo safi (Vs. 11) Kwa maana sisi ni viumbe vipya- mwenendo wetu si wa Dunia hii- kwetu ni mbinguni.
  2. Ni lazima tutangaze kwa nguvu zote (V. 12) wema na fadhili zake kwetu.

   MWISHO.

  • Mpaka Yesu Kristo arudi, tutaendelea kuwa wageni na wasafiri duniani.
  • Tukumbuke kwamba tumezingirwa na watu wa mataifa wenye tabia ya kigeni- Basi tuwatangazie wokovu wa Mungu wetu.
  • Kama Balozi wa Yesu Kristo tuwafundishe mataifa tamaduni za mbinguni.
  • Tukaache Dunia hii bora zaidi kuliko jinsi tuliikuta.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Rev, DR. Willy Mutiso

Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Recent Posts

MSAADA WA MUNGU WAKATI WA MATESO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: ZABURI 46:1.   Biblia inatuakikishia kwamba Mungu wetu ni “Msaada…

11 hours ago

GOD GUIDES OUR DESTINIES.

SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: PROVERBS 3:5-6.   Every destiny is a divine…

13 hours ago

PUT OFF AND PUT ON

SERIES: THROUGH THE BOOK OF COLOSSIANS. TEXT: Colossians 3:5-10   We have put off the…

15 hours ago

GOD OF THE BREAKTHROUGHS

SERIES: THE GOD WE SERVE TEXT: 2nd SAMUEL 5:17-20   Breakthroughs are divine interventions that…

2 weeks ago

WHO IS SPEAKING TO YOU?

SERIES: DRAWING NEAR TO GOD TEXT: LAMENTATIONS 3:37 It reminds believers that God's word alone…

3 weeks ago

CHECHEA MSHINDI ALIYE NDANI YAKO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: 1 YOHANA 5:4.   Wakristo wengi wanaishi maisha ya kushindwa…

3 weeks ago