Categories: Swahili Service

VITA JUU YA IBADA.

MFULULIZO: DANIELI MUNGU NDIYE HAKIMU.

SOMO: DANIELI 3:1-30

 

Shetani adui yetu yuko vitani dhidi ya wale wanao mwabudu Mungu katika kweli na Roho. Leo tutazitazama silaha anazotumia na jinsi ya kushida vita juu yake.

Mwongozo wa kitabu cha Danieli ni ukuu wa Mungu wetu Yehova Mungu wa Israeli.

Mungu ni mwenye nguvu zote, tena anayafahamu yote. Hivyo Mungu ndiye pekee anayestahili sifa na Ibada.

Shetani adui naye anategeneza vita juu ya Ibada. Ibada ni kuanguka chini na kusujubu.

Katika Danieli 3, tunaona vita kali juu ya Ibada ya kweli. Ikiwa unaenda vita lazima kuwa na silaha. Adui anazo silaha anazotumia juu ya wanaomwabudu Mungu katika kweli na Katika Roho. Hebu tutazame:-

JE, SILAHA ZA SHETANI ZA VITA DHIDI YA IBADA NI GANI?

  • Hapa tunapata silaha nne (4) dhidi ya Ibada:
  1. Sanamu-(5:1)

“Mfalme Nebukadreza, alifanya sanamu ya dhahabu , ambayo urefu wake ulikuwa ni dhiraa sitini na upana wake dhiraa sita akasimamisha katika uwanda wa Dura Katika wilaya ya Babeli.”

  1. Maanake sanamu-
    • Sanamu ni chochote kinacho simama mahali na Nafasi ya Mungu Mwenyezi.
  2. Mifano ya sanamu-(Mathayo 13:16-23) (22)

“………….Shughuli za dunia na udanganyifu wa mali hulisonga, mle neno likawa halizai.”

  1. Vita juu ya Ibada ni kubwa sana, Sanamu zake ni kubwa kiasi 90ft urefu wa 9 ft upana wake.
  • Sanamu zinakuwa upesi zinakua kubwa na kubwa zaidi mpaka zinachukua sehemu yote ya Ibada yetu kwa Mungu.
  1. Wasawishi na Mashabiki (V.2-3)

“Ndipo Nebukadreza akatuma watu kuwakusanya , maamiri na manaibu, na maliwali, na mawaziri na mawakili na wakuu wa wilaya zote ili wahudhurie wakati wa kuizindua ile sanamu.”

  1. Je, hawa watu wote wana nini cha kufanana?
  • Hawa ni watawala wenye nguvu na mamlaka wenye kuwasawishi watu, wenye kusema!!
  • Baada ya kuwaita mwenye kusema, Nebukadreza aliwaita mastar wa sinema, wasanii, waimbaji , mwenye kutangaza, wa biashara wanariatha, waandishi, warebu na maselebu, na wote walialikwa kuzindua ile sanamu ya dhahabu.
  1. Adui anapotaka kushinda vita juu ya Ibada kwa Mungu anafahamu lazima kupata idhini kutoka kwa selebu
  2. Silaha ya tatu dhidi ya Ibada ya Keseli ni nyimbo, Style na Muziki (v.5)
  • Kuna nyimbo ambazo zikiiimbwa zinakufanya kupenda kuanguka na kuabudu sanamu.
  • Hizi ni nyimbo zinazokuvutia mbali na Ibada kwa Mwenyezi Mungu. Hizi ni nyimbo zinazo pendeza mwili na kusifu wanadamu kuliko kumsifu Mungu.
  • Hizi ni nyimbo zinazo kufanya yasiyompendeza Mungu.
  • Nyimbo na sauti hizi ni Silaha ya shetani dhidi ya Ibada , Katika kweli na katika
  1. Silaha ya Nne (4) ya vita juu ya Ibada ya kweli ni kusurutishwa kitakachofanywa kwako ikiwa utaabudu Mungu-Vs. 6.

“Na kila mtu asiyeanguka na kuabudu atatupwa saa hiyo hiyo katika tanuri ya moto uwakao.”

  • Adui anao njia ya kufanya mambo yawe magumu kwa wale watakataa kuabudu sanamu.
  • Je, ibada inaweza kulazimishwa juu ya mtu?
  • Ibada ya kweli inatoka kwa moyo na uhuru wa mwenye kuabudu.
  • Je, silaha hizi za shetani zina nguvu?-Vs. 7.

“Basi wakati huo, watu wa kabila zote waliposikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na zomari na namna zote za ngoma, watu wote na mataifa na lugha wakaanguka, wakaiabudu ile sanamu, mfalme Nebukadreza aliyoisimamisha.”

VITA JUU YA IBADA YA MWENYEZI MUNGU HAIKUFAULU-Vs. 12.

“Lakini wako Wayahudi kadha wa kadha uliowaweka juu ya mambo ya wilaya ya Babeli, yaani Shadraka, Meshaki na Abednego, watu hawa Ee mfalme, hawakujali wewe, hawaitumikii miungu yako, wala kuiabudu ile sanamu ya dhahabu ulioisimamisha.”

  • Mashitaki yalikuwa tatu dhidi ya Shadraka, Meshaki na Abednego.
  1. Hawa watu hawakujali wewe mfalme.
  2. Hawa watu hawaitumikii miungu yako.
  3. Hawa watu hawaiabudu ile sanamu ya dhahabu uliosimamisha.
  • Hapa panao somo kwetu.
  1. Kile unajali sana, utakitumikia.
  2. Kile unacho tumikia utakiabudu.
  3. Ikiwa haupendi unachoabudu, basi usikipe wakati wako, wala kukijali.
  4. Ikiwa unapenda kumwabudu Mungu zaidi, basi mpe wakati wako na kumjali.

“Basi kwa hasira Nebukadreza akatoa amri kwa ghadhabu waletwe hao Shadraka na Meshaki na Abednego. Basi wakawaleta watu hao mbele ya mfalme”-Vs. 13.

  • Nebukadreza alitumia silaha ya kusurutisha.

“Vs. 15, “Basi sasa, kama mkiwa tayari wakati mtakapoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na zomari na namna zote za ngoma, kuanguka na kuisujudia sanamu niliyoisimamisha ni vema; bali msipoisujudia, mtatupwa saa hio hio katika tanuri iwakayo moto. Naye ni nani Mungu yule atakayewaokoa nyinyi na mikono yangu?”

  • Silaha ya kusurutisha inafanya kazi shetani anafanya shida yako kuonekana kubwa kuliko Mungu wako”-Vs. 16-18.
  • Lakini silaha ya kusurutisha haifanyi kazi juu ya Shadraka, Meshaki na Abednego.
  • Kila mkristo anahitaji vitu tatu kumuabudu Mungu:-
  1. Ushawishi-(conviction).
  • Ni lazima ushawishike ndani ya moyo wako kumuabudu Mungu-Kutoka 20:1-6.
  • Danieli 3:16-18, “Ee Nebukadreza hamna haja kukujibu katika hili.”
  • Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa nguvu zako zote na kwa nafsi yako yote.
  • Bila kuwa na ushawishi ndani yako utapoteza vita juu ya ibada yako kwa Mungu.
  1. Ujasiri-Confidence.
  • Shadraka, Meshaki na Abednego walikuwa na ujasiri mkuu katika Mungu wao.

“Mungu wetu tunaye mtumikia aweza kutuokoa na tanuri ile iwakayo moto, naye atatuokoa na mkono wako, ee mfalme, bali kama si hivyo ujue ee mfalme ya kuwa sisi hatukubali kuitumikia miungu yako, wala kuisujudia hiyo sanamu uliosimamisha.”

  • Ujasiri unatokana na ushawishi.
  • Kila mahali, kila wakati, kwa njia zote, Mungu anaweza kuokoa.
  • Muabudu Mungu wako hata kabla hajakuokoa.
  1. Kujitoa-Commitment.
  • Hawa vijana Waebrania walijitoa muanga.
  • Haijalishi hata Mungu asipowaokoa bado watamtumikia Mungu.
  • Ushawishi, ujasiri na kujitoa kabisa kwa Mungu ndio ibada ya kweli.

SOMO JUU YA WATU WA MUNGU.

  1. Watu wa Mungu ni watu wanaoteswa-Vs. 19-23.
  • Tutajaribiwa imani yetu kwa moto mara saba.
  1. Watu wa Mungu wanateswa kwa sababu ya imani.
  2. Watu wa Mungu wanateswa kwa sababu ya Mwokozi wao-3:13-15.
  3. Unapotupwa motoni kitakacho chomeka ni kamba zinazokufunga. Yesu ataonekana karibu.
  4. Watu wa Mungu ni watu wakupandishwa cheo-Vs. 28-30.
  5. Unaposimamia ukweli-utasimama peke yako.
  6. Unapotembea na Mungu hauko peke yako.
  7. Mungu wetu hawezi kufananishwa-Vs. 28-30.
  • Wacha Mungu aitwe Mungu-Amen.

MWISHO

  • Lengo la somo letu ni kujenga, usawishi, ujasiri na kujitoa kumtumikia Mungu na kumwabudu yeye pekee.
  • Pamoja na vitisho kutoka kwa wenye mamlaka-Mungu wetu anaweza kutuokoa na hata bila wokovu wake, bado tutamtumikia Mungu.
  • Je, tutamwabudu Mungu hata bila kuona ushindi hau tutangojea ishara kwanza?
  • Tunapomsimamia Mungu, Mungu atatusimamia.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Rev, DR. Willy Mutiso

Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Recent Posts

MSAADA WA MUNGU WAKATI WA MATESO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: ZABURI 46:1.   Biblia inatuakikishia kwamba Mungu wetu ni “Msaada…

3 weeks ago

GOD GUIDES OUR DESTINIES.

SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: PROVERBS 3:5-6.   Every destiny is a divine…

3 weeks ago

PUT OFF AND PUT ON

SERIES: THROUGH THE BOOK OF COLOSSIANS. TEXT: Colossians 3:5-10   We have put off the…

3 weeks ago

GOD OF THE BREAKTHROUGHS

SERIES: THE GOD WE SERVE TEXT: 2nd SAMUEL 5:17-20   Breakthroughs are divine interventions that…

4 weeks ago

WHO IS SPEAKING TO YOU?

SERIES: DRAWING NEAR TO GOD TEXT: LAMENTATIONS 3:37 It reminds believers that God's word alone…

1 month ago

CHECHEA MSHINDI ALIYE NDANI YAKO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: 1 YOHANA 5:4.   Wakristo wengi wanaishi maisha ya kushindwa…

1 month ago