Categories: Swahili Service

VITU VYETU VYA DHAMANI.

MFULULIZO: YESU KRISTO KWETU NI DHMAMANI

SOMO: 1 PETRO 1:1-4.

 

Katika Petro wa kwanza na wa pili, mtume Petro mara 5 anataja vitu vya dhamani ambavyo Mungu amewapa watu wake. Tunaposema kitu cha dhamani, watu wengi wanafikiri dhamni ni kitu ambacho ni cha maana sana. Pengine wengine wanasema watoto wao ndio dhamani zaidi, pengine mke au mume wake ndio dhamani zaidi. Kwa wengi ni fedha zao, dhahabu na gari zao.

Huko Marekani kuna museum iitwao Smithsonian institute of natural science and history. Kuna jiwe moja ya maana sana iitwayo “Hope Diamond,” (“Almasi ya tumaini).” Hili jiwe linalindwa na kamera na askari polisi, ndani yake kuna almasi ya dhamani sana.

Kama waumini kuna vitu vya dhamani sana ndani yetu, ndivyo Petro anasema tunalindwa sana ndani ya Kristo Yesu. Kila kitu na mali tuliyo nayo itateketea kutoka hapa duniani. Watu tulionao, watoto, wazazi, wandugu, mke, mume watateketea siku moja kutoka dunia hii. Hata “Hope diamond” itateketea siku moja.

Lakini sisi tumepewa vitu vya maana sana na vya dhamani haviwezi kuteketea kamwe. Leo tunatazama vitu vya dhamani zaidi ambavyo vimewekwa dhamani ndani yetu. Hili tupate kuvielewa vitu hivi dhamani tutasoma katika nyaraka zote mbili za Petro. Hebu tuone hizi vitu vya dhamani:-

MAJARIBU YETU NI YA DHAMANI-1 Petro 1:7.

  1. Petro anatueleza kwamba majaribu ya imani yetu ni ya dhamani sana!!
  • Mabonde tunayopitia, moto tunaopitia.
  • Moto tunaopitia unajaribu imani yetu kama jinsi dhahabu lazima kupitia kwa moto.
  • Majaribu ya imani inatusafisha ili tuwe safi sana.
  • Katika yale majaribu tunamjia Kristo karibu zaidi.
  • Wanaojaribiwa wako karibu na Mungu zaidi.
  1. Katika bonde za maisha, tunakumbushwa ukweli mkuu zaidi.
  1. Tunakumbushwa kuwa Yesu Kristo yu pamoja nasi-Waebrania 13:5; Yohana 6:16-20.
  2. Tunakumbushwa kwamba hata katika dhoruba na mabonde Mungu ni yeye amepanga yote-Warumi 8:28; Isaya 45:7.
  3. Tunakumbushwa kwamba katika majaribu tunakua zaidi katika Yesu Kristo-2 Wakorintho 4:17.
  4. Tunakumbushwa kwamba mema yanatungojea mbele-Warumi 8:18.
  5. Tunakumbushwa kwamba hata mambo yawe mabaya Mungu angali mwema-Ayubu 1:20-21.
  1. Katika majaribu na mabonde ya maisha tutatokea tukiwa bora zaidi, tunapata nguvu zaidi na imani yetu inakua zaidi tunapojaribiwa.
  • Wanafunzi wa Kristo walipata nguvu zaidi walipojaribiwa, Meshack, Shadrach na Abednego walimfahamu Mungu zaidi katika ule moto.
  • Nuhu alipata imani timilifu wakati wa kujaribiwa.
  • Martha na Mariamu walipata nguvu zaidi katika kifo na kufufuka kwa Lazaro ndugu yao.
  • Katika njaa nyikani wale watu 5,000 walipata imani timilifu walipolishwa na Kristo.
  • Majaribu na mabonde yanatuonyesha Mungu na nguvu zake juu ya maisha yetu.

DAMU YA YESU NI YA DHAMANI-1 Petro 1:19.

  1. Damu ya Yesu Kristo ni dhamani sana.
  • Tunahitaji kudhamini sana damu ya Kristo.
  • Tunahitaji kujifunika kwa damu yake kila saa. Damu ya Yesu Kristo ni ya dhamani.
  1. Damu ya Yesu Kristo ndiyo bei hasa ya ukombozi-1 Petro 1:19.
  2. Damu ya Yesu Kristo ni ishara ya upendo wa Mungu kwetu-Warumi 5:8.
  3. Damu ya Yesu Kristo pekee inaosha dhambi zetu zote-Ufunuo 1:5; 1 Yohana 1:7.
  4. Damu ya Yesu Kristo pekee inakubaliwa juu mbinguni.
  • Damu ya Kristo ni ya dhamani sana.
  1. Kwa maana damu ya Yesu Kristo ni ya dhamani sana, basi tunahitaji kuidhamani zaidi.
  • Wacha tukadhamini ile damu yake.
  • Wacha tukadhamini ule msalaba wake.
  • Msalaba hauokoi, lakini kazi iliyofanyika mle msalabani.
  • Siku hizi wahubiri wengi hawataki kutaja damu na msalaba, lakini kwetu ule msalaba na ile damu na yeye aliyemwaga damu yake ni dhamani sana.

MWOKOZI WETU NI WA DHAMANI-1 Petro 2:6-7.

  1. Petro anazidi kutueleza kwamba Yesu Kristo mwenyewe ni wa dhamani.
  • Yesu Kristo ni wa dhamani sana kwa wale wameokoka.
  1. Yesu Kristo ni wa dhamani kwa Watakatifu wa Mungu.
  1. Kwa sababu anatupenda-Yeremia 31:3; Warumi 8:38-39.
  2. Kwa sababu Yesu Kristo anatujali-1 Petro 5:7.
  3. Kwa sababu Yesu Kristo anaelewa na mahitaji yetu-Waebrania 46:1.
  4. Kwa sababu Yesu Kristo alilipa gharama za wokovu wetu-Yohana 15:13.
  • Watu wengine wote watakuangusha, lakini Yesu Kristo hawezi.
  1. Watu watakuacha.
  2. Wapenzi wako watakuacha.
  3. Kanisa linaweza kukuacha.
  4. Serikali imekuacha.
  • Lakini Yesu Kristo hawezi kukuacha.
  • Nilipomjia alinipokea jinsi nilivyokuwa-Yohana 6:37; 1 Yohana 1:9.
  • Mwokozi wetu ni wa dhamani zaidi.

IMANI YETU NI YA DHAMANI SANA-2 Petro 1:1.

  1. Petro anazidi kutueleza kwamba imani yetu ni dhamani sana.
  2. Imani yetu ni ya dhamani zaidi kwa maana ndiyo imani pekee inapokelewa mbinguni kwa Mungu.
  • Imani zingine zile ni udanganyifu wa mwanadamu, Islamu, Mormon, Buddha, Hindu, shindoism,  dini za kiafrika, Regio, catholic (Roman).
  • Njia pekee ni Yesu Kristo-Yohana 14:6.
  1. Imani yetu ni ya maana na dhamani kwa sababu:
  1. Ni bila malipo-Ufunuo 22:17; Isa. 55:1.
  2. Imefunguliwa kwa wote-Yohana 3:16; Warumi 10:13.
  3. Inatosha na kamilifu-Waebrania 7:25.
  4. Ni kazi ya Mungu-Waefeso 2:8-9; Waebrania 12:2.
  5. Haina udanganyifu wowote-Matendo 16:31.
  6. Ni imani ya milele-Yohana 6:37; 10:28.

AHADI TUMEPEWA ZA DHAMANI SANA-2 Petro 1:4.

  1. Petro anaeleza kwamba tumepewa ahadi za milele, ahadi za kweli.
  • Tunahitaji kushika ahadi za Mungu, ni ahadi za kweli.
  1. Ahadi hizi ni za nguvu.
  1. Ahadi ya upendo wake Mungu-Warumi 8:38-39; Yeremia 31:3.
  2. Ahadi ya uwepo wake Mungu-Mathayo 28:20; Waebrania 13:5.
  3. Ahadi ya utoshelevu wake-Wafilipi 4:19; Mathayo 6:25-33.
  4. Ahadi ya neema zake-2 Wakorinthi 2:9.
  5. Ahadi ya mbinguni-Yohana 14:1-3; Ufu. 21:4.
  1. Imesemekana kwamba tumepewa ahadi 7,000 katika Biblia.
  2. Ahadi za Mungu ni za milele, ahadi za mwanadamu zinabadilika, lakini Mungu habadiliki.

MWISHO

  • Mungu kwa kweli ametupatia vitu vya dhamani sana.
  • Je, utalinda vitu hivi vya dhamani?
  • Pengine leo hii wewe utadai ahadi moja ya hizi ahadi.
  • Je, umeokoka, leo mjie Mwokozi wako.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Rev, DR. Willy Mutiso

Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Recent Posts

MSAADA WA MUNGU WAKATI WA MATESO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: ZABURI 46:1.   Biblia inatuakikishia kwamba Mungu wetu ni “Msaada…

2 weeks ago

GOD GUIDES OUR DESTINIES.

SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: PROVERBS 3:5-6.   Every destiny is a divine…

2 weeks ago

PUT OFF AND PUT ON

SERIES: THROUGH THE BOOK OF COLOSSIANS. TEXT: Colossians 3:5-10   We have put off the…

2 weeks ago

GOD OF THE BREAKTHROUGHS

SERIES: THE GOD WE SERVE TEXT: 2nd SAMUEL 5:17-20   Breakthroughs are divine interventions that…

3 weeks ago

WHO IS SPEAKING TO YOU?

SERIES: DRAWING NEAR TO GOD TEXT: LAMENTATIONS 3:37 It reminds believers that God's word alone…

4 weeks ago

CHECHEA MSHINDI ALIYE NDANI YAKO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: 1 YOHANA 5:4.   Wakristo wengi wanaishi maisha ya kushindwa…

1 month ago