Categories: Swahili Service

WACHA KUMWIBIA MUNGU

MALAKI 3:6-12

Mpango wa Mungu juu ya mali na fedha zako ni tofauti sana na mpango wa dunia. Watu wanasema kusanya mali na fedha na usitoe. Mungu anapendezwa tunapotoa (Mithali 28:27) watu wanao toa na kuwapa wengine wanakuwa watu wa furaha, amani na salama (Mithali 19:17, 22:9) .Yesu kristo alitufundisha kanuni ya kutoa na kupokea (Luka 6:38)

Tunahitaji kujiona kama watoaji wala si      wapokeaji tu. (dead sea and sea of Galilee) channels and not reservoirs. Watu wa Israeli wakati wa Malaki walikuwa na shida ya     kumwacha Mungu.

Hebu tuone:-

  1. WACHA KUMWIBIA MUNGU (MALAKI 3:6-9)
  • Mungu wa Israeli asema hapa “nirudieni mimi, nami nitawarudia nyinyi”
  • Katika kifungu cha 8, Mungu anasema “je, mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi.”
  • Walimwibia Mungu kwa njia gani? “mmeniibia zaka na dhabihu”
  • Zaka maana yake ni “fungu la kumi”
  • Kumbuka ni lazima kumpa Mungu yaliyo mema na bora zaidi (give God the best) kumpa Mungu kinachokugharimu (give to God that which costs you.)
  • Mungu anasema nirudieni, kuwa karibu na Mungu, kupitia kwa matoleo yako. Usimnyime Mungu zaka na sadaka yako.
  • Usiwache chochote kusimama katikati yako na Mungu wako – usiwache fedha yako kusimama kati yako na Mungu wako.
  • Matajiri wanapenda fedha zao, lakini zaidi watu wa mapato ya chini ni wachoyo kwa Mungu sana.
  • Kazi ya Mungu si kukunyanganya vitu lakini kukupatia vitu.
  • Mungu kweli haitaji fedha zako! Huko mbinguni barabara zimejengwa kwa dhahabu safi, milingo ya huko ni almasi safi!! Kuta za mbinguni ni mawe ya dhamani sana.
  • Lakini Mungu anadai zaka na sadaka kwa sababu ya utii na upendo wako.
  • Pia, kanuni ya kutoa na kupokea, ni kanuni ya kupanda na kuvuna (luka 6:38). Upendo kazi yake ni kutoa (yohana 3:16)

II.  JITOE KUTOKA KWA LAANA YA UMASIKINI (MALAKI 3:9)

  • “Ninyi mmelaaniwa kwa laana, maana mnaniibia mimi.”
  • Kutotoa zaka na sadaka ni laana juu ya laana “mmelaaniwa kwa laana.”
  • Unapoishi katika laana hauwezi kupokea Baraka, huwezi kuona msaada wako.
  • Kwanza jitoe kwa laana, Baraka zitakwadama na kukupita na kukugojea mbele yako na jamii yako.
  • Wengi kanisani wanateseka leo kwa maana hawatoi kama ilivyo.
  • Zaka ni ya Bwana, lakini dhabihu, sadaka na matoleo yale mengine ni zaidi juu ya zaka yako.
  • Tunapolaaniwa si Mungu analaani, lakini ni sisi twajilaani—tunavuna tulichopanda, laana kwa laana, baraka kwa Baraka.

III. LETENI ZAKA KAMILI GHALANI (MALAKI 3:10)

  • Ghala la Mungu ni kanisani unapolishwa neno na kushiriki.
  • Zaka yako si kwa vituo vya TV – (runinga) huko unawapa mchango wako. (Zaburi 35)
  • Zaka yako ni 10% gross si net. Unataka Mungu akupe Baraka ya jumla gross si net. (Mithali 3:9)
  • Zaka ni sehemu ya kwanza ya mapato yako, tenga sehemu ya kwanza.
  • Mungu anasema tumujaribu kwa njia ya kutoa zaka kamili.
  • Mungu atayafungua madirisha ya mbinguni na kumwanga Baraka hata isiwepo nafasi ya kutosha.
  1. Madirisha ya mbinguni ilifunguliwa mara moja hapo mwanzo (Mwanzo 7:11-12) (3:10)
  • Kumbuka kwamba zaka si yako, bali ni ya Mungu hivyo zaka haiwezi kuwa mbengu yako ya kupanda.
  • Sadaka na dhabihu yako ndizo mbengu yako ya kupanda (II Wakorintho 9:9-10)
  • Unapotoa sadaka yako, Mungu atakupatia kibali mbele ya watu, hivyo utazindishiwa, kupandishwa na kuongezewa zaidi, maana upendo unatoa.
  1. Mungu atawakemea yeye alaye. (3:11)
  • Kuna vitu vinavyo kula fedha zetu tusipotoa zaka na sadaka. Magojwa, magari kuaribika, malipo ya kila haina.
  • Bwana atajenga kuta, shetani hawezi kupanda.
  1. Kanuni na sababu ya zaka (10%0
  • Mungu anapenda kilicho bora zaidi (Mithali 3:9)
  • Mpe Mungu yaliyo bora zaidi kila juma hau kila mwezi.
  • Sababu ya zaka ni ibada, kuwatumikia makuhani kuisafi nyumba ya Bwana.

MWISHO

  • Zaka na sadaka zako zinafungulia Baraka zako (kumbu kumbu 28:8)
  • Zaka na sadaka zako zitamaliza umasikini kwako (Luka 6:38)
  • Wacha kumwibia Mungu wako, zaka ni yake Mungu.

 

The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Rev, DR. Willy Mutiso

Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Share
Published by
Rev, DR. Willy Mutiso

Recent Posts

DAMU YA UTAKASO.

MFULULIZO: AGANO LA UTAKASO. SOMO: KUTOKA 12:12-13.   Damu ya Yesu Kristo ndiyo mhuri wa…

11 hours ago

KEY TO DIVINE SPEED.

SERIES: SUPERNATURAL ADVANCEMENT. TEXT: HABAKKUK 3:19.   The journey of fulfilling your destiny does not…

13 hours ago

BE YE THANKFUL TO GOD.

SERIES: THROUGH THE BOOK OF COLOSSIANS. TEXT: COLOSSIANS 3:15   Thankfulness is a great attitude…

15 hours ago

LEVELS OF THE ANOINTING.

SERIES: THE ANOINTING. TEXT: EZEKIEL 47:1-5   There are levels of the anointing and each…

4 days ago

UMETAKASWA KUPOKEA KIBALI.

MFULULIZO: AGANO LA UTAKASO. SOMO: ESTA 2:15-18.   Kibali cha Mungu ndicho kinacho watenga watoto…

1 week ago

THE GOD WHO SHIFTS THE HEAVENS IN YOUR FAVOR.

SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: HAGGAI 2:6-9.   God has the power to…

1 week ago