MFULULIZO: MAISHA NA NYAKATI ZA ELISHA
SOMO: 2 WAFALME 6:8-23 (16).
Watu wa Mungu wanaonekana dhaifu, tunapowalinganisha na watu wa dunia. Lakini hio si kweli. Nguvu na uwezo ziko na kanisa kwa maana jeshi lisiloonekana linawazingira watu wa Mungu kila wakati. Walio nasi ni wengi kuliko walio pamoja nao-Vs. 16.
Tunahitaji kufunguliwa macho ya kiroho kuona majeshi wa Mungu na Majeshi (Yehovah-Sabaoth) Mungu wa Majeshi-Vs. 17.
- Majeshi ya dunia hii-China=4 million, India 2 million, USA-1 million.
- Jeshi la wadudu-Yoeli 2:15-zinge, taoni.
- Jeshi la malaika wa mbinguni-Waamuzi 5:20; 2nd Sam. 5:24; 2nd Wafalme 6:17.
- Watu wa Mungu. Sisi zote ni jeshi kuu, kanisa lililo mbinguni na kanisa lilio duniani.
- Jeshi la maji; hewa, miti, mawe, mwezi, jua, barafu (Napoleoni-500,000 walikufa).
Mfalme wa Shamu alikuwa akifanya vita na Israeli.
Kwa siri aliamisha majeshi yake mpaka nchi ya Israeli.
Lakini nabii Elisha kwa neno la ufahamu na hekima alionyeshwa na Mungu mienendo yao na kumweleza mfalme wa Israeli.
Mfalme wa Shamu aliona ni vyema kumkamata Elisha.
Elisha aliwatumia majeshi ya Shamu upofu.
Hivyo Elisha akawakamata wote na kuwapeleka kwa mfalme wa Israeli mle Samaria.
Jeshi la Shamu likawa maabusi wa vita (prisoner of war), baadaye Elisha akawarudishia nguvu za kuona tena!! Kasha akawarudisha huko kwa Shamu kwa aibu nyingi mno.
Katika ujumbe wetu leo, tunatazama mambo tatu.
- Je, watu wa Mungu ni wadhaifu na masikini?
- Je, Mungu wetu ni ngao tosha mbele ya adui zetu?
- Je, Bwana anawazingira watu wake kwa jeshi lisiloonekana kwa macho ya mwili? Hebu tutazame:-
WATU WA MUNGU WANAONEKANA WANYONGE, MASKINI.
Elisha na mtumishi wake.
- Watu wa ulimwengu wanaendesha mambo yao kwa kutegemea isia zao, macho, sikio, pua, kupapasa, ndimi zao kuonja (senses).
- Mambo yasioonekana kwao ni hali ya mazingaombwe na shetani.
Mfalme wa Shamu Beni Hadadi 2 aliwatumikia wapelelezi, kupeleleza Israeli, lakini kila wakati alipowatumia Elisha alimjulisha mfalme wa Israeli.
- Beni Hadidi 2, alijulishwa na majeshi yake kwamba, Elisha anafahamu na kuona mambo yote, hata mpaka kwa chumba cha kulala mfalme!!
- Siku ya leo tunajua, kila mtu aliye na simu ya mobile anajulikana mpaka kuonekana na kusikilizwa na serikali yao.
Kwa maili nyingi sana, kupitia neno la ufahamu (word of knowledge) juu ya mfalme wa Shamu, Elisha alifahamu yote anayopanga mfalme juu ya Israeli-Mithali 15:3.
Mungu anafahamu tutakachosema kabla hatujasema. Hatuwezi kuficha chochote kutokana na macho ya Mungu-Ayubu 5:12.
Beni Hadadi alitumia jeshi lake kumkamata Elisha. Jeshi la Shamu lilikuwa na nguvu zaidi ya Israeli. Alifikiri kwa vita vya usiku akamkamata Elisha kuishi kupigana na Israeli.
- Wakristo wanaonekana dhaifu leo.
- Elisha mtumishi wa Mungu anatuwakilisha kama watu wa Mungu.
- Maaadui wetu ni wengi zaidi, hatuna silaha za vita, dunia ina silaha zote na systems.
- Unapo tazama adui zako ni wengi na wenye nguvu, wanao pesa zaidi. Je, Mungu anawajali watu wake?
- Kuteseka kama wakristo ni pamoja na mpango wa Mungu kwa maisha yetu-Mathayo 5:11-12; Wafilipi 1:29; 2nd 1:8; 2:3.
- Kuteseka kama wakristo ni kunaonyesha sisi ni kama Yesu Kristo-1st Petro 4:14. Roho ya ulimwengu itatesa Roho wa Kristo-Wagalatia 4:29. Tumebarikiwa tunapoteseka!!
- Kuteswa kama mkristo kunaleta utakatifu-1st Petro 2:12.
- Dhawabu zetu mbinguni zinategemea vile uliteseka kwa ajili ya Kristo-2 Wakorintho 4:17.
- Paulo na Sila waliteswa sana, wakafurahi!!-2 Wakorintho 1:10; Wafilipi 1:19; 2 Timotheo 4:17; Matendo 12:17.
MUNGU NDIYE NGAO YETU.
Maandiko yanatueleza na kutuahidi ulinzi, usalama na udhabiti.
- Mungu ni ukuta kuwazunguka watu wake-Zakaria 2:5. Hakuna silaha itaweza-Isaya 54:17.
- Jina la Bwana ni ngome imara-Mithali 18:10.
- Kristo yuko pamoja na watu wake-Mathayo 18:20
- Mapepo watoroka-Marko 16:17.
- Kwa jina la Yesu Kristo uponyaji-Marko 16:18
- Jina la Yesu Kristo ni neema tosha-Yohana 14:13.
- Neno la Mungu ni ngao-Zaburi 91:4. Neno la Mungu upanga-Waefeso 6:17.
- Damu ya Kristo ni silaha juu ya nguvu za shetani-Zaburi 78:49; Ufunuo 12:11.
MALAIKA WA MUNGU WANAWALINDA WANA WA MUNGU.
- Mungu amewandaa malaika kutulinda.
- Elisha alijua kwamba analindwa na nguvu za Mungu-Zaburi 34:7.
- Nguvu za moto na winguiliwalinda na kukwaongoza wana wa Israeli jangwani.
- Balaamu alisimamishwa na malaika, Gideoni na Eliya walifahamu ulinzi wa Mungu.
- Usiogope-2 Wafalme 6:16 walio pamoja nasi ni wengi kuliko walio nao-Ufunuo 12:4; Danieli 8:10.
- Mungu ni kimbilio-Zaburi 121:4; Zaburi 91:5-11.
Mungu alitumia giza ya upofu juu ya adui wa Elisha.
- Mfalme wa Israeli Jehotam (849-842BC) aliona ulinzi wa Mungu.
MWISHO
- Je, ni vita gani wewe unapitia leo? Usiogope walio pamoja nawe na wengi.
- Kumbuka vita ni vyake Bwana-2 Mambo ya Nyakati 20:15.
- Paulo ametueleza sisi ni zaidi ya washindi-Warumi 8:37.
The following two tabs change content below. Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.