Categories: Swahili Service

WASAMARIA NI WATU PIA

MFULULIZO: SAFIRI NA MTUME YOHANA

SOMO: YOHANA 4:1-30

 

Katika somo letu leo tunaona mwanamke aliyeishi maisha ya mzunguko mzunguko, aliyekuwa katika mzunguko wa furaha yaani, ‘merry go-round’. Maisha yake yalikuwa yamechakaa lakini siku moja Yesu Kristo alikutana naye, katika kisima cha Yakobo karibu na mji wa Sikari. Yesu alipokutana na huyu mwanamke Msamaria, aliyafungua macho na kugundua kwamba kuna maisha mapya.

Maisha mapya ni huru kutoka, maisha ya kubeba mizigo, shida za maisha. Yesu alimwongoza mwanamke huyo kupata uzima na Amini maishani.

Leo kuna mtu amechoka na maisha ya dunia hii. Umechoka na merry-go-round ya maisha, umechoka na jinsi maisha yalivyo na unataka mabadiliko. Mapenzi ya Mwokozi hivi leo ni kila mmoja wetu apate kufikia maisha na uzima tele- Yohana 10:10.

Hebu tutazame:-

TAABU, UMASKINI NA HUZUNI ZA MSAMARIA- 4:1-18

  • Alikuwa mwanamke.
  • Wayahudi hawakuwa na heshima kwa wanawake (kama waislamu).
  • Wayahudi (wanaume) waliamini afadhali mbwa kuliko mwanamke.
  • Myahudi alipoamka asubuhi alisema, “ninakushukuru Mwenyezi Mungu haukuniumba mwanamke!!”
  • Alikuwa msamaria.
  • Wasamaria walikuwa wakosa kabila (outcasts) walikuwa kama waswahili maana walikuwa uzao na mchanganyiko wa Wayahudi na na watu wa mataifa.
  • Walichukiwa sana kiasi hawangeweza kuingia hekaluni, hivyo walibuni dini yao.
  • Alikuwa mwanamke mwenye dhambi.
  • Alichukiwa na watu wote na zaidi wanawake wenzake walimchukia.

Taabu ya kutengwa- V.6

  • Wanawake wa kawaida aalienda kuchota maji katika kisima cha Yakobo asubuhi mapema.
  • Huyu mwanamke anachota maji saa sita!!
  • Kutoka mjini Sikari ilikuwa kilomita mbili.
  • Kubeba maji wakati jua ni kali ilikuwa ngumu- lakini alienda pekee kwa kutengwa na wanawake.
  • Kwa nini huyu mwanamke alitaabika hivi- V. 17- 18 na V. 28 alikuwa mwanamke wa ujuzi mwingi sana.
  • Wanaume alioishi nao pengine walikuwa waume wa hawa wanawake.
  • Wanawake walimtenga, bali walimsema.
  • Hata alipookoka hakwenda kuwaeleza wanawake wenzake, bali aliwaendea wanaume!!- V. 28.
  • Uma ulimtenga kwa mbali sana.
  • Mwanamke msamaria ni picha ya kila mtu bado kuokoka. Huyu hana uhusiano na Mungu wa Mbinguni.
  • Katika mazungumzo na Yesu Kristo, mwanamke msamaria alimwambia Yesu kuwa ametengana na Mungu pia- V. 20-22.
  • Ibada ndogo aliyoifanyia Mungu haikutosha, alitengwa kiroho- Isaya 59:1-2.
  • Hii ni taabu kubwa kutoomba, kutoabudu na kukosa ushirika na Mungu ni maisha duni sana.
  • Watu waliotengwa wako katika hali mbaya, wanaomba lakini Mungu hasikilizi- Zaburi 66:18.
  • Watu bila wokovu wanaenda kanisani lakini hawawezi kuabudu katika kweli na katika Roho!!

Taabu ya kutojua kweli- V. 7- 26.

  • Huyu mwanamke alitaka na kumjadili Yesu Kristo juu ya dini.
  • Kwanza alimwona Yesu Kristo kama mtu Myahudi wa kawaida- V. 9, 11-12; 15.
  • Mwanamke msamaria alileta maneno ya dini, ili shida yake isionekane- V. 16-18.
  • Yesu Kristo alimwambia mwanamke msamaria kwamba hajui hajui- V. 10.
  • Usichojua kinaweza kukupeleka jehanamu- Waefeso 2:8-9.

Taabu ya kutofautiana kwake- V. 11-26.

  • Mwanamke msamaria aliishi dhambini- V.16-18, lakini anafikiri anaweza mjadili Kristo- unafiki!!
  • Pamoja na mijadala yetu, Mungu anasema, njia ni moja kwenda mbinguni- Yohana 14:6; Matendo 4:12; Matendo 16:31.
  • Mungu amesema kwa Matendo, hatuwezi kumfikia Mungu- Waefeso 2:8-9; Tito 3:5.
  • Wewe na mimi ni nani kubishana na Mungu?- Warumi 9:20.

MWOKOZI ASIYE NA KIFANI

V 4- asiye na kifani kwa neema yake.

  • Ilimpasa kupitia Samaria.
  • Wayahudi wengi walipita njia ndefu wasipite Samaria.
  • Wayahudi waliwachukia sana Wasamaria.
  • Lakini Yesu Kristo si kama mwanadamu- ni wa neema nyingi sana.
  • Mshukuru Mungu, wakati alikupitia! Neema ya Mungu inatupitia!!

Yesu Kristo hana kifani katika subira yake- V. 7-26.

  • Kwa subira nyingi Yesu Kristo alitumia wakati mwingi na huyu mwanamke.
  • Yesu Kristo anatukuta mahali tulipo na kutuendeleza kwa wokovu wake- Ufunuo 3:20.

Yesu Kristo hana kifani kwa vipawa vyake- V. 10-14.

  • Yesu Kristo alimwambia mwanamke msamaria atampa maji ya uzima.
  • Yesu Kristo alimwahidi kwamba kama atakunywa maji ya uzima hatapata kiu tena.
  • Huyu mwanamke alikuwa amejaribu njia zote kupata amani na raha kujitosheleza matarajio na mapenzi ya moyo wake, bila kutosheka.
  • Moyo wake ulikuwa tupu na wenye kiu.
  • Tendo la ndoa halikuweza, ndoa ilikuwa imevunjika.
  • Watu hawakumpa furaha na amani.
  • Sasa Mwokozi Yesu Kristo amempa alichotafuta maisha yake yote.
  • Yesu Kristo amemwahidi safari moja ya kunywa maji ya uzima inatosha.
  • Yesu Kristo hawezi kulinganishwa na yeyote yule.
  • Tunapomjia Kristo, tunapata yote ndani ya yote.

WOKOVU WA AJABU

Kulikuwa na mabadiliko ya ajabu katika shughuli zake- V.28, 2 Wakorintho 5:17.

Kulikuwa na mabadiliko katika njia zake-Vs. 28-29.

  • Huyu mwanamke alienda zake kuwaeleza wanaume habari za Yesu Kristo.
  • Kwa nini wanaume? Maana aliwajua wote.
  • Wanawake walimchukia lakini wanaume walimpenda sana.
  • Ikiwa wokovu ni sahihi kutakuwa na mabadiliko mengi katika maisha.

Kulikuwa na mabadiliko juu ya kumtambua Yesu Kristo.

  • 9 alimwona Yesu kama “Myahudi.”
  • 11 alimwita Yesu Bwana (sir).
  • 19 alimwona Yesu kama “nabii.”
  • 29 alimwita Yesu Kristo Masihi.
  • Alimwona Yesu Kristo kama utoshelevu wa mwoyo wake.
  • Ikiwa utapata kuokoka lazima ufike mahali pa kuelewa Yesu ndiye tumaini pekee-Matendo 4:12.

MWISHO

  • Je, umeokoka? Je, umefika mahali katika maisha yako unapo mtegemea Yesu Kristo pekee kwa wokovu wako?
  • Leo mjie Yesu Kristo kwa moyo wako wote utapata kuokoka.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Rev, DR. Willy Mutiso

Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Recent Posts

MSAADA WA MUNGU WAKATI WA MATESO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: ZABURI 46:1.   Biblia inatuakikishia kwamba Mungu wetu ni “Msaada…

3 weeks ago

GOD GUIDES OUR DESTINIES.

SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: PROVERBS 3:5-6.   Every destiny is a divine…

3 weeks ago

PUT OFF AND PUT ON

SERIES: THROUGH THE BOOK OF COLOSSIANS. TEXT: Colossians 3:5-10   We have put off the…

3 weeks ago

GOD OF THE BREAKTHROUGHS

SERIES: THE GOD WE SERVE TEXT: 2nd SAMUEL 5:17-20   Breakthroughs are divine interventions that…

4 weeks ago

WHO IS SPEAKING TO YOU?

SERIES: DRAWING NEAR TO GOD TEXT: LAMENTATIONS 3:37 It reminds believers that God's word alone…

1 month ago

CHECHEA MSHINDI ALIYE NDANI YAKO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: 1 YOHANA 5:4.   Wakristo wengi wanaishi maisha ya kushindwa…

1 month ago