Categories: Swahili Service

WATU WAMJUAO MUNGU WAO

MFULULIZO: DANIELI-MUNGU NDIYE HAKIMU.

SOMO: DANIELI 11:1-45 (30-35), 32.

 

Danieli 11 ni sura ya ajabu katika kitabu cha Danieli. Vifungu 1-35 vilikuwa wakati ujao kwa Danieli, lakini ni historia kwetu leo. Vifungu vya 36-45 vilikuwa wakati ujao kwa Danieli na pia kwetu leo. Leo tunataka kutizama Maanake vifungu hivi 30-45 na kuelewa hasa maana yake kwetu na jinsi ya kutekeleza juu ya maisha yetu leo.

Mungu ametuita kila mmoja wetu kuwa shujaa hodari. Ametuita tuwe watu wamjuao Mungu wao, watu hodari, watu wafanyao mambo makuu. Mashujaa hodari wanafanyika Tunapofanya uamuzi. Je, wewe umeamua kuwa hodari na shujaa, anayemjua Mungu wake, hodari na anayefanya mambo makuu?

Watu wa Mungu ni hodari na wanafanya mambo makuu-Vs. 22. Katika kifungu hiki tunasoma mambo matatu-

  1. Sasa ndiyo wakati.
  2. Mahali ndio hapa.
  3. Sisi FBC-Athi river ndio watu wale

Wakati ndio huu; katika historia Mungu anawatafuta watu watakao tekeleza mpango wake.

  • Mungu alipohitaji kuwa na rafiki alimchagua Ibrahimu.
  • Mungu alipohitaji Mkombozi alimchagua Musa.
  • Mungu alipohitaji watu wake, aliwaita Israeli.
  • Mungu alipohitaji kiongozi atakayemwamini alimwita Yoshua.
  • Mungu alipohitaji Mwokozi wa ulimwengu alimtuma Yesu Krsito.
  • Mungu alipohitaji shahidi aliita kanisa lake (FBC-Athi). Huu ndio wakati wetu.
  • Huu ndio wakati wetu-Matendo 2:17.
  • Sisi ndio watu hodari watakaofanya mambo makuu-1 Petro 2:9.
  • Hebu tuone jinsi ya kuwa na nguvu za kufanya mambo makuu.

KUMJUA MUNGU.

  • Je, Maanake kumjua Mungu ni nini?
  • Watu wengi wanasema wanamjua Mungu, lakini wanamjua kwa jina pekee.
  • Haitoshi kumjua Mungu kwa jina. Mungu anapenda tumjue kibinafsi-Warumi 10:1-10.
  • Tunamjua Mungu kibinafsi kupitia Bwana Yesu Kristo-Yohana 1:6-7.
  • Pamoja na kumjua Mungu ni lazima tuendelee kumfahamu zaidi na zaidi kila saa, kila siku:-
  1. Tunamjua Mungu tunaposhirikiana naye, tunapotumia wakati katika ushirika wa binafsi.
  • Henoko alitembea na Mungu kwa karibu-Mwanzo 5:22-24.
  • Henoko alienda pamoja na Mungu, mpaka Henoko akatoweka, maana Mungu alimtwaa.
  1. Tunamjua Mungu kwa kumsikiliza anenapo nasi kama jinsi Mariamu dadake Martha.
  2. Tunamjua Mungu kwa kunena naye-Zaburi 55:16-17.
  3. Tunamjua Mungu kwa kutazama njia zake za utendaji-2 Petro 3:18.
  4. Tunamjua Mungu tunaposhirikiana naye na watu wake-Waebrania 3:12-14.
  • Kumjua Mungu ndicho kiini hasa cha kuwa hodari na kufanya mambo makuu.

KUWA HODARI.

  • Jinsi tumjuaye Mungu ndivyo tutakuwa hodari.
  • Tutakuwa hodari mwili, roho, nafsi na utakatifu-Waefeso 6:10-12.
  • Jinsi tumjuavyo Mungu wetu ndivyo:-
  1. Tutakuwa hodari na wajasiri ndani yake.
  • Tutajaa uhakika wa kiroho, tutakuwa wajasiri katika vita vya kiroho-Warumi 8:33-39.
  1. Tutakuwa hodari na wenye nguvu kushinda majaribu na maovu.
  • Yusufu alikuwa hodari juu ya majaribu, alimwogopa Mungu wake-Mwanzo 39:7-14.
  1. Tutakuwa hodari kuwafariji wenzetu wakati wa shida na majaribu. Tutakuwa watu wa kutegemewa na wote wenye shaka na dhaifu-Isaya 40:28-31.

WATAFANYA MAMBO MAKUU.

  • Mambo makuu (exploits) ni mambo hodari.
  • Gideoni alifanya mambo makuu, akiwa na watu 300-(Waamuzi 7:19-23).
  • Samsoni alifanya mambo makuu sana-Waamuzi 14:5-6.
  • Eliya alifanya mambo makuu mlimani Karmeli-1 Wafalme 18:36-39.
  • Walifanya mambo makuu katika Waebrania 11.
  • Wanafunzi na mitume wa Yesu Kristo walifanya mambo makuu-Matendo 15:26; 17:6.
  • Tutafanya mambo makuu kupitia maombi na shuhuda zetu-Yakobo 5:17-18.
  • Mambo makuu yanafanyika kupitia-
  1. Upendo
  2. Utii
  3. Unyenyekevu
  4. Kujikana
  5. Kanuni za kumsimamia Mungu wao.

MWISHO

  • Mungu anapenda ajulikane wa watu wake.
  • Kutomjua Mungu ni hatari sana-Mathayo 7:21-23.
  • Tukimjua Mungu tutakuwa hodari na tutafanya mambo makuu.
  • Kufanya mambo makuu kwa wengine wetu ni-
  1. Kustahimili wakati unajisikia kujiuzulu.
  2. Kukaa katika ndoa yako kuliko kutalaki.
  3. Kutembea maili ya pili na watoto wako kuliko kutupa mbao.
  4. Kusimama wima na kungojea uponyaji wako wakati daktari amesema vingine.
  5. Kumjua Mungu kutatusaidia kwenda mbali zaidi ya nguvu za mwanadamu.
  • Kufaulu katika Ukristo wako ni njia moja pekee “Kumjua Mungu wako.”
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Rev, DR. Willy Mutiso

Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Recent Posts

MSAADA WA MUNGU WAKATI WA MATESO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: ZABURI 46:1.   Biblia inatuakikishia kwamba Mungu wetu ni “Msaada…

2 weeks ago

GOD GUIDES OUR DESTINIES.

SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: PROVERBS 3:5-6.   Every destiny is a divine…

2 weeks ago

PUT OFF AND PUT ON

SERIES: THROUGH THE BOOK OF COLOSSIANS. TEXT: Colossians 3:5-10   We have put off the…

2 weeks ago

GOD OF THE BREAKTHROUGHS

SERIES: THE GOD WE SERVE TEXT: 2nd SAMUEL 5:17-20   Breakthroughs are divine interventions that…

4 weeks ago

WHO IS SPEAKING TO YOU?

SERIES: DRAWING NEAR TO GOD TEXT: LAMENTATIONS 3:37 It reminds believers that God's word alone…

1 month ago

CHECHEA MSHINDI ALIYE NDANI YAKO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: 1 YOHANA 5:4.   Wakristo wengi wanaishi maisha ya kushindwa…

1 month ago