SOMO: UFUNUO 15:3-4; ISAYA 51:11
Ujumbe wa leo ni swali hili, Je, wewe unaweza kuimba wimbo wa Musa na wimbo wa Mwana kondoo? Historia ya Biblia inatufunulia kwamba Yakobo alihama toka nchini Kanaani na kuingia nchi ya Misri kutafuta chakula. Baada ya wana wa Israeli kustawi huko Misri waliishia kuwa watumwa Misri kwa miaka 400. Je, ni kwa nini Mungu aliwaacha mle Misri muda huo mrefu hivyo?
Isaya 51:11, “Nao waliokombolewa na Bwana watarejea, watafika Sayuni wakiimba, furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao; watapata shangwe na furaha, huzuni na kuugua zitakimbia.”
Hapa Biblia inataja wimbo wa Musa. Katika ujumbe wetu hivi leo tunapenda kuelewa ni nini wimbo wa Musa? Je, wimbo wa Musa unaimbwa lini? Je, ni nani anastahili kuimba wimbo wa Musa?
Katika Kutoka 15:1-19, tunapata maneno yote ya wimbo wa Musa. Je, unaweza kuimba wimbo huu?
Katika Mwanzo 46:5-7, tunaona unabii wa wimbo wa Musa. Pia katika Mwanzo 15:12-15, Mungu alimpa Ibrahimu unabii wa yatakayojiri juu ya wana wa Israeli.
Je, kwa nini Mungu aliruhusu mbegu ya Ibrahimu kupitia utumwa huu na kwa kiasi hicho?
Sababu zake:-
- Mungu alipenda kutupatia picha kwamba wote wanaotembea kwenda mbinguni ni lazima kwanza wawe wageni na wasafiri hapa duniani. Mtu asipopita katika utumwa hawezi kuelewa na uhuru na ukombozi.
- Wasafiri wa kwenda mbinguni lazima kupitia Misri. Misri maanake ni ulimwengu, kila atakaye okoka sharti kuacha Misri.
- Wamisri watatudhiaki sisi tukiendelea kuishi Misri. Tukiendelea kuishi hapa duniani na kucheza wimbo wake tutaendelea kuteseka.
- Mungu alipenda watu wake wapitie wakati wa jaribu. Hebu tuone:-
SHULE ZA MUNGU.
- Mungu anazo shule kadhaa ambazo watoto wake sharti wapitie mpaka wapite mitihani yao.
- Wengi wetu tunapitia katika shule za Mungu bila kuelewa kinacho tendeka maishani.
- Shule ya tabia nzuri na nidhamu:
- Huenda Mungu anakupitishia shule hii sasa hivi.
- Shule ya tabia na nidhamu ni lazima kwa watoto wa Mungu.
- Mpaka mimi na wewe kupitia shule hii na kupita mitihani yake.
- Mungu hawezi kukuachilia kwenda mbele na kukupandisha bila wewe kupitia na kuhitimu shule na mitihani yake.
- Shule ya unyenyekevu.
- Mungu anapoona kwamba umekosa unyenyekevu atakufanya ufanye kazi chini ya watu ambao ni wadogo wako.
- Mpaka wewe ujifunze kanuni za kunyenyekea.
- Ukakuwa ukisema, “Je, Mungu wangu, kwa nini nitawaliwe na wadogo wangu, na watoto wangu na watu wa umri wa chini?
- Mpaka utakapojifunza kunyenyekea, Mungu atakwambia sasa umenyenyekea, umehitimu.
- Shule ya kiasi.
- Wengine wetu tumekosa kuwa na kiasi mpaka maisha yetu yamekosa udhabiti.
- Tamaa mbaya, ulafi, ulevi zinafanya maisha ya mtu kukosa kiasi-Waefeso 4:17-32.
- Shule ya maombi.
- Wengine, Mungu anawapitisha shule ya maombi na kuwapa maombi ya kuomba. Mpaka kupita mitihani ya kuomba.
- Shule ya kufunga saumu.
- Mungu anapitisha watu wengine kwa shule ya kufunga saumu.
- Watu ambao Mungu aliwabarikia zamani na pesa, lakini watazitumia kwa anasa, sasa hawana kitu.
- Mungu anawasomesha somo kwamba, “Nitakapokupa pesa tena utaelewa jinsi ya kuzitumia.”
- Yesu Kristo mwenyewe alipitia shule ya utii, hata ingawa alikuwa Mungu mwenyewe.
Watu wengi hawawezi kuimba wimbo wa Musa leo kwa sababu wangali huko Misri.
- Wimbo wa Musa ni wimbo wa washindi.
- Ushindi juu ya watesi, juu ya utumwa, juu ya kutumiwa vibaya.
- Ushindi juu ya umaskini, juu ya wanao sumbua wengine, juu ya wanao kwandama katika maisha yako.
- Ushindi wa kuweza kuona adui zako wakizama maji ya bahari katika bahari ya Shamu-Wimbo wa Musa.
- Mtu hawezi kuimba wimbo wa Musa bila kuwa mshindi.
- Wimbo wa Musa ni wimbo wa wale walio zaidi ya washindi-Warumi 8:37-39.
- Kristo hapendi yeyote aishi katika utumwa wowote.
- Unapoona ya kwamba adui na watesi wako hawako tayari kukufungulia lazima kutumia mbinu za Musa. Tuma kwa tauni na magonjwa juu yao na jamaa zao, zamisha adui zako katika bahari ya mauti. Ndivyo wimbo wa Musa utakuwa wimbo wako!!
WIMBO WA KWANZA NA WIMBO WA MWISHO WA USHINDI.
- Unaweza kuitimu kuimba wimbo wa Musa.
- Huu wimbo wa Musa ni ushindi wa kwanza.
- Ushindi wa kwanza ni ushindi juu ya shetani na juu ya mwili.
- Lakini ushindi juu ya shetani na juu ya mwili sio ushindi kamili.
- Ushindi ulio bora zaidi ni kuimba wimbo wa mwisho.
JE, NI NINI WIMBO WA MWANA KONDOO?-Ufunuo 15:3-4.
“Nao waliimba wimbo wa Musa mtumishi wa Mungu, na wimbo wa Mwana kondoo wakisema ni makuu na ya ajabu Matendo yako. Eh Bwana, Mwenyezi, ni za haki na za kweli njia zako; Ee mfalme wa mataifa. Ni nani asiyekucha, Ee Bwana, na kulitukuza jina lako? Kwa kuwa we peke yako u mtakatifu, kwa maana mataifa yote watakuja na kusujudu mbele zako; kwa kuwa Matendo yako ya haki yamekwisha kufunguliwa.”
- Wimbo wa Mwana kondoo ni wimbo wa waliokombolewa watakapofika mbinguni.
- Kwanza tutaimba wimbo wa Musa kisha wimbo wa Mwana kondoo.
- Kila mmoja atakayefika mbinguni lazima kuimba wimbo wa Musa na wimbo wa Mwana kondoo.
- Lazima tutumie talanta zetu za kuimba hapa duniani kisha huko mbinguni.
- Huwezi kuimba wimbo wa Musa na wimbo wa Mwana kondoo bila kuokoka. Baada ya kuokoka lazima kutembea na Yesu Kristo mpaka mwisho wa dahari.
- Wakristo wengi wa siku hizi wamekataa kutoa ushuhuda wao mbele za watu, wamekataa kuitwa majina kwa sababu ya wokovu wao.
- Kukata ushuhuda ni kukata kuimba wimbo wa Musa na wimbo wa Mwana kondoo.
MAOMBI
- Kila kusononeka na kilio, toweka kutoka kwangu katika jina la Yesu Kristo.
- Kila nguvu za giza zinazofanya kazi kinyume changu na ushindi wangu, achilia sasa katika jina la Yesu Kristo.
- Nitatangaza gurumo na radi ya Mungu juu ya adui zangu-katika jina la Yesu Kristo.
- Ninajifungua kutoka kwa utumwa wa dhambi, uchawi na urogi katika jina la Yesu Kristo.
- Bwana wangu, nina kushukuru kwa ushindi-katika jina la Yesu Kristo.
