MFULULIZO: TUMAINI HAI.
SOMO: 1 PETRO 1:10-12.
Mtume Petro amekubali kwamba wakristo wa kwanza wametawanyika pote wakihofia maisha yao. Hawa Wakristo amewahimiza kwamba wakafurahi sana hata katika mateso. Amewaeleza kwamba wamepata urithi mkuu katika Kristo. Mateso ni kwa muda mfupi tu, tukilinganisha na urithi tuliopata katika Yesu Kristo.
Petro amewapongeza sana kwamba hata ingawa hawakumwona Kristo katika siku zake mwili na hata ingawa sasa hawamuoni bali wanampenda sana. Kule kumwamini Mungu ambaye hatumwoni kunatuzalia wokovu.
Hivyo kuishi tumaini hai na kuwa na hakika juu ya wokovu ndio wazo kuu katika sura ya kwanza ya Petro.
Petro amewaonyesha kwamba kiini hasa cha wokovu ni Yesu Kristo pekee. Wokovu unatupa raha.
Sasa Petro anatueleza ukuu wa wokovu tuliopewa.
Isaya 43:11, “Mimi, naam mimi ni Bwana zaidi yangu mimi hapana Mwokozi.”
- Wokovu ni neno la ajabu, wokovu ni kitu cha ajabu sana.
- Mungu kupitia kwa nabii Isaya anaazimia kwamba, hakuna Mwokozi mwingine isipokuwa yeye.
- Wokovu unaitajika na kila mwanadamu kwa sababu ya shida yetu-dhambi.
- Wote wamepotea, wote wamekufa, wote hawajiwezi na kwa kawaida sisi sote ni maadui wa Mungu na wote ni watoto na hasira ya Mungu-Warumi 3:22; Waefeso 2:1-4.
- Huenda daktari wa dawa anaweza kukutibu, mshauri anaweza kukusaidia kwa shida zako, polisi pengine akukinge na adui, lakini Mungu pekee ni Mwokozi-Kutoka 34:6.
- Jambo la kwanza linalofanya wokovu wetu kuwa mkuu ni kwamba wokovu unatoka mahali moja na Mungu moja!!
- Wokovu wetu ni mkuu kwa maana ulinunuliwa kwa bei ya juu zaidi-Damu ya Yesu Kristo-Isaya 43:11. Hebu tutazame:-
MANABII WALITAFUTA-TAFUTA NA KUCHUNGUZA-CHUNGUZA-1 Petro 1:10.
- Wokovu unatoka kwa Mungu ndio wazo kuu ya Biblia yote-(Mwanzo-Ufunuo).
- Paulo anamweleza Timotheo kwamba hekima ya Mungu inawaongoza watu kuokoka, kupitia kwa imani ndani ya Yesu Kristo-2 Timotheo 3:15.
- Yesu Kristo alipotoka jangwani kujaribiwa na ibilisi alifika Nazareti akasoma Isaya-Luka 4:18-19; Isaya 61:1-2 juu ya kazi yake Mwokozi.
- Wokovu na ukombozi ndicho kiini cha Biblia yote-Mwanzo 3:15; Waebrania 1:1.
- Manabii wote waliubiri habari za kuzaliwa, huduma, kufa na kufufuka kwa Yesu Kristo, yaani Injili.
- Lakini manabii na Agano la Kale hawakuelewa hasa jinsi huu wokovu utakuja duniani, lakini walitafuta-tafuta na kuchungulia-chungulia kutoka mbali!!
- Kwa kweli manabii walijua Mkombozi wa ulimwengu yuaja lakini hawakujua kwa njia gani na ni lini-Isaya 60:1-3.
- Ayubu alijua Mkombozi na Mteteaji wetu yu hai asijue ni lini-Ayubu 19:24-26.
- Lakini sisi tumepata Ufunuo wote, kwa sababu sisi tuko na Agano la Kale na Agano Jipya!!
ROHO MTAKATIFU ALITABIRI WOKOVU-1 Petro 1:11.
- Unabii wa Agano la Kale ulikuja kwa Roho Mtakatifu-2 Timotheo 3:16-17.
- Petro naye anakiri mtume Paulo juu ya kazi na huduma ya Roho Mtakatifu juu ya unbii-2 Petro 1:21.
- Petro anamwita Roho Mtakatifu, “Roho wa Kristo aliye kuwa ndani yao.”
- Hatuwezi kamwe kutenga “Kristo wa milele” na Mungu Baba na Mungu Roho Mtakatifu-Kumbukumbu 6:4.
- Yesu Kristo mwenyewe alijitabiri-Zaburi 22:14-18; Isaya 53:4-6; Danieli 7:13-14; Zakaria 2:10-13.
- Wokovu huu tuliopokea ni ajabu, umetufikia kutoka mbali sana.
- Watakatifu wa kale walihesabiwa haki kwa ajili ya imani yao katika Mwokozi aliyetabiriwa-Ayubu 19:25.
- Msalaba wa Yesu Kristo ndio Hinge ya historia na ukombozi (B.C/A.D).
WOKOVU ULIHUBIRIWA NA MITUME-1 Petro 1:12.
- Petro mtume ndiye wa kwanza kabisa kuhubiri Injili katika Agano Jipya, katika siku ya Pentekoste.
- Mhubiri ya Mtume Petro siku ya Pentekoste yalikuwa kwa uwezo na nguvu za Roho Mtakatifu.
- Baadaye mitume wengine kama Paulo, Timotheo, Sila, Filipo, Yohana, Yakobo na wenzao waliendelea kuhubiri Injili ya wokovu.
MALAIKA WANATAMANI KUCHUNGULIA WOKOVU-1 Petro 1:12.
- Katika Zaburi 104:4, “Malaika ni upepo na miali ya moto.”
- Malaika ni wa haina mbalimbali, ni Watakatifu.
- Malaika wa mbinguni wanashangaa wokovu na jinsi tulivyo wanadamu.
- Malaika wanashangaa mambo ya wokovu.
- Malaika na pia daimoni hawawezi kuokoka, hivyo hawaelewi na ukombozi.
- Lakini hata ingawa hivyo, malaika wanapenda sana kuelewa maana ya ukombozi-Ufunuo 5:7-12.
- Malaika wamekuwa shahidi wa mpango wa Mungu wa ukombozi tangu jadi.
- Malaika wanahudumia wale walio warithi wa wokovu-Waebrania 1:14.
- Malaika watajiunga pamoja nasi kumsifu Mungu mbinguni.
- Kwa sababu malaika hawana mwili hawatuelewi, lakini wanashangaa mbingu yote inashughulikia mwanadamu.
- Malaika hawakuumbwa na umbo, sura na chapa ya Mungu kama jinsi mwanadamu.
- Yesu Kristo hakuwafia malaika walioasi, hivyo shetani na mapepo hawawezi kuokoka.
- Wokovu na ukombozi ni mkuu, gharama zake ni kuu, damu ya Yesu Kristo.
MWISHO
- Haijalishi kinachofanyika ndani ya maisha yako, Mungu amekupenda kiasi Yesu akafa kwa ajili yako!
- Haijalishi mateso yako leo na kesho, Mungu amelipa deni yako yote, sasa umealikwa kusimama mbele za Mungu pamoja na wingi wa malaika na Watakatifu wote mbinguni milele na milele.
- Milele na milele tutaimba wimbo wa Musa na wimbo wa mwana kondoo.
- Je, wewe utakuwako? Sharti uokoke!!
The following two tabs change content below. Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.