YEHORAMU– ALIFARIKI BILA KUTAMANIWA.

2 MAMBO YA NYAKATI 21:1-20

UTANGULIZI

Tunapotembea katika barabara ya maisha, tunaendelea kuandika historia ya jinsi tutakumbukwa mara tutakapo fariki dunia. Tabia zetu ndizo watu watakumbuka. Mfalme Yehoramu mwana wa mfalme Yehoshafati alifariki bila kutamaniwa na kuliliwa na mtu yeyote. Kama Yesu Kristo atakawia zaidi kurundi kwake duniani, Kila mmoja wetu katika chumba hiki lazima kukutana na mauti. Tangu kuzaliwa tunaanza kutembea kuelekea siku ya kufa

Kila mtu anapenda kukumbukwa na kuliliwa na watu wake. Hebu tuone kifo cha mfalme Yehoramu aliyefariki bila yeyote kumtamani:-

I.  ALIFARIKI BILA KUTAMANIWA

  1. Mkristo wa kweli anapofariki mawazo yanakuwa mawilili, kwanza tunafurahi maana anaenda mbinguni kwa Baba. Lakini pia tunalia maana ameacha pengo nyumbani, jamii, kanisa na uma.
  2. Mithali 10.7 “kuwakumbuka wenye haki huwa na Baraka bali jina la mtu mwovu litaoza”
  3. Mtu mzuri anapokufa bila Yesu Kristo tunahuzunika sana maana huyu ameenda kuzimu, na kukaa milele bila Mungu. Mtu mbaya anapokufa tunapenda kuangazia matendo yake yaliyokuwa mema na hatutaki kutaja mabaya yake.
  4. Yehoramu alipofariki hakuna aliyejali na hakuna aliye mlilia
  5. 2 Mambo ya Nyakati 21:18-20 – “Mungu alimpiga matumbo kwa ugojwa usiyeponyeka. Baada ya miaka mwili Yehoramu alikufa katika kuugua vibaya.
  • Watu wake hawakumwakishia moto, kama walivyomfanyia Yehoshafati, Asa na Daudi baba zake
  • Yehoramu alikuwa miaka 40 alipofariki
  • Hakuna yeyote alimwomboleza, kumlilia na kumtamini Yehoramu
  • Mazishi yake haikutambulika katika makaburi ya wafalme wa Yuda. Walimtenga hata katika mauti.
  1. Howard Hughes alikufa na kuacha $ 2.5billion
  • Alikuwa tajiri zaidi katika America, alikuwa na kampuni yake pekee ya ndege, mahoteli yake yangaliko duniani, casino zake zinajulikana. Alipokufa ni mtu moja wa ukoo alitokea alikuwa mtoto wa mjomba yaani cousin. Watu wa kasino pekee ndio walitulia kwa dakika moja kumkumbuka.
  • Alizikwa na nyumba mauti – funeral home (13/12/1976)
  1. Kufariki bila kuombolezwa, bila watu kujali ni jambo mbaya zaidi.
  2. Mfalme Napoleoni Bonaparte, katika utawala wake ufaranza watu 500,000 walikufa katika vita.
  • Alipoenda uamisho wa Uingereza pale kisiwa cha St. Helena – mke akamwacha (Marie Louise). Akaolewa na Bwana mwingine.
  • Mtoto wake wa kiume hakumwandikia barua
  • Kaburi yake kumeandikwa “hapa amelala”
  • Kwa nini Yehoramu alifariki bila kutamaniwa?

II.  YEHORAMU ALIISHI VIBAYA

  1. Aliishi maisha maovu
  2. 2 Mambo ya Nyakati 21:4 – aliwaua nduguze wote kwa upanga na baadhi ya viongozi wa Israeli
  3. 2 M. Nyokati 21:6 – ali mwoa binti yake Ahabu. Athalia mwanaume mwovu zaidi
  4. (21:10) Yehoramu alimwacha Bwana Mungu wa baba zake
  5. (21:11) aliwaelekeza watu wa Yerusalemu na Yuda katika dhambi ya uasherati
  6. Mungu adhiakiwi (Wagalatia 6:7)
  7. Panda wazo utavuna tendo, panda tendo utavuna mazoea, panda mazoea utavuna tabia, panda tabia utavuna hatima na maisha (Samuel smiles 1812)
  8. Yehoramu alijiishia binafsi, alikufa pekee yake. Luke 12:19-20
  9. Yehoramu aliishi bila Mungu, akafariki bila Mungu (Mithali 13:9)

III. BASI SISI NASI TUISHI AJE?

I Yohana 1:9, Wagalaha 2:20, Warumi 14:7-8, wafilipi 1:20

  1. Andika jina lako juu ya maisha ya watu si juu ya mawe.
  2. Anayeishi maisha matakatifu zaidi ndiye anafaa zaidi kufa. (Wafilipi 1:21)

 

MWISHO

  • Yehoramu aliishi na kufariki bila kutaminiwa na watu wote
  • Unavyoishi ndivyo utakavyo fariki.

 

The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Rev, DR. Willy Mutiso

Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Recent Posts

MSAADA WA MUNGU WAKATI WA MATESO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: ZABURI 46:1.   Biblia inatuakikishia kwamba Mungu wetu ni “Msaada…

2 weeks ago

GOD GUIDES OUR DESTINIES.

SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: PROVERBS 3:5-6.   Every destiny is a divine…

2 weeks ago

PUT OFF AND PUT ON

SERIES: THROUGH THE BOOK OF COLOSSIANS. TEXT: Colossians 3:5-10   We have put off the…

2 weeks ago

GOD OF THE BREAKTHROUGHS

SERIES: THE GOD WE SERVE TEXT: 2nd SAMUEL 5:17-20   Breakthroughs are divine interventions that…

3 weeks ago

WHO IS SPEAKING TO YOU?

SERIES: DRAWING NEAR TO GOD TEXT: LAMENTATIONS 3:37 It reminds believers that God's word alone…

4 weeks ago

CHECHEA MSHINDI ALIYE NDANI YAKO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: 1 YOHANA 5:4.   Wakristo wengi wanaishi maisha ya kushindwa…

1 month ago