YEHOSHAFATI ALIRUDI NYUMA

2 MAMBO YA NYAKATI 17-18

UTANGULIZI

Kubeba msalaba wote ni rahisi kuliko kubeba msalaba nusu. Mtu anayejaribu kuishi katika dunia mbili hupoteza zote mbili. Kwa wengi wetu, kama watu wa Mungu, ingesemekana kama jinsi watu wa      Galatia “mlikuwa mkipiga mbio vizuri, ni nani aliyewazuia msitii kweli?” (Wagalatia 5:7) “Enyi wagalatia msio na akili, ni nani aliyewaroga, nyini ambao Yesu Kristo aliwekwa wazi mbele ya Macho yenu yakuwa amesulubiwa?” Hata ingawa vizuizi ni vingi hakuna sababu wale wamepewa mambawa ya Imani waweze kuzuiwa katika maisha yao ya kiroho. Yehoshafati kama Asa baba yake alianza vizuri– lakini. Asubuhi ya maisha yake ilipata mawingu na mawimbi mengi hivyo Yehoshafati akaingia katika shida na kurudi nyuma. Maisha ya mfalme Yehoshafati ni funzo na onyo kwetu. Hebu tuone:-

I.  YEHOSHAFATI ALIHESHIMIKA SANA (17:3)

  • “Naye Bwana alikuwa pamoja na Yehoshafati”
  • Uwepo wa Bwana pamoja nasi ni hakikisho ya ushindi na utoshelevu.
  • Sababu ya Bwana kuwa na mfale Yehoshafati ni “Alikwenda katika njia za kwanza za Daudi babaye”
  • Njia za kwanza za Daudi na za babaye– Asa, zilikuwa siku nzuri za maisha yao.
  • Mioyo yao ilikuwa safi mbele za Mungu.
  • Siku zako nzuri ni siku zile umetembea na Mungu.
  • Asa aliambiwa na nabii Azaria “Bwana yu pamoja nanyi mkiwa pamoja naye” (II Mambo ya Nyakati 15:1-4)
  • Wale wanao mpa Mungu heshima, Mungu huwapa heshima. Wanao mdhihaki Mungu, wao hudhiakiwa.

II.  YEHOSHAFATI ALITIWA MOYO SANA KATIKA NJIA ZA BWANA (17:6)

  • Mfalme Uzzia alipokuwa na nguvu, moyo wake ulitukua hata akafanya maovu, akamwasi Bwana (26:16)
  • Kiburi kinapomuinua mtu kinamtoa mtu huyo kutoka kwa njia za Bwana.
  • Kumwacha Bwana ni kushindwa na pia ni mauti.
  • Mungu hatamwinua mtu mwenye kiburi, maana kiburi ni kinyume cha Mungu (Zaburi 37:4)

III.YEHOSHAFATI ALIFUNGWA NIRA MOJA NA WASIO AMINI. (18:1)

  • “Yehoshafati alikuwa na mali na heshima tele, akafanya ujama na mfalme Ahabu” (v.1)
  • Ahabu alijulikana sana kama adui wa Mungu.
  • Ahabu alimkasirisha Mungu zaidi kuliko wafalme wote wa Israeli (I Wafalme 16:33)
  • Pamoja na urafiki, kinachofuata ni ushirika hivyo Yehoshafati akashuka kwenda Samaria (18:2)
  • Ahabu wa dunia hii wako tayari kabisa kuwapokea watumishi wa Mungu wanao teremka chini.
  • Nehemia alipoalikwa na Tobia kuteremka chini wakutane, Nehemiah alisema siwezi (Nehemia 6:1-4)
  • Yesu Kristo alipokaa hapa duniani hakuwa na ushirika na dhambi (2 Wakorintho 6:14-18)

IV.  YEHOSHAFATI ALIJISALIMISHA KABISA KWA ADUI (18:3)

  • Yehoshafati alijitia nira shingoni
  • Tunauza uhuru wetu katika Bwana tunapokuwa watumwa wa mwnadamu.
  • Tunapo jifungisha nira moja na wasioamini, hatuwezi kumtumikia Mungu. Hatuwezi kuwahubiria wenye dhambi.
  • Aliyeokoka hawezi kuwa kama mtu aliyemgeni kwa neno la Mungu na kwa Roho mtakatifu (18:3)
  • Moja ni Bwana wenu , yaani Kristo yesu. Hatuwezi sema “mimi ni kama wewe” (18:3)

V.  YEHOSHAFATI KWA SIRI YA MOYO HAKUTOSHEKA (18:4-5)

  • Yehoshafati alipendekeza Mungu auliwe juu ya kwenda vitani (v.4)
  • Mara moja Ahabu aliwakusanya manabii wake 400.
  • Manabii wa uongo ni wengi sana kuliko nabii wa kweli. Wachungaji wa uongo ni wengi zaidi kuliko wale wa kweli.
  • Nabii wa Ahabu walikuwa na upako wa kuhubiri mambo yanayopendeza.
  • Wahubiri wanaopendeza wanadamu wana changia pakubwa kuendelesha dini na madhehebu, lakini hawawezi kamwe kutuliza mioyo inayoumia katika dhamabi.
  • Ahabu alichukia sana nabii Mikaya mwana wa Imla (18:7-27)

VI.  YEHOSHAFATI KWA AIBU NYINGI ALIPATIKANA (18:30-31)

  • Yehoshafati alimlilia Mungu na Mungu akamsaidia (v.30-31)
  • Ahabu aliuliwa katika vita hata ingawa alikuwa amejificha sana.
  • Kutoamini na kurudi nyuma kunatuacha bila nguvu mbele ya adui zetu.

 

MWISHO

  • Sauti za ushauri ni nyingi duniani– Je utasikiza nani?
  • Usifungwe nira moja na wasioamini.
  • Je, rafiki zako ni nani?
  • Roho ya uongo ni kama roho wa usharati maana zinasaliti.

 

The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Rev, DR. Willy Mutiso

Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Recent Posts

MSAADA WA MUNGU WAKATI WA MATESO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: ZABURI 46:1.   Biblia inatuakikishia kwamba Mungu wetu ni “Msaada…

2 weeks ago

GOD GUIDES OUR DESTINIES.

SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: PROVERBS 3:5-6.   Every destiny is a divine…

2 weeks ago

PUT OFF AND PUT ON

SERIES: THROUGH THE BOOK OF COLOSSIANS. TEXT: Colossians 3:5-10   We have put off the…

2 weeks ago

GOD OF THE BREAKTHROUGHS

SERIES: THE GOD WE SERVE TEXT: 2nd SAMUEL 5:17-20   Breakthroughs are divine interventions that…

4 weeks ago

WHO IS SPEAKING TO YOU?

SERIES: DRAWING NEAR TO GOD TEXT: LAMENTATIONS 3:37 It reminds believers that God's word alone…

1 month ago

CHECHEA MSHINDI ALIYE NDANI YAKO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: 1 YOHANA 5:4.   Wakristo wengi wanaishi maisha ya kushindwa…

1 month ago