Categories: Swahili Service

YESU KRISTO – MKATE WA UZIMA

MFULULIZO: SAFIRI NA MTUME YOHANA.

SOMO: YOHANA 6:22-35.

 

Sura hii ya sita inapofunguliwa tunampata Yesu Kristo akiwahubiri watu wengi, watu wenye njaa zaidi. Alipomaliza kuwahubiri walikuwa na njaa katika miili yao. Kwa mikate mitano na samaki wawili, Yesu Kristo aliwashibisha wanaume 5,000 na wanawake na watoto si haba. Mungu pekee ndiye anauwezo wa kufanya miujiza kubwa kama huu. Kwa jumla watu waliolishwa siku hio walikuwa zaidi ya watu 15,000. Watu hawa maelfu walikula na mabaki ya vikapu 12 zikabaki. Hii ilikuwa kikapu kimoja kwa kila mwanafunzi asiyesadiki!! Baada ya Yesu Kristo kutenda muujiza ule, aliwafundisha watu wote juu ya mkate ulio hai (mkate wa uzima).

Yesu Kristo ni mkate wa uzima. Mikate ni chakula cha watu walio wengi duniani kote. Afrika, Asia, Marekani, Amerika Kusini na Australia. Mkate ndio chakula pekee watu wanakula asubuhi, mchana na usiku (universal)!!

Yesu Kristo ni mkate wa uzima kwa watu wote wa dunia hii.

Yesu Kristo ndiye mahitaji ya dunia yote (the desire of all nations) mpenzi wa dunia yote ndiye Kristo (Ezra).

Mpaka leo hii Yesu Kristo ni mkate wa uzima kwa wote duniani. Hebu tutazame Yesu Kristo-mkate wa uzima:-

UTU WA MKATE WA MBINGUNI.

  1. Mkate wa mbinguni ni mtu-Yohana 6:34:35.
  • Mkate wa mbinguni si dini hau dhehebu bali ni mtu.
  • Hatuwezi kuokolewa na dini hau mpango, wokovu ni mtu-Yesu Kristo pekee-Matendo 4:12.
  1. Mkate wa mbinguni ni nguvu za Mungu-Vs. 35.
  • Mkate wa mbinguni ana nguvu ya kuokoa wenye dhambi wote.
  • Wote wanaomjia Kristo kwa njia ya imani wanapata kuokolewa.
  • Yesu Kristo anaahidi uzima, wokovu, salama na utoshelevu. Lakini wengine na dini zao wanaleta mauti-Mithali 16:25.
  1. Mkate wa mbinguni ni ahadi-Vs. 47-51.
  • Mkate wa mbinguni ni uzima.
  • Mkate wa dunia hii unaweza kutusaidia mwili na baadaye tunakufa.
  • Yesu Kristo ni mkate wa uzima wa milele.
  • Unapookolewa na Yesu Kristo unaishi milele daima.
  1. Mkate wa mbinguni una bei yake-Vs. 53-59.
  • Hili mwenye dhambi kufurahia mkate wa mbinguni ni lazima mwenye dhambi kumpokea Yesu Kristo-Isaya 55:1; Ufunuo 22:17.
  • Kuokoka ni kumpokea Yesu Kristo ndani ya maisha yako-Amini ndiye bei ya kuokoka (only believe).

KUPOKEA MKATE WA MBINGUNI-Yohana 6:1-13.

  1. Kristo aliwaonyesha watu jinsi ya kupokea uzima wa mbinguni- kwa njia ya miujiza mikate mitano na samaki wawili-1-13.
  • Yesu Kristo anatosha kwa wokovu wa kila mtu duniani.
  • Amewaokoa wengi duniani lakini bado kunao nafasi moja atakaye!!
  • Wokovu wa Yesu Kristo ni tele na kubaki-Vs. 13.
  1. Yesu Kristo aliwaeleza juu ya manna-Vs. 30-33.
  1. Manna ni chakula cha mbinguni. Manna ilikuwa mkate mdogo-Kutoka 16:14.
  • Hii manna ni picha ya unyenyekevu wa Yesu Kristo.
  • Kristo hakuzaliwa katika makao ya mfalme lakini katika hori ya ng’ombe.
  • Yesu Kristo kwa unyenyekevu alikuja duniani kuokoa wenye dhambi-Marko 8:20.
  1. Manna ilikuwa mviringo (round)-Kutoka 16:14.
  • Yesu Kristo ni wa milele na milele.
  • Yesu Kristo mwanzo wake si mle Bethlehemu-Yohana 1:1.
  1. Manna ilikuwa mkate mweupe-Kutoka 16:31.
  • Maanake ni utukufu wa Yesu Kristo.
  • Alizaliwa bila dhambi, aliishi bila dhambi, alikufa bila dhambi, Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu-1st Petro 2:22; 2 Wakorintho 5:21.
  1. Manna ilinyesha usiku-Kutoka 16:13-14.
  • Yesu alikuja kuwaokoa wenye dhambi katika giza ya dhambi zao.
  • Yesu Kristo ni nuru ya ulimwengu wa giza na mauti.
  1. Watu hawakuelewa manna.
  • Kutoka 16:15-waliita manna-maanake “hii ni nini?”
  • Watu wa kale hawakumwelewa Yesu Kristo.
  • Mpaka leo wanadamu hawamwelewi Mwokozi Yesu Kristo-Yohana 1:11-12; 10:20.
  • Hivi leo wengine wanasema Kristo ni nabii, mwalimu, mtu mwema!!
  • Lakini Kristo ni Mwokozi wa ulimwengu-Mungu wa milele.
  1. Manna ilikuwa chakula tosha kwa wote-Kutoka 16:17-18.
  • Yesu Kristo ni Mwokozi tosha.
  • Yesu anatosha kuokoa, kudumisha na kulinda.
  • Mungu aliwalisha mamilioni ya watu wa Israeli kila siku kwa miaka 40!!
  1. Manna ilikuwa tamu sana kwa ladha yake-Kutoka 16:31.
  • Manna ilikuwa mkate tamu na kushibisha.
  • Wanaompokea Yesu Kristo wanatoshelezwa maisha yao-Zaburi 34:8
  1. Manna ilikuwa chakula cha kusambaza-Kutoka 16:32.
  • Tunahitaji kuwaeleza wengi habari za Yesu Kristo, katika nguvu za Roho Matakatifu na kuacha matokeo mikononi mwa Mungu-2nd Timotheo 2:2.
  1. Yesu Kristo ndiye mkate hai-Vs. 52-58.
  • Kristo aliwaeleza Wayahudi kwamba waliokula ile manna jangwani baadaye walikufa mauti.
  • Yesu Kristo ni manna ya uzima wa milele. Tunapo mla Yesu Kristo hatuwezi kufa!! Yeye ni uzima-Yohana 10:28; 4:14.
  • Yesu Kristo ndiye njia, kweli na uzima-Yohana 14:6.

KAZI YA MKATE WA MBINGUNI.

  1. Mkate wa mbinguni huleta wokovu-Vs. 51.
  • Yesu Kristo pekee ndiye wokovu wa mwanadamu-Matendo 16:31; 4:12; Yohana 3:16.
  1. Yesu Kristo yuatosha-Vs. 35.
  • Hakuna kutosheka pasipo Yesu Kristo.
  • Mfalme (Mythology-Greek) Tantalus alihukumiwa huko kuzimu, kwa kuwekwa katika bahari-maji yalifika shina lake, lakini alipojaribu kuyanywa maji, maji yale yalimkwepa. Kichwani mwake kulikuwa na matawi ya matunda tamu, alipojaribu kula yalimkataa-Hivyo alikufa kwa kiu na njaa. Hivyo ndivyo dunia ilivyo.
  • Hatuwezi kushibishwa na walimwengu (“Tantalize”). Yesu Kristo pekee anatosha.
  1. Yesu Kristo ni salama moyoni-Vs. 37-40.
  • Wanao okolewa na Yesu Kristo wamo salama, hawawezi kupoteza kamwe.

MWISHO

  • Yesu Kristo pekee ndiye tumaini kwa dunia yote.
  • Je, umefanya nini na Yesu Kristo?
  • Je, wewe ni salama mikononi mwa Mungu?
  • Yesu Kristo ndiye mkate wa uzima-Amen.
The following two tabs change content below.
Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Latest posts by Rev, DR. Willy Mutiso (see all)

Rev, DR. Willy Mutiso

Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.

Recent Posts

MSAADA WA MUNGU WAKATI WA MATESO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: ZABURI 46:1.   Biblia inatuakikishia kwamba Mungu wetu ni “Msaada…

2 weeks ago

GOD GUIDES OUR DESTINIES.

SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: PROVERBS 3:5-6.   Every destiny is a divine…

2 weeks ago

PUT OFF AND PUT ON

SERIES: THROUGH THE BOOK OF COLOSSIANS. TEXT: Colossians 3:5-10   We have put off the…

2 weeks ago

GOD OF THE BREAKTHROUGHS

SERIES: THE GOD WE SERVE TEXT: 2nd SAMUEL 5:17-20   Breakthroughs are divine interventions that…

4 weeks ago

WHO IS SPEAKING TO YOU?

SERIES: DRAWING NEAR TO GOD TEXT: LAMENTATIONS 3:37 It reminds believers that God's word alone…

1 month ago

CHECHEA MSHINDI ALIYE NDANI YAKO.

MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: 1 YOHANA 5:4.   Wakristo wengi wanaishi maisha ya kushindwa…

1 month ago