MFULULIZO: SAFIRI NA MTUME YOHANA.
SOMO: YOHANA 6:15-21.
Maisha ni mfululizo wa changamoto na shida. Kila wakati pengine uko katika bonde la changamoto hau uko karibu kuingia hau unatoka. Sababu ni kwamba Mungu anakujenga tabia yako, kwa maana kwa Mungu tabia ni maana zaidi kuliko starehe.
Mungu anapenda zaidi utakatifu wako kuliko furaha yako.
Lengo la Mungu kwetu ni kukua katika tabia na kufanana na Yesu Kristo.
Maisha ni kama jinsi reli na line zake mbili, upande moja mema upande mwingine mabaya.
Katika somo letu leo, Yesu Kristo alikuwa amemaliza siku yenye shughuli nyingi mno za huduma nyingi.
Yesu Kristo alikuja kufanya mambo matatu-
Yesu Kristo alikuwa amechoka kweli kweli. Hivyo Kristo aliwaamuru wanafunzi wake wakwee kwenda upande mwingine wa bahari ya Galilaya, lakini Yesu Kristo hakuingia katika chombo na wao.
Walipokuwa katikati ya bahari, bahari ilichafuka sana, dhoruba kuu ikawapata.
Dhoruba ilikuwa kuu kiasi Mathayo anasema ilikuwa kama tetemeko ya ardhi (Sunami). Luka naye anasema dhoruba ilikuwa kubwa kiasi maji yaliingia katika kile chombo.
Hivyo, dhoruba ilikuwa kubwa, maji yakapiga kile chombo, maji yakaingia ndani, chombo kikawa katika kuzama baharini!!
Biblia inasema watu (Wayahudi) walikuwa wanataka kumlazimisha Yesu kuwa mfalme wao (Yohana 6:15).
Wanafunzi wa Yesu walishuka kwenda baharini (6:17) naye Yesu Kristo alipanda mlimani peke yake-6:16.
Wanafunzi tayari waliingia baharini, lakini baada ya maili tatu hau nne (5-6km) dhoruba iliwapata wao (6:19).
Katika dhoruba ndio walimwona Yesu Kristo akitembea juu ya maji akiwajia, wakaogopa sana (6:20).
Yesu Kristo alinena na wao na kuwaambia “ni mimi, msiogope”-6:21 walipokea chomboni kwza furaha, wakafika walipokuwa wanaenda.
Kisa hiki chaonyesha kwamba kuna wakati shida zinakuja ndani ya maisha yetu.
Wakati wa dhoruba za maisha “Je, Yesu Kristo yuko wapi?” kunao kweli tatu juu ya dhoruba za maisha. Hebu tutazame:-
KWANZA, DHORUBA ZINAKUJA KAMA SEHEMU YA KILA MTU.
DHORUBA ZINAKUJA HATA TUNAPOKUWA KATIKATI YA MAPENZI YA MUNGU.
DHORUBA MAANAKE SI ISHARA YA KUTOKUWAKO KWA MUNGU-Yohana 6:16-21.
MWISHO
MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: ZABURI 46:1. Biblia inatuakikishia kwamba Mungu wetu ni “Msaada…
SERIES: THE GOD WHO NEVER FAILS. TEXT: PROVERBS 3:5-6. Every destiny is a divine…
SERIES: THROUGH THE BOOK OF COLOSSIANS. TEXT: Colossians 3:5-10 We have put off the…
SERIES: THE GOD WE SERVE TEXT: 2nd SAMUEL 5:17-20 Breakthroughs are divine interventions that…
SERIES: DRAWING NEAR TO GOD TEXT: LAMENTATIONS 3:37 It reminds believers that God's word alone…
MFULULIZO: MAISHA BILA VIZUIZI. SOMO: 1 YOHANA 5:4. Wakristo wengi wanaishi maisha ya kushindwa…