MFULULIZO: MAISHA NA NYAKATI ZA ELISHA
SOMO: 2 WAFALME 9:1-37; UFUNUO 2:18-29.
Nabii Elisha sasa alikuwa mzee sana. Yehu alipoitaji kupakwa mafuta kuwa mfalme, Elisha alimtumia nabii mwanafunzi kumtawaza Yehu.
Leo tunaangazia mwanamke mwenye uovu mwingi sana Yezebeli. Yezebeli alikuwa mwanamke mwenye ushawishi mkuu katika Israeli yote.
Mume wake Yezebeli alikuwa Ahabu, mfalme wa Israeli. Ahabu naye alikuwa jeuri na mfalme mwovu zaidi katika Israeli.
Pia tuangazie watowashi watatu. Mtowashi ni mwanaume aliye hasiwa. Kuhasiwa ilikuwa desturi ya zamani. Sheria za Musa zilikashifu desturi ya kuhasiwa wanaume. Sheria ya Musa pia ilikataza waliohasiwa kuingia ibada-Kumbu kumbu 23:1; Walawi 22:23-25. Yesu Kristo alisema kuna watowashi, watowashi wanaofanywa watowashi na wanadamu, watowashi wanaojifanya watowashi kwa sababu ya kumtumikia Mungu. Hebu tuone:-
JEZEBELI NA AHABU.
- Kisa cha Yezebeli na Ahabu kinapatikana katika Agano la kale.
- Yezebeli wa Thiatira mtu wa roho na tabia ya Yezebeli.
- Yezebeli alizaliwa na mfalme wa Tyre hivyo Yezebeli alikuwa mzaliwa wa mfalme.
- Amezaliwa katika nyumba ya mfalme, katika mali, pesa na mamlaka.
- Babaye Yezebeli aliabudu Baali mungu wa Kanaani jina lake Ethi-baal (anayefanana na Baali).
- Maanake baali (anaye miliki) possessor.
- Baali aliruhusu mauaji ya kafara na uasherati wa kila namna; kama jinsi miungu ya Waromi na Wagiriki yaani Aphrodite na Venus.
- Ishara ya Baali ilikuwa chombo cha kiume (male sexual organ).
- Ahabu alikuwa mwanaye mfalme wa Israeli aitwaye Omri-1st Wafalme 16:25.
- Yezebeli alipoolewa Israeli aliwaleta manabii 450 kutoka Tyre na manabii 400 wa kike (Ashteroth). Ishara ya Ashteroth ilikuwa chombo cha kike (female sexual organ).
- Katika ikulu ya mfalme Ahabu ilikuwa sherehe kila siku.
- Yezebeli alichukua utawala wa Israeli watu milioni kumi, isipokuwa watu 7001-1st Wafalme 16:33.
- Yezebeli alisimamia mauaji ya Nabothi, na kumnyang’anya shamba lake-1st Wafalme 21:19-23.
- Maadui wa Yezebeli walikuwa manabii ya Yehova.
- Yezebeli alichukia sana neno la Yehova, kutubu dhambi, kumnyenyekea, haki na ukweli-1st Wafalme 18:20-40.
- Nabii Eliya alisimama peke yake. Manabii wote walikuwa wametoweka, wengine wengi walikuwa wamekufa.
- Eliya alikuwa nabii wa nguvu, lengo na kujitoa. Watu kama Eliya wameandikwa katika Waebrania 11:33-40.
- Eliya alimfahamu Mungu wa miujiza, ishara na maajabu.
- Eliya alimfahamu Mungu anayejibu kwa moto. Eliya aliwamaliza m manabii wote wa Baali kwa upanga!!
HUKUMU NA REHEMA ZA MUNGU-1st Wafalme 19:1-2.
- Yezebeli hakuwa juu ya mlima Karmeli siku ya mashindano ya Baali na Yehova.
- Yezebeli mwenyewe hakuona mto kutoka mbinguni, lakini manabii wake wote walikufa hapo.
- Ahabu alikuwa mtu mbaya zaidi, lakini Yezebeli alikuwa hodari zaidi katika dhambi zake.
- Ahabu ni picha nzuri ya viongozi wanao tazama maovu yakitendeka bila kuchukua jukumu kuzuia maovu.
- Dhambi inampeleka mtu mbali zaidi ya jinsi alipenda kwenda. Dhambi inaweka mtu muda zaidi ya jinsi alipanga kukaa. Dhambi inagharimu mtu zaidi ya jinsi yuko tayari kulipa!!
- Ahabu alienda mbali zaidi, akakaa zaidi, akalipa zaidi katika uongozi wa Yezebeli. Ahabu hakutenda lolote lile.
YEZEBELI WA THIATIRA-Ufunuo 2:18-19.
- Yezebeli wa Thiatira alikuwa ni roho yake Yezebeli.
- Roho ya Yezebeli ni roho anaye chukua mamlaka ya kiroho kinyume na kuleta roho bandika.
- Wakati wa Yohana Batizaji, kulikuwa na Herode na mke wake Herodiasi.
- Herodiasi alikuwa ndiye mwenye kusema.
- Roho ya Yezebeli inaweza kutokea mahali popote, hata aka nisani.
- Kanisa ya Thiatira ilikuwa kanisa nzuri, Matendo yao yalikuwa mema sana, lilikuwa kanisa ya upendo na imani.
- Ibada zake zilikuwa za nguvu na watumishi wote walikuwa wazuri lakini mwanamke Yezebeli alichukua uongozi wote, uchungaji ulikuwa katika mikono na Yezebeli wa Thiatira.
- Roho ya Yezebeli ni roho ya kudhibiti, kukalia (control and manipulate).
- Roho ya Yezebeli ni roho ya uchawi.
- Roho ya Yezebeli si kwa wanawake pekee, bali ni roho inayowapata wanaume pia.
- Roho ya Yezebeli inaweza kujia waimbaji, viongozi wa ibada, wazee wa kanisa, nabii na mchunhaji.
- Shetani alikuwa na roho ya Yezebeli ndivyo alitimuliwa mbinguni-Isaya 14.
YEHU NA WATOWASHI-2 Wafalme 9:30-33.
- Yehu alikuwa mfalme wa kumi (10) katika Israeli.
- Yehu alikuwa mtu mwema, kutekeleza haki katika Israeli.
- Siku moja Yehu alikuja kwa nyumba ya Yezebeli.
- Yezebeli aliweka wanja machoni mwake na kupamba kichwa chake vizuri, akachungulia dirishani.
- Yezebeli kwa kujitoa sana alipenda sana kumkatia Yehu.
- Lakini Yehu hakuwa kama wanaume wengine, hakumtamani Yezebeli, hakumweshimu au kumwogopa.
- Ndipo Yehu akauliza “aliye upande wangu ni nani?”
- Watowashi watatu waliosikia sauti ya Yehu walimtupa Yezebeli chini kupitia kwa lile dirisha.
- Hawa watowashi wameumizwa na Yezebeli, hakuwa na chochote mpaka kitambulisho chao. Waliitikia Yehu “sisi tuko upande wako.”
- Yezebeli alikufa, damu yake ikamwagika, nyingine juu ya ukuta na nyingine juu ya farasi naye Yehu akamkanyanga-kanyanga.
- Hivo roho ya Eliya ikachipuka ndani ya wale watowashi-maisha na enzi yake Yezebeli ikakwisha Israeli.
- Je, hizi ni siku za Eliya?
UPAKO WA YEHU-2 Wafalme 9:1.
- Elisha alimpa mmoja wa wanafunzi nabii maagizo ya kumtawaza Yehu.
- Vs. 1 chukua chupa hii ya mafuta mkononi mwako ukaende Ramothi-Gileadi.
- Vs. 2 ukifika huko mtafute Yehu mwana wa Yehoshafati mwana wa Nimshi.
- Mchukue mpaka chumba cha ndani.
- Vs. 3 mimina juu ya kichwa chake Yehu na kusema Bwana asema hivi, nimekutia mafuta uwe mfalme juu ya Israeli.
- Vs. 4 kijana nabii alipofika Ramothi Gileadi alimpata Yehu, akamtawaza kuwa mfalme kwa neno la Mungu, kisha akakimbia akaenda zake mbio.
- Vs. 11 watu wa Mungu hawapewi heshima. Nabii wa Mungu anaitwa “Mwenye wazimu.”
- Yehu ameingizwa kuharibu kabisa jamii ya Ahabu na Yezebeli-V. 8.
- Yehu pia akamuua Ahazia.
- Mwili wa Yezebeli uliliwa na mbwa ukatimia unabii wa Eliya.
MWISHO.
- Dhambi ya Ahabu ilikuwa kufunganishwa katika ndoa pamoja na Yezebeli. Ahabu alimpa mke wake Yezebeli uongozi, kiasi Yezebeli akaleta miungu na Baali na Ashterothi-1 Wafalme 17, 18, 21.
- Dhambi ya Yezebeli -1 Wafalme 19, 21.
- Kuwaua manabii wa Yehova, kumuua Nabothi-2 Wafalme 9:36.
- Kuhidhinisha ibada za sanamu Israeli.
- Kukalia wanawe Joramu na Ahazia.
- Yehu alisimamishwa na Mungu kuleta hukumu juu ya nyumba ya Ahabu.
- Kazi ya Elisha inaanza kufika tamati.
- Mungu hapendi dhambi.
The following two tabs change content below. Rev, Dr. Willy Mutiso is the Senior Pastor at First Baptist Athiriver. He is widely known for his practical and dynamic teaching style which helps people apply the timeless truths of Scripture to their everyday lives.